Vijana Njooni CCM, ndoto zenu zitatimia

Paul Makonda

Member
Jul 8, 2011
97
186
Vijana Njooni CCM,

nyerere na vijana.jpg


Miongoni mwa sifa ambazo Chama Cha Mapinduzi kimejipambanua nazo katika Nyanja za kimataifa na kitaifa ni pamoja na utaratibu na mfumo bora wa uendeshwaji wake, kwamba ni Chama kilicho kamili katika muundo wake, misingi yake, kanuni na taratibu zake. Lakini pamoja na hayo CCM inayo historia iliyotukuka si tu ya kuikomboa TANZANIA kutoka katika mikono ya wakoloni lakini pia kusaidia mataifa mengine ya kusini mwa jangwa la Sahara.

jerry + jk.jpg


Chama Cha Mapinduzi, pamoja na mambo mengine bora, kimetimia vyema katika muundo wake kwa kuwepo kwa jumuiya imara zinazoishikilia na kuipa nguvu kila Uchao. Ipo jumuiya ya Vijana ambayo lengo kuu la Kuundwa kwake ni kuhakikisha kuwa Chama na Taifa linaandaa na kulea Viongozi wake wa kesho. Ni chama cha Mapinduzi pekee miongoni mwa vyama vyetu vya siasa hapa nchini ambacho kina “Sera ya malezi ya Vijana” iliyotungwa tangu 1981 na kuendelea kufanyiwa review mpaka sasa.

jakaya na jk.jpg


Vijana ndani ya Chama Cha Mapinduzi wanamatumaini Zaidi na wanaandaliwa na kusafishiwa njia ya mafanikio yao kwa mapenzi na weledi wa Viongozi. Tabia hii ya viongozi wa CCM kuwaandaa Vijana makini na kuwatengezea mazingira kwa kuwalea na kuwadhibiti katika matendo na mienendo ndio ambayo inakihakikishia Chama hiki Uhai wa miaka mingine 50 na hata Dahari. Ni wazi leo ukiwaangalia Vijana ndani ya CCM unaona picha ya Viongozi bora wa kitaifa wa Miaka 20 ijayo, ukiomuona JANUARY, NAPE, JERRY, n.k unaona picha ya Viongozi bora wa baadae tofauti na ukiangalia wenzetu SUGU, LEMA., NASSAR etc unaona kiza na wingu zitto.

jk + nape.jpg


Tofauti na vyama vingine, CCM ukiwa kijana una-reside your right of trial and error, kwa maana tumeshuhudia Vijana wengi ambao walikosea lakini wanapewa nafasi na kuwa Viongozi wakubwa na wazuri baadae, mifano hii iko mingi, binafsi nimewahi kufanya makosa lakini niliitwa na kuonyeshwa njia, na nilifanyiwa hayo sio kwa sababu mimi ni msukuma ama ------, kwa sababu kwenye Chama Chetu Usukuma ama ukwere sio sifa ya kuwa kiongozi kwa maana sikuangaliwa kabila langu ili niadhibiwe ama nisamehewe. KABILA halimbebi mtu ndani ya CCM.

JM2.jpg


Ipo siku niliitwa na Mzee wangu KINGUNGE NGOMBALI na akawa ananifundisha darasa la ITIKADI, tukaendelea na mjadala nikamuuliza ameweza vipi kuwa kiongozi mkubwa na mwenye heshima ya kipekee ndani ya Chama hali yeye haamini katika DINI yeyote.,akanijibu kwa ufupi na ufasaha kuwa DINI ya mtu sio sifa ya kuwa KIONGOZI ndani ya CCM. Kwenye CCM kila kijana na kila kiongozi ana sifa sawa na wengine, hakuna aliye mbora mbele ya wenzake, vipo vigezo vinavyotumika kumpata kiongozi, sio lazima uwe PADRI ama MCHUNGAJI ndio uonekane unafaa kuwa kiongozi ndani ya Chama, kwetu sisi DINI ya mwanachama sio sifa ya kuwa bora kwa wengine.

nyerere - mkapa.jpg


Nitoe wito kwa Vijana wenzangu kuuona ukweli huu na kuufuata, ufike wakati Vijana wajiandae na waandaliwe kuwa Viongozi Bora wa Kizazi Chao. Njooni CCM ambako ndoto zenu zitatimia, michango, uwezo na mawazo yenu itathaminiwa. Njooni ambako mtaonyeshwa njia ambayo mtakuwa tayari kuifata.

MWENYEZI MUNGU AWABARIKI NA AWAONGOZE KATIKA NJIA YA SAWASAWA.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

Vivaa Vijana Vivaaa…!!!
 
kwani miaka yote vijana walikuwa wapi kama si ndani ya CCM inayoongoza nchi hii tangu uhuru na je kwa nini ndoto zao bado ni giza totoro? Ushauri wangu kwa vijana ambao tumeshaona nuru basi tuikimbilie huko huko iliko lakini kuendelea kuwa ndani ya CCM ni sawa na kukubali kuendelea kujifunika blanketi jeusi wakati kumeshakucha kitambo!!
 
Tumekusoma Mh. Makonda, ila naomba unitoe dukuduku kwenye maswala kadhaa:
(i) Kwani ndani ya chama chetu, vijana ni mpaka umri gani?
(ii) Hivi uchaguzi wa kuwapata wagombea kuanzia Arumeru Mashariki, Kalenga na sasa Chalinze, je yalifuatwa hayo uliyoyaainisha?
(iii) Hapo kwenye neno "wingu Zitto" je ni typo erra ama ulikusudia kufukisha ujumbe fulani?
(iv) Katika viongozi wa miaka ishirini ijayo, umemuacha Ridhiwani kwa makosa ama makusudi?
(v) Wewe ndani ya chama upo kambi gani?

Ni hayo tu kwa leo Mh. Paul Makonda.
 
mbona sisi wazazi wetu hawakuwahi kuwa viongozi wa ccm ? Hicho si ni chama cha WAKE NA WATOTO WA VIONGOZI ! wewe tunafahamu kwamba umefaidika na makundi yaliyomo ,je unataka na sisi tuingie kwenye siasa zenu za majitaka ?
 
Nilikuwa sikui kuwa kumbe bado kuna wasukuma wajinga namna hyo. We ni msukuma gani mwenye akili za kushikiwa?
 
Wewe kweli mwizi wa simu, kwani miaka yote vijana walikuwa wapi, na hao waliopo sasa mmewafanyia nini?umetoa mifano ya kina Makamba, unamaanisha CCM haina cha kukufanyia usipokuwa mwanasiasa?unajua umuhimu wa vijana kuwa na mawazo yanayokinzana?

Mkuu usimbishie huyo jamaa. Anamaanisha vijana waende CCM WAKAFAIDI. Wale wanye majina ya wakubwa watapewa nafasi ila wale wasio na majina watatumika kama viburudisho.

ImageUploadedByJamiiForums1394617762.185189.jpg

ImageUploadedByJamiiForums1394617905.460639.jpg

ImageUploadedByJamiiForums1394617947.373393.jpg



Sent from my iPad using JamiiForums
 
Uko sahihi sana sugu lema wenje huwezi sema ni viongozi wa kesho

Mm Nina kaushauri kwako kihistoria kama vile sita na Lowasa hawaelewani kwanini wewe ni rafiki wa sita na umekuwa ukimsakama lowasa kwanini ukubali kutumiwa na wazee wakati wanamaugomvi yao ?

Simpendi samweli sita maana ndiye alianzisha agenda ya ufisadi na kukiharibia chama mpaka kukipunguzia umaarufu Wake tunaitwa mafisadi kwasababu ya sita

Simpendi lowasa maana tuhuma anazotuhumiwa nazo nikama ni za kweli maana hizi pesa anazogawa katoa wapi pia Lowasa na ROSTAM wameua uzalendo ndani ya ccm na kufanya chama kifanye kazi kwa shida uchaguzi watu wamezoe ccm wanagawapesa kisa lowasa na Rostam
 
Kweli Makonda una upeo finyu sana wa kufikiri. Yaani unazungumzia vijana kama January Makamba, wakati amepanda ngazi kwa mgongomwa babaake Yusuf? Hujui kuwa siku hizi CCM imebaki kurithisha vijana wao madaraka? Leo Makamba kambeba mwanaye Bumbuli, mara JK kamtuma Ridhiwani Chalinze, mara watoto wa vigogo wamejazwa ndani ya NEC na BOT. Hiyo ndio dira ya vijana kwa CCM?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom