Vijana tuchangamke kabla jua halijazama

Vijana tuchangamke kabla jua halijazama

Aurora

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2014
Posts
7,308
Reaction score
5,276
Za jumapili wana JF,

Naona baadhi ya watu wazima wanaofanya kazi za kuajiriwa hadi uzeeni. Mtu anakaribia 60's lakini bado anaamka alfajiri kuwai kibaruani au hata kupelekeshwa na wakubwa wake wa kazi hata kama amewazidi umri.

Wengine wanadiriki hata kuomba kuongezewa mkataba wa ajira hata kama ameshafikisha 60.

Vijana wenzangu inabidi tuone mbali mapema, hasa kwa walioajiriwa, tufanye kazi kwa malengo, wekeza vya kutosha, fungua miradi yako, by the time of 40's unafanya mambo yako.

Nawatakia jumapili njema
 
Tatizo lingine, wanatafuta kazi wanakuja kupata karibia na umri wa kustafu, wafanyeje sasa.
 
Umeongea vyema sana na nimependa range ya umri ulioutaja maana mpaka 40 inawezekana kabisa uwe umeshajipanga,tnx ni ushaur mwema sana na wa kuuzingatia
 
Za jumapili wana jf

Naona baadhi ya watu wazima wanaofanya kazi za kuajiriwa hadi uzeeni...mtu anakaribia 60's lakini bado anaamka alfajiri kuwai kibaruani au hata kupelekeshwa na wakubwa wake wa kazi hata kama amewazidi umri...

Wengine wanadiriki hata kuomba kuongezewa mkataba wa ajira hata kama ameshafikisha 60....

Vijana wenzangu inabidi tuone mbali mapema,hasa kwa walioajiriwa,tufanye kazi kwa malengo,wekeze vya kutosha,fungua miradi yako....by the time of 40's unafanya mambo yako....

Nawatakia jumapili njema

ahsante sana kwa ujumbe mzuri na kutukumbusha, ila tunatakiwa kuanza trial n error before kugonga 40,
unaeza hata ukipiga kazi ndani ya miaka 5. ukiwa na malengo unakuwa tayari unafanya kazi huku unamiradi inaendlea...
 
Umeongea vizuri sana mleta mada, ila sasa kwa wengine kunakuwa na situations ambazo ndio humpelekea kuwa hivyo (kushindwa kuwekeza).Mathalan kuna wengine anaanza serikalini, ameanza katika 30s let say hapo ana BA yake so scale yake ni D1. Hapo take home yake 470,000/=. Hajalipa kodi hapo kwa sehemu kama Dar, bado nauli daily (hapo anaishi Gongo la Mboto).ukirudi nyumbani wanajua umefika chuo kikuu na unafanya kazi Dar basi wao kila siku wanakutangazia dhiki. Unawapa, si umetumia nawe nguvu zao? Life linasonga. Hapo ukicheki mileage inasoma, unaamua kuoa... Uuuwi! Majukumu yameongezeka...mwisho wa siku unajukuta at point zero hata kufungua kibanda cha vocha huwezi.So wengine wanashindwa kutokana na sababu zingine nje ya uwezo wao.binafsi siungi mkono kushindwa kwao hata kidogo na wala sifurahii mtu kuwa mtumwa wa mwingine ila ndio hali tu ya maisha.Mwisho kabisa nakupa big up mtoa mada kwa kuleta uzi mzuri hivi jumapili yavleo
 
Za jumapili wana JF,

Naona baadhi ya watu wazima wanaofanya kazi za kuajiriwa hadi uzeeni. Mtu anakaribia 60's lakini bado anaamka alfajiri kuwai kibaruani au hata kupelekeshwa na wakubwa wake wa kazi hata kama amewazidi umri.

Wengine wanadiriki hata kuomba kuongezewa mkataba wa ajira hata kama ameshafikisha 60.

Vijana wenzangu inabidi tuone mbali mapema, hasa kwa walioajiriwa, tufanye kazi kwa malengo, wekeza vya kutosha, fungua miradi yako, by the time of 40's unafanya mambo yako.

Nawatakia jumapili njema

Mama tuanze na wewe, sijui umejipangaje mpaka sasa hivi? Hivi wewe siyo mmoja wa wale wanaomaliza chuo kikuu na kuanza kulilia ajira badala ya kutumia elimu yao kujiajiri? Hivi ukipata kazi serikalini hayo unayoyasema utayaweza kweli? Labda kama utakuwa fisadi! Unaujua mshahara wa graduate? Chezea ccm wewe!! Kama unataka salama anzieni huko huko chuoni kutafakari jinsi mtakavyoepuka utumwa wa kuajiriwa, kama mnapata elimu ambayo itawawezesha kujiajiri ni bora mkaanza huko huko bila kutafuta kuajiriwa, maana mpaka uje uipate hiyo kazi tayari umegonga 35. Hapo kuna kuolewa na kuoa (ukishaingia huko na 35 yako ndo kwishney kabisa) hapo 50 lazima igonge tu utake usitake!!

Nawahurumieni sana vijana sasa hivi mmeanza kupiga ndogo ndogo eti kazi za umma ziwe za mikataba ya miaka 3 kwa vipindi viwili, sasa hiyo fedha ya kukutoa mpaka uanzishe miradi ya kujiajiri iko wapi? Hapa tunafuga mafisadi, ufisadi unaanzia huko huko chuoni kwa kudanganyana hivi hivi, maana hapo jamaa akipewa uhasibu ni kupanga kufisadi tu ili atoke kiamaisha haraka haraka!!
 
na Mungu atusaidie kuyakumbuka haya maneno yako...ulichokisema kinaukweli %100

Kwa scale ya mshahara ulotaja hapo ni dalili kuwa ni muajiriwa wa serikali,kwahiyo ww chukuwa mkopo wa miaka 5-10 kiwango cha mkopo kuanza 20-50mil nadhani apo Ndio utatoka ila Lengo ni kuanzisha mradi n sio kununua gari
 
Ni kwelu kabisa mi naona ikifika 45 hamna haja ya kuendelea na utumishi wa umma ni mda wa kujiajiri ila tatizo ni majukumu sisi waswahili tunazaana sana unakuta mtu 55years bado anawatoto wako std 4 mwingine std 7 mwingine form 2 sasa mpaka hao watoto waje wamalize chuo si unakuta umesha gonga 60 na ushee na hela ya kiinua mgongo yote imekwisha na hiyo kanuni mpya ya mafao ikipitishwa ndiyo itakuwa balaaa zaidi,haya bado extended families mara sijui michango ya harusi,sijui kipaimara sijui kibeseni yaani ni sheeeeedah
 
  • Thanks
Reactions: lin
Back
Top Bottom