VIJANA na SIASA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VIJANA na SIASA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Exaud J. Makyao, Feb 9, 2010.

 1. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2010
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sioni vijana (kati ya miaka 20 - 30) wakipata nafasi muhimu katika siasa za nchi zetu za Afrika.
  Nafasi nyingi za juu za kisiasa zimekaliwa na wazee walioshiba miaka.
  Hii ina maana kwamba vijana hawana uwezo kuongoza siasa za nchi zetu?
  Kuna watu hudai kuwa vijana hawana hekima ya kutosha katika kufanya maamuzi makubwa ya kitaifa.
  Kwa kuzimulika nchi za Afrika Mashariki TANZANIA, KENYA na UGANDA,sijui ukweli ukoje hapa wakuu.
  Natoa hoja.
   
 2. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  vijana ni wavuta bangi....................................

  source: mh. wasira
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Hivi kumbe A.Mashariki ina nchi hizi..!

  Vijana wanafaa kutumikia taifa lao kwa kaajili ya nguvu walizo nazo zaidi, lakini si kwenye ngazi za juu za maaamuzi, MAANA HUKOWATAKOROGA.

  Ni ukweli uliositirika kwamba maamuzi mengi ya vijana yana mwelekeo wa jazba na uharaka usio na maana!

  Ukiamua kuingiza vijana kwenye ngazi za maamuzi, lazima wawe na back-up ya nguvu kabisa ya wazee.

  Ukiona Mbunge kijana sana ujue kwamba amechaguliwa na kundi la vijana wenye hasira ya maisha, ambao wanadhani kijana mwenzao atawaelewa hatraka na kuwasaidia.

  My take-
  Vijana wawe groomed kushika nafasi za uongozi, na si kutoka masomoni au uraiani direct na kuwa viongozi. Mifano ni kama ya akina JK, ambao wamekulia kwenye Siasa!
   
 4. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2010
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  My loard.
  Hii ni kweli?
   
 5. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2010
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mkuu PakaJimmy,
  Hoja zako hizi haziwezi kupita bila kuchambuliwa.
  Ngoja wadau wazipitie kwanza.
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Feb 9, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Exaud, thanks for bringing this into our attention

  To be honest, vijana hawana mpango na siasa in real life, wengi tunaishia kulalamika kuandika

  But the same vijana wahamasishaji wazuri kabisa wa michango ya harusi!!. Kijana akimaliza chuo kapata kazi Zain na ka take home kake ka laki sita, CRDB wakimpa mkopo wa gari , utamtaka??

  Kuridhika ndio kumetuponza, na katika dunia ya survival of fittest na ubepari achilia mbali ubinafsi, jamaa wanaitumia nafasi hiyo hiyo kutuburuza.

  The situation is even worse kwa graduates wetu, they simply hate politics starting form their respective colleges, ukitaka ushahidi uliza uchaguzi kwa mfano wa DARUSO-udsm ni wanafunzi wangapi huwa wanapiga kura?

  Miaka ya zamani vijana kwa mfano vyuoni ndio walikuwa mstari wa mbele katika kila kitu ikiwamo kuleta productive challenges kwa serikali

  Exaud nadhani inabidi uombe sana mpendwa!
   
 7. F

  FM JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2010
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hao wazee unaowaona katika siasa sasa hivi, walianza wakiwa vijana. Nadhani issue hapa si kwamba vijana hawahusishwi, pengine vijana wengi wa umri huo sasa hivi hawajihusishi na siasa.
   
 8. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2010
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  WABEROYA,
  Kwa mawazo haya, nasikitika kwanini vijana wamekuwa na image hii.
  Hii ni sawa kweli au kuna mahali vijana wameharibiwa?
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  Feb 9, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Tumeridhika, hakuna shida Tanzania. Ni nchi ya maziwa na asali! na hakuna wa kufumbua macho haya mpaka upate shida halau ndio Tunailaumu serikali.

  debate hamna mashuleni, viongozi hawana inspiration kwa wanafunzi, maprofessor pia hawana mvuto, mtu ku-waza leo awe kama Kikwete si ataugua kichaa, Lakini kuwaza uwe leader kama akina Obama ni rahisi kuliko JK!

  Dhana ya zidumu heshima za mwenyekiti nazo zimeliangamiza taifa, viongozi hawana uwezo wa kukaa na ku-debate na wanaowaongoza, kila kitu amri, na maamuzi yasiyo husisha jamii. viongozi kwa kifupi ni watawala. Kwa namna hii huwezi ukampata kijana anayetamani ku-challenge na kuwa challenged ila kutawala. na kutawala ni function ya kuwekwa mahali bila hata idhaa ya watu. au kuwadanyanaya watu kutumia umaskini wao wa fedha.

  kuna sababu nyingi I guess, ila kubwa ni kuridhika
   
 10. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2010
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kwa maelezo haya,
  naona tatizo katika mfumo wa elimu tulio nao.
   
 11. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #11
  Feb 10, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,754
  Trophy Points: 280
  Mkuu Waborya umenena,

  Mtizamo hasi wa jamii pia unachangia vijana wa age kati ya20 hadi 30 kuwa katika siasa.

