Vijana, msifanye makosa kama niliyofanya. Kujiunga na CHADEMA ni sawa na kucheza karata tatu!

Chris Lukosi

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
4,581
2,937
Kuna uzi umeanzishwa hapa ukihoji sababu za mie kujiunga na chadema na baada ya muda mfupi kurudi nyumbani CCM.

Ndugu zanguni, kufanya kosa ni kawaida lakini kuendelea kulifanya hilo kosa ndio tatizo. Mimi Nilijiunga na Chadema nikitegemea kuwa ndio njia pekee ya kujiunga na harakati za kujenga nchi yetu Tanzania, lakini madudu niliyoyakuta huko ndio yalinifanya nitoke nduki.

Hizo post zote wanazotumia kuhoji maamuzi yangu nilizitundika mie mwenyewe na nakiri kuwa katika makosa niliyowahi kuyafanya duniani, Kujiunga na chadema lilikuwa kosa kubwa kabisa katika maisha yangu na sitolisahau maishani.

Mimi kujiunga chadema nilikuwa nimepotea na bila kujijua nikajikuta katikati ya maandamano yasiyo na kibali. Lakini niliyashtukia makosa hayo na kuamua kurudi nyumbani. Kutenda kosa ni kawaida kwa mwanadamu lakini kuendelea kulitenda hilo kosa hata baada ya kujua umetenda kosa ni kosa kubwa.

Mimi kujiunga na chadema ilikuwa hakuna tofauti na mtu aliecheza ule mchezo unaoitwa kapesa kekundu au karata tatu. Niliingia huko nikiwa na hope ya kuungana na watu wanaotaka kuleta mabadiliko nchini na nilitumia muda wangu mwingi kuzunguka UK nzima kukijenga chama. Muda wote huu nikiwa UK nilikuwa bado sijakijua chama vizuri mpaka pale nilipofika Nyumbani na kukutana na viongozi wa juu kabisa.

Nikagundua Chadema ni tofauti kabisa na nilivyodhani.

Chadema ni chama kinachomilikiwa na watu wachache na si chama cha wananchi kama mnavyodhani. Hakuna kamanda yeyote anayeweza kuukosoa uongozi hata pale itakapoonekana wazi kuwa wamekosea. Ukiwakosoa utaitwa msaliti/masalia na kufukuzwa. Hili liliniogopesha sana na nikajiuliza ikiwa hawa watu leo hatuwezi kuwahoji pale wanapokumbwa na kashfa kama za matumizi ya hela za ruzuku kupeana vyeo nk wakiwa bado hawajashika dola , jee tutaweza kuwahoji wakiwa wameshika Dola?

Nawasikitikia vijana wenzangu ambao bado wako chadema kwani wako kwenye basi lenye madereva watatu ambao hawaelewani, wameacha kuendesha basi na sasa wanavutana kuhusu nani aendeshe hilo basi mwaka 2015, Dereva mmoja ni kijana na mwingine ni mtu mzima akisaidiwa kwa ukaribu na mwenye basi. Kuna huyu dereva mwingine kutoka singida yeye bado hajaonyesha nia lakini najua muda wowote na yeye atasema anataka kuendesha na hapo ndio tutasikia mengi sana na once again watakuwa very bize hapa JF kutoa matamko na bila kusahau matusi mazito mazito kwa yeyote atakaenyosha nia.

Chadema sio chama kamili cha kisiasa kama vile wengi wanavyodhani, chadema ni mkusanyiko wa wapiga deals wanaotegemea siku wakiingia ikulu wafanye kweli,

Nina uhakika vijana wengi wakijitambua wataiga mfano wangu na kurudi nyumbani CCM tulijenge taifa. Mabadiliko ya kweli na maendeleo ya kweli yatatoka ndani ya CCM. Kama kweli unataka mabadiliko na maendeleo ya kweli basi rudi nyumbani ufanye hivyo.

Vijana msikubali kutumiwa kwa kufanywa chambo cha vurugu na maandamano yasiyo na vibali kuwapatia umaarufu watu wachache ambao ninakuhakikishieni, siku wakipata wakitakacho watawaona kama walevi tu

Mfano mzuri ni yule muandishi wa habari wa mjengwa (sio LUDO ) aliepanda basi kwenda Dar kuhudhuria harambee iliyofanyika serena hotel, kijana alitumia akiba yake yote kwenda dar baada ya kualikwa na lema kupitia mimi. Kijana alipofika nje ya hotel Lema alimfuata nje na kuchukua ule mchango lakini hakumruhusu kuingia ndani, Kijana alikaa nje mpaka saa saba usiku bila mafanikio kuingia ndani kisa alkikuwa hafanani na waliokuwemo ndani na alikuwa akionekana kamanda mchovu tu. Mmie ilibidi nimtumie nauli yule kijana na kumlipia hotel arudi Iringa. Mpaka leo kijana hajui hata kama mchango wake ulifika au la na alisikitika sana jambo ambalo ni moja tu ya mambo yaliyonifanya niwashtukie chadema kuwa they are just deal makers.

Chadema wanapenda kutumia matukioa ya majanga kama mtaji wa kisiasa na nina uhakika nchi ikiwa kimya bila matukio mabaya uongozi wa chadema huwa bored sana.

Nawatakia Pasaka njema
[h=2]Re: Vijana msidanganywe na CHADEMA, hakuna shortcut kwenye maisha. Ukitaka kujua shortcut kula nauli[/h]

quote_icon.png
By Chris Lukosi
Ndugu zanguni,

Nimegundua kuwa vijana wengi ambao wamekuwa brainwashed sasa wameacha hata kufanya shughuli zao za kuwaingizia kipato na matokeo yake wanatumia muda mwingi kwenye mikutano na maandamano yasiyo na vibali na hizi harakati zao wanazoita M4C.

Suala hili nimelithibitisha pale nilipoona hadi wasomi kama ma Dr wanapoacha kazi zao na kujiunga na hiki kikundi cha wapiga deals na kuanza kujidhalilisha kwa kutukana watu humu kama mateja wakitegemea kuwa ifikapo 2015 watapata uwaziri au ukuu wa mikoa kama sio wilaya.

Chadema imeweza kuwadanganya hadi mateja kuwa wakichukua nchi wao ndio watakuwa polisi na usalama wa taifa, jambo ambalo limesababisha vijana wengi siku hizi kuchukia polisi na badala ya kuwaona kuwa ni walinzi wa taifa wao sasa wanawaona ni adui ya chadema.

Ningependa tu kuwaasa ndugu zangu, Chonde ! Chonde! msikubali kurubuniwa na ahadi za uongo ambazo hata nyinyi wenyewe mnajua kabisa ni ndoto kukamilika.

Vijana msikubali kutumika kwa manufaa ya watu wachache wanaotaka kupiga deal kwa mgongo wenu
Vijana msikubali kudanganywa kuwa Chadema ikichukua nchi mabomba yatatoa maziwa na mbege
stock-illustration-19190041-land-of-milk-and-honey.jpg

Vijana msikubali kutumiwa kufanya vitendo kinyume na sheria ya nchi ili kuwafurahisha viongozi wa chadema
Vijana mkae mkijua kujiunga na chadema ni sawa na kula nauli ya kukupeleka unakotaka kwenda
Vijanna mkae mkijua kuwa ukila nauli itabidi utembee kwa miguu na hapo ndio utakapojua short kati zote
Vijana mkae mkijua kuwa hakuna shortcut kwenye maisha wala hakuna mteremko kwenye maisha
Vijana mkitaka kutumia shortcut kwenye maisha mwisho wake sio mzuri kwani shortcut mara nyingi ni uhalifu
Vijana amkeni fanyeni siasa zenye lengo la kuletea maendeleo na amani taifa letu
Vijana sio lazima ukiachana na utapeli wa chadema uhamie CCM kuna vyama vingi bora vya upinzani kama NCCR nk (kama unataka kuwa mpinzani)

Nimeamua kuyasema haya kwa faida ya taifa letu kwani mimi mwenyewe nilipojiunga na chadema nilijua nimejiunga na chama chenye kuwatetea wananchi kabla sijashtukia kuwa niko pale kutumika kwa faida ya watu wachache ambao wanaongoza chama kiimla na pamoja na kuwa nilikuwa kiongozi ndani ya chama nilikuwa sina haki au kauli ya kuweza kukemea matendo mabovu ya viongozi, mfano mzuri wenyewe mnaona ZZK anavyobezwa na wenzake sembuse nyie wenzangu?????

Chadema ni ya wachache, na wachache wenyewe ni wa kaskazini walio karibu na Mzee Mtei

JITAMBUE!

Mungu ibariki Tanzania



 
Hivi huyu jamaa huko UK hakuna upinzani? USA hakuna upinzani? Nchi itaendeleaje bila upinzani?
Hivi mtu unaishi nje ya nchi tena UK unashindwa kujua maana ya opposition party? Kama ulijiunga chadema kwa kupotea waache na wengine wapotee kwani unawasadia nini?
 
Tumeshakuzoea Mwingereza wewe wa Essex, huna mpya blahblah mbumbumbumm!! Unalelewa huko UK unaongelea mambo ya Bongo we vp.
Ulitukana mto kabla hujavuka mamba, una bahati ulikuwa ndiyo umeanza ukafanikiwa kurudi.
 
Tumeshakuzoea Mwingereza wewe wa Essex, huna mpya blahblah mbumbumbumm!! Unalelewa huko UK unaongelea mambo ya Bongo we vp.
Ulitukana mto kabla hujavuka mamba, una bahati ulikuwa ndiyo umeanza ukafanikiwa kurudi.
Yote hayo hamkuyaona wakati mnampa uongozi? Lema alikua mgeni wa nani? Hata hizo nguo anazovaa amenunuliwa na Lukosi.
 
Mvinyo wa Pasaka mbaya sana , hasa ukinywea kwenye pub iliyombali na nyumbani.

Hivi , kama huyo kijana anayemsema wa Iringa alikuwa hana hata nauli ya basi kurejea kwao, za mchango alitoa wapi? Ama alikuwa katumwa kazi maalum na alipobainika kafungiwa nje? Jambo hili linanifikirisha sana.

Dili , ni wewe na tenda yako ya bandarini dar, tutakufuatilia kama unalipia kodi zote halali ,maana CCM ni kichaka cha wezi.....
 
Kaka unastaili heshima ya pekee kwa maamuzi uliyofikia lakini bado hujaonesha maovu yakutosha ambayo wanayafanya.Naomba utuambie mengi zaidi kwani vijana bado hawajaamka, wanafikiri ukiwa CDM ndio utaweza kulikomboa taifa hili lakini minaamini popote ulipo unaweza kupambana na kuleta maendeleo katika taifa.
 
Pasaka njema nawe pia
.wamekusikia na wamekuelewa hapa wanatafuta vijisababu vya kukukosoa wanashindwa
 
Hata mimi nakuunga mkono ndugu yangu Chriss Lukosi kwa ushauri wako mzuri. Ni kweli wale wote wanaotarajia kujiunga na hicho chama kwaajili ya njaa zao, basi ni heri wasifanye hivyo. Wale wazalendo tu ndiyo watakaoweza kuendana na hicho chama. Bilashaka mambo yako hivisasa ni mazuri zaidi kuliko kule ulipokuwa unahangaika na kubeba box.
 
Chadema sio chama kamili cha kisiasa kama vile wengi wanavyodhani, chadema ni mkusanyiko wa wapiga deals wanaotegemea siku wakiingia ikulu wafanye kweli,

Wewe ndio unapenda vya bwerere baada ya kutishwa tu na ccmafisi kuwa watakufungia biashara yako ukarudi ccmafisi na kuanza kuwasifia. Yetu macho tunakusubiri 2016, tulitegemea kuwa ww ni mwelewa na uko nje ya nchi uwezi kutishwa na ccmafisi kumbe ww ndio mwoga wa kutupwa. Endelea kuwatumikia ccmafisi na yote unayoyaeleza hapa tupo mashaidi ucje sema ooh nililazimishwa kusema ivyo
 
Ndugu zanguni, kufanya kosa ni kawaida lakini kuendelea kulifanya hilo kosa ndio tatizo. Mimi Nilijiunga na Chadema nikitegemea kuwa ndio njia pekee ya kujiunga na harakati za kujenga nchi yetu Tanzania, lakini madudu niliyoyakuta huko ndio yalinifanya nitoke nduki.


Hizo post zote wanazotumia kuhoji maamuzi yangu nilizitundika mie mwenyewe na nakiri kuwa katika makosa niliyowahi kuyafanya duniani, Kujiunga na chadema lilikuwa kosa kubwa kabisa katika maisha yangu na sitolisahau maishani.

Daaaah kama kuna watu wanafiki wewe ulitakiwa upewe tuzo kabisa. Sentensi niliyosoma naamini hata CCM wenyewe watakuwa wanakushangaa.

CCM inajua bila chenga kabisa kuwa CDM ni wakweli na wawazi katika utekelezaji na usimamizi wa mambo mbali mbali ya chama au bungeni lakini inchokifanya haitaki kuachia madaraka kwa sababu kuachia madaraka siyo utamaduni wa nchi za dunia ya tatu.

Wao ndiyo waliotuletea mfumo wa vyama vingi lakini kuutekeleza imekuwa mtihani sana. Kama mtu anashindwa kihalali hapo ndipo tunapoweza kusema demokrasia imechukua mkondo wa na siyo ubabaishaji.
 
lukosi,keep this pathetic insincerity to your girlfriend,pretenders are worse than devils,endelea kubeba mabox huko na kuosha vyombo
 
Nilipokuwa kanisani Jumapili iliyopita ambayo yaitwa Palm Sunday kwa kithungu, tulisomewa kwamba Yuda Iskariote alimwuza Yesu kwa wayahudi kwa vipande 30 vya fedha kama Ludovick alivyomwuza Rwekatare kwa Mwigulu Mchemba kwa vipande 50 elfu vya fedha. Ndio raha ya kuingia CCM ati?
 
Ungetuambia uliwashauri lipi hawakukusikiliza na ulilitoa lini na mahali gani. Naje tangu umerudi unakokuita nyumbani umepeleka ushauri gani wakaufatilia mpaka unawasifu kiasi hiki? Bora ungerudi ukakaa kimya kuliko unayoyaongea sasa maana hata mtoto anayejiunga na JF leo anakuona limbukeni tu wakuropoka tena akisifia unasifia kitu hata miezi sita bado!!!
 
Back
Top Bottom