Vijana mmepwaya kwenye uongozi

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,898
11,745
Pamoja na kuaminiwa na wananchi pamoja na Rais ni dhahiri vijana mmepwaya kwenye uongozi. Mmebaki kuwa watu wa kufanya kazi ili muonekane tu, na nyie ni mafoto na kuyaweka kwenye mitandao ya kijamii ili muonekane mnafanya kazi kumbe sivyo.

Vijana mnavyofanya kazi ili muonekane mnafanya kazi hii ni sawa na mtoto ambaye hataki kujisomea akikuona mzazi anakimbia kujifanya yupo busy anasoma. Vijana mmekosa dira yoyote katika uongozi ambayo itamsaidia mwananchi wa kawaida mmebaki kutafuta sifa binafsi na kutoa matamko ambayo hayatekelezeki na kuwa aibu kwenu.
 
Mm ni kijana kabisa 27 bado ntaendelea tuu na imani yangu kuwa UONGOZI NI BUSARA NA KWAKWELI BUSARA INAENDANA SANA AGE, ukuu wa mkoa parefu sana kupewa kijana hasa wa type ya muuza sura na mpenda kusifiwa km makonda
 
Hivi mnategema kijana wa UVCCM ataleta mabadiliko? Kijana anaesubiria upinzani waongee na yeye atoe tamko? Tunahitaji vijana wachapa kazi wasiokua na uchama ndani yao.
 
Mkuu, vipi kijana mwenzako, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Vincent Mashinji aliyeaminiwa na Mwenyekiti wako na Kamati kuu? Je hajapwaya
 
Mkuu, vipi kijana mwenzako, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Vincent Mashinji aliyeaminiwa na Mwenyekiti wako na Kamati kuu? Je hajapwaya
Uwe unatumia akili unapojibu post za wanaume, kuna sehemu hapo juu nimetaja chama cha siasa.
 
Ukiachana na siasa za kupiga domo sana majukwaani, kwa ujumla wake, ukawa hasa hasa Chadema wana wabunge ambao wameflop sana, kinachowabeba ni pere peree mingi, ila uhalisia wake ni kua hawana weledi wowote.
 
Uwe unatumia akili unapojibu post za wanaume, kuna sehemu hapo juu nimetaja chama cha siasa.
Maelezo yako yamelenga vijana waliochaguliwa na wananchi na walioteuliwa na Rais. Ndio maana nimekuongezea hapo kuwa hata Mashinji kapwaya sana japo ulilenga kumtaja lakini ukakwepa
 
Vijana ni viongozi wa leo kazeni buti, watupeni lupango vijana wazururaji na wasio kuwa na ajira, wakamateni ombaomba, hakikisheni bar zinafungwa saa mbili na muziondoe katika makazi ya watu, wakusanyeni walevi sehemu moja, kamateni dadapoa wote, safi sana, wapi heche suguta jembe la ukweli, wapi mnyika wakuchana laivu.
 
Maelezo yako yamelenga vijana waliochaguliwa na wananchi na walioteuliwa na Rais. Ndio maana nimekuongezea hapo kuwa hata Mashinji kapwaya sana japo ulilenga kumtaja lakini ukakwepa
Huyo ni kiongozi wa chama inawezekana anafanya vizuri kwenye chama chake, kuwa kimya sio sababu kwamba hufanyi kazi, hivi tangu uchaguzi uishe umemsikia Kinana, hoja imejikita kwa hawa vijana wa kubwabwaja kila siku huku utendaji zero, kuna wazee wanachapa kazi kimya kimya huoni selfie wala picha na mambo yanaenda sasa hawa vijana wameajiri mpaka wapiga picha.
 
Hivi mnategema kijana wa UVCCM ataleta mabadiliko? Kijana anaesubiria upinzani waongee na yeye atoe tamko? Tunahitaji vijana wachapa kazi wasiokua na uchama ndani yao.
Msijidanganye!! Halmashauri zote zinazo ongozwa na BAVICHA zimesinzia, tulidhani walivyokuwa wanaimba mabadiliko, tutayaona laki mmmmmmm, nenda kimara, nenda serengeti, nenda iringa, nenda Bunda, nenda Tarime, BAVICHA wamebaki tu kumgomea Tulia
 
Sio kila uzi unahusu vyama tafuta uzi wenye kuhusu vyama uchangie.
 
Back
Top Bottom