  Pia,vijana wanajua kujiingiza ktk siasa ktk umri mdogo ni hatari na ni kujiharibia maisha

  pia,vijana wengi hawajiamini na mara nyingi wanakatishwa tamaa,hili hapa nina experience nalo kabisa

  Ila natoa tamko,mimi kiama mim huu mwiko nitauvunja.Bungeni kunahitajika vijana sana...siasa si sehemu ya kwenda wastaafu.
   
 12. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #12
  Feb 12, 2010
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  BEN, WABEROYA,
  Sasa nini kifanyike?
  Tuwaache wazee washike hatamu tu siyo?
   
 13. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #13
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Twajifunza kuwa chachu ya mabadilko hutokana na mgandamizoo katika jamii..Mfano ubaguzi afrika kusini, ukoloni afrika, ubaguzi USA, ukabila Kenya, Mauaji ya Halaiki Rwanda...etc.

  Tanzania mgandamizoo wetu ni upi na uko kwa kiasi gani katika kundi lipi na lenye mbinu zipi katika UPAMBANAJI DHIDI YAO????

  Vijana wa Tanzania twahitaji mgandamizoo sahihi na kwa hakika tutaamkaa na kukumboa taifa letu toka kwa wanyonyaji Viongozii..
   
 14. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #14
  Feb 12, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 8,118
  Likes Received: 2,422
  Trophy Points: 280
  Kushika nafasi muhimu kunahitaji uzoefu? Kwenye 'nafasi muhimu' kuna ulaji au utumishi? Hao walioshiba, wameshiba nini?
   
 15. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #15
  Feb 12, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Vijana wenyewe unaowasema wako wapi???? Hawa wanafiki wanaojifanya kuipinga serikali kwa majina ya bandia kumbe hakuna lolote. Kazi kuloloma tu ooh hiki hakiendi hivi ooh hiki vile, hakuna lolote. Njaa tu inasumbua vijana wa kibongo, hata ukipewa nafasi utakuwa kama hao wengine tu. Nyinyi ni WANAFIKI. Nchi hii imeshauzwa. Vijana mlie tu, labda baba yako awe na yeye matawi ya juu, kama walivyo kina Hussein Mwinyi na Ridhiwani Kikwete vinginevyo nyinyi mbuzi tu!

  Mtaishia kuandika andika upuuzi tu humu. Hamfiki kokote. Hamko Makini, Mamluki mnatumiwa tu.

  Mabingwa wa kulalamika. Kuanzia sasa Nawapuuza!!!!!!!!
   
 16. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #16
  Feb 12, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,754
  Trophy Points: 280

  I'm speechless!

  My brother thi is only what you can argue?we are still lagging behind by far.

  well,Kunahitajika mjadala ya kweli na hasa unaohusu umuhimu wa vijana ktk kuamua mustakabali wa taifa lao.Kuna umuhimu wa kupigia upatu taasisi za vijana kama baraza la taifa la vijana.Hapa tungepata ma-think tankers wengi ambao ni vijana nakutakua na fursa pana kwa taifa kujiwekea hazina ya viongozi maahiri

  Pia baraza la vijana litatakiwa liwe financed frm an independent source ili wasiwe prone kwa political parties and some few thugs.

  Pia,kuna haja ya kupiga kampeni tena ya kuamsha muamko na kuielimsha jamii ili kugeuza mtazamo wao juu ya vijana ktk kupewa nafasi za uongozi nk.
   
 17. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #17
  Feb 13, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  I am happy that you have used the word mgandamizo...these very same people can wake up any time! they need external force. So either we are pushing hard and we want changes today or we dont want nature to take place.

  Our education system, culture etc do not give rooms for youth to think independently and to challenge society positively. Sadly, our leaders, opposition parties even religious group they are doing the very same mistake!

  There is not problem in Tanzania now, lets them enjoy time will come, when people will say 'arent the same people??'
   
 18. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #18
  Feb 13, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Change should start individually, never waste your time to wake up slamber, s/he may slap you!! do you remember Mwanakijiji wrote the article 51 reasons for JK not to proceed, the next day we received 102 why JK should continue! who wrote that, do you think Kingunge? no very same youth!!!

  Yes, leaders will be blamed forever, but we need real change individually, that will initiate other people around us!!
   
 19. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #19
  Feb 15, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nafikiri vijana wapo na wengine wameonyesha walau kwamba wanaweza kufanya siasa kwenye level ya kitaifa, kuna mtu kama zitto, dundu, makamba (jr), etc

  Kuna tatizo la mfumo hasa kwenye vyama wa kuzuia vijana kukua kisiasa kwasababu ya siasa za tanzania imekuwa kama ownership fulani hivi (club) hasa kwenye upinzani

  Kwa CCM huko vijana wapo kina nchimbi, maige, serukamba etc..

  Tatizo kubwa je katika hao vijana kuna anayeleta fikra mbadala na mwenye tabia njema kwa manufaa ya nchi? very few indeed!

  Sioni kama vijana wanawaunga mkono vijana wenzao kushika nafasi either kwa makusudi au kwasababu ya kutaka mshiko sijui?
   
 20. tgeofrey

  tgeofrey JF-Expert Member

  #20
  Feb 15, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 531
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Vijana wengi wanakatiswa na tamaa na wazee wenye hiyo siasa kusimika majina ya vijana wao, wakiangalia hawana majina makubwa yaliyozoeleka wanajikatisha tamaa.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...