Vijana njooni tujifunze kitu

Vijana njooni tujifunze kitu

ilaz

Senior Member
Joined
Jul 13, 2017
Posts
100
Reaction score
61
Tuko vijana wawili wote ni waajiriwa wa serikalini na wote tulianza kazi mwaka 2012. Mwaka mmoja baada ya kuanza kazi kila mtu alikuwa na ndoto za maisha yake, mimi nilikuwa ni mwoga wa maisha na mwenzangu alikuwa mtu wa kutake risk.
MIMI
Nilikopa 10mill benki ya NMB na mwenzangu alinishawishi sana niingie kwenye kilimo ila moyo wangu haukuwa tayari kwa kipindi kile. Nilichukua milioni 10 kama ilivyo na kuizika kwenye ujenzi kiwanja tayari nilikuwa nacho. milioni 1 nilimalizia deni la kiwanja na iliyobaki ilianza ujenzi. Kilichotokea hela yote iliisha na ujenzi haukufika popote. Ziliisha kwenye msingi na kupandisha kozi nne tu za tofali. Milioni 9 yote niliizika chini, kuna muda nikienda site huwa nakaribia kulia nikiangalia matofali.

MWENZANGU
Alikopa milioni 6 benki ya CRDB akaipeleka kwenye kilimo cha nyanya mkoani Morogoro. Mwaka wa kwanza alianza na ekari 3. Hapa alivuna kipindi kizuri ambapo bei ya nyanya ilikuwa juu akatengeneza hela ya kutosha. Msimu uliofuatia alilima ekari 6 ili kuongeza faida zaidi.
Tatizo lilipoanza:
hizi nyanya alivuna kwenye msimu mbovu sana ambapo masoko yote DSM yamejaa malori ya nyanya. Hapa dalali anaringa mpaka umnyenyekee. Nusu ya nyanya aliuza kwa bei ya hasara na nusu nyingine ziliozea sokoni ikabidi zikose soko.
Jamaa hakukata tama, kaingia tena benki kutop up mkopo ili arudi tena kwenye kilimo kaongeza milioni 3. Kalima ekari 4.
Tatizo jengine likajitokeza:
Karibia miezi miwili tu baada ya kupanda akapokea simu kutoka mfanyakazi wa shambani kwake kuwa wamasai wameingiza ng'ombe shambani na kula miche yote ya nyanya. Siku inayofuata kapanda basi asubuhi hadi shambani kufika anasema machozi yalimtoka kuona jinsi ng'ombe walivyoshambulia shamba lake vimebaki vipisi tu. Kapeleka kesi polisi maana mwenye mifugo anajulikana. Kilichofuatia ni longo longo za polisi na kalenda za njoo baada ya wiki moja mara siku ukienda sijui aambiwe askari anaeshughulikia kesi yake kasafiri. Kumbe mmasai ameshatoa hongo kwa mkuu wa kituo. Jamaa anachoma anauli DSM-Moro kula, kulala akaona hapa ntazidi kufilisika kaachana na kesi.
Hadi leo hii hajakaa vizuri kimaisha.
Sasa hivi wote tunaugulia maumivu ya makato ya benki na wote hatujafikia malengo yetu.
USHAURI
Ukitaka kuanza jambo lolote pia jipange kwa lolote.
 
hahahahahahahahahaha Somo la Hadithi yako imenifanya nichekeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Ukikopa hela bank usiitumbukize yote kwenye kilimo.

Kilimo ni kama kamari kiwe umwagiliaji au kinachotegemea mvua.
 
Kilimo cha kungoja mvua sio sustainable.

Mo anasema hela iko shambani muulize yeye analima wapi, shamba lake liko wapi?
 
Tuko vijana wawili wote ni waajiriwa wa serikalini na wote tulianza kazi mwaka 2012. Mwaka mmoja baada ya kuanza kazi kila mtu alikuwa na ndoto za maisha yake, mimi nilikuwa ni mwoga wa maisha na mwenzangu alikuwa mtu wa kutake risk.
MIMI
Nilikopa 10mill benki ya NMB na mwenzangu alinishawishi sana niingie kwenye kilimo ila moyo wangu haukuwa tayari kwa kipindi kile. Nilichukua milioni 10 kama ilivyo na kuizika kwenye ujenzi kiwanja tayari nilikuwa nacho. milioni 1 nilimalizia deni la kiwanja na iliyobaki ilianza ujenzi. Kilichotokea hela yote iliisha na ujenzi haukufika popote. Ziliisha kwenye msingi na kupandisha kozi nne tu za tofali. Milioni 9 yote niliizika chini, kuna muda nikienda site huwa nakaribia kulia nikiangalia matofali.

MWENZANGU
Alikopa milioni 6 benki ya CRDB akaipeleka kwenye kilimo cha nyanya mkoani Morogoro. Mwaka wa kwanza alianza na ekari 3. Hapa alivuna kipindi kizuri ambapo bei ya nyanya ilikuwa juu akatengeneza hela ya kutosha. Msimu uliofuatia alilima ekari 6 ili kuongeza faida zaidi.
Tatizo lilipoanza:
hizi nyanya alivuna kwenye msimu mbovu sana ambapo masoko yote DSM yamejaa malori ya nyanya. Hapa dalali anaringa mpaka umnyenyekee. Nusu ya nyanya aliuza kwa bei ya hasara na nusu nyingine ziliozea sokoni ikabidi zikose soko.
Jamaa hakukata tama, kaingia tena benki kutop up mkopo ili arudi tena kwenye kilimo kaongeza milioni 3. Kalima ekari 4.
Tatizo jengine likajitokeza:
Karibia miezi miwili tu baada ya kupanda akapokea simu kutoka mfanyakazi wa shambani kwake kuwa wamasai wameingiza ng'ombe shambani na kula miche yote ya nyanya. Siku inayofuata kapanda basi asubuhi hadi shambani kufika anasema machozi yalimtoka kuona jinsi ng'ombe walivyoshambulia shamba lake vimebaki vipisi tu. Kapeleka kesi polisi maana mwenye mifugo anajulikana. Kilichofuatia ni longo longo za polisi na kalenda za njoo baada ya wiki moja mara siku ukienda sijui aambiwe askari anaeshughulikia kesi yake kasafiri. Kumbe mmasai ameshatoa hongo kwa mkuu wa kituo. Jamaa anachoma anauli DSM-Moro kula, kulala akaona hapa ntazidi kufilisika kaachana na kesi.
Hadi leo hii hajakaa vizuri kimaisha.
Sasa hivi wote tunaugulia maumivu ya makato ya benki na wote hatujafikia malengo yetu.
USHAURI
Ukitaka kuanza jambo lolote pia jipange kwa lolote.
[emoji121]
MKOPO SIO KITU CHEMA,
INGAWA NI KITU CHEMA.

[emoji377] [emoji124] [emoji469] [emoji377] [emoji124] [emoji469] [emoji377] [emoji124] [emoji469]
 
Sasa ndio manini haya umeandika?? Kwa akili za makande kama hizi ata upewe dola 100,000 hutotoboa ww
 
Umenikumbusha machungu ya shama la matikiti yangu yalivyo vamiwa na ng’ombe, Bahati nzuri sikukopa bank...
Kuna mambo yanaumaa acha tu mkuu,
Poleni sana mjipange upya
 
kuna watu wanasema hela ipo shamba ni kweli lakini inabidi mtu ujipange haswa.
 
na hili ndio
Kilimo cha kungoja mvua sio sustainable.

Mo anasema hela iko shambani muulize yeye analima wapi, shamba lake liko wapi?
tatizo kubwa wengi tunalima kwa kutegemea mvua, tunapanda kwa pamoja na kuvuna kwa pamoja matokeo yake sokoni tunakutana kwa pamoja.
 
Sasa ndio manini haya umeandika?? Kwa akili za makande kama hizi ata upewe dola 100,000 hutotoboa ww
nimepata funzo kutoka kwa jamaa, nami nikiamua kuingia kwenye kilimo najua nianzie wapi
 
Kilimo cha kungoja mvua sio sustainable.

Mo anasema hela iko shambani muulize yeye analima wapi, shamba lake liko wapi?
Mwenzako analima KATANI, wewe unalima NYANYA ?
 
Tuko vijana wawili wote ni waajiriwa wa serikalini na wote tulianza kazi mwaka 2012. Mwaka mmoja baada ya kuanza kazi kila mtu alikuwa na ndoto za maisha yake, mimi nilikuwa ni mwoga wa maisha na mwenzangu alikuwa mtu wa kutake risk.
MIMI
Nilikopa 10mill benki ya NMB na mwenzangu alinishawishi sana niingie kwenye kilimo ila moyo wangu haukuwa tayari kwa kipindi kile. Nilichukua milioni 10 kama ilivyo na kuizika kwenye ujenzi kiwanja tayari nilikuwa nacho. milioni 1 nilimalizia deni la kiwanja na iliyobaki ilianza ujenzi. Kilichotokea hela yote iliisha na ujenzi haukufika popote. Ziliisha kwenye msingi na kupandisha kozi nne tu za tofali. Milioni 9 yote niliizika chini, kuna muda nikienda site huwa nakaribia kulia nikiangalia matofali.

MWENZANGU
Alikopa milioni 6 benki ya CRDB akaipeleka kwenye kilimo cha nyanya mkoani Morogoro. Mwaka wa kwanza alianza na ekari 3. Hapa alivuna kipindi kizuri ambapo bei ya nyanya ilikuwa juu akatengeneza hela ya kutosha. Msimu uliofuatia alilima ekari 6 ili kuongeza faida zaidi.
Tatizo lilipoanza:
hizi nyanya alivuna kwenye msimu mbovu sana ambapo masoko yote DSM yamejaa malori ya nyanya. Hapa dalali anaringa mpaka umnyenyekee. Nusu ya nyanya aliuza kwa bei ya hasara na nusu nyingine ziliozea sokoni ikabidi zikose soko.
Jamaa hakukata tama, kaingia tena benki kutop up mkopo ili arudi tena kwenye kilimo kaongeza milioni 3. Kalima ekari 4.
Tatizo jengine likajitokeza:
Karibia miezi miwili tu baada ya kupanda akapokea simu kutoka mfanyakazi wa shambani kwake kuwa wamasai wameingiza ng'ombe shambani na kula miche yote ya nyanya. Siku inayofuata kapanda basi asubuhi hadi shambani kufika anasema machozi yalimtoka kuona jinsi ng'ombe walivyoshambulia shamba lake vimebaki vipisi tu. Kapeleka kesi polisi maana mwenye mifugo anajulikana. Kilichofuatia ni longo longo za polisi na kalenda za njoo baada ya wiki moja mara siku ukienda sijui aambiwe askari anaeshughulikia kesi yake kasafiri. Kumbe mmasai ameshatoa hongo kwa mkuu wa kituo. Jamaa anachoma anauli DSM-Moro kula, kulala akaona hapa ntazidi kufilisika kaachana na kesi.
Hadi leo hii hajakaa vizuri kimaisha.
Sasa hivi wote tunaugulia maumivu ya makato ya benki na wote hatujafikia malengo yetu.
USHAURI
Ukitaka kuanza jambo lolote pia jipange kwa lolote.
upuuzi wa kilimo me siutaki kabisa,nimetelekeza ekari kumi zangu kimanzichana mpaka leo
 
Wengine tunajua riba ni mbaya kwa hiyo huwa hatuhangaiki na mikopo kwani tulishaambiwa ni mbaya.

Bora mgefungua joint account na kudunduliza mpaka hapo mkaona sasa tunaweza fanya kitu cha maana.

Pia kwa muda huo mngekuwa na plan nyingi kabla ya kuizika chini.
Hapo la kujifunza ni kuwa mkopo hauna faida kabisa zaidi ya maumivu.
Poleni sana
 
Back
Top Bottom