Vijana DAR kuundamana kuunga mkono hotuba ya Kikwete

greatthinkers,




inanisikitisha sana kuona vijana wanarubunika kirahisi rahisi, lakini kwa kuwa mnaipenda ccm ni vizuri makafanya hivyo. Labda kwa kuwakumbusha maandamano ya cdm yalipinga yafuatayo
  • malipo kwa dowans sasa mi nawaomba kesho muunge mkono malipo hayo.
  • kupanda gharama za maisha sasa naomba muunge mkono bei mpya ya sukari
ungeni mkono pia
  • rites
  • ,ticts,
  • meremeta,
  • alince air,
  • ndege ya rais,
  • radar,
  • bot twin towers,
  • iptl,
  • richmond,
  • noti mpya,
  • kiwira,
  • alex stewart,
  • safari za nje ya nchi utadhani yeye ni waziri wa mabo ya nje
  • ticts na uchafu mwingine ambao wamefanya hao wezi

hivi kesho ni siku gani