Nilidhani mtoa mada angetoa somo la vijana kujikwamua kiuchumi kutoka katika lindi la umaskini unaokua kila siku. Sijaona popote ambapo mtoa mada amekuwa "objective" katika kuonesha jinsi gani kijana wa kijijini asiyekuwa na elimu ya chuo kikuu anaweza kunufaika na uwepo wa ccm. Mtoa mada anazungumzia "the privileged few" kama yeye ambao ni sehemu ndogo sana ya vijana wa nchi hii "and very unfortunately" ni vijana wa "class" ya juu na wala sio ile ya kati au ya chini. "Unless" anifafanulie tena alichotaka kuandika "otherwise" hakuna hoja yenye mashiko hapa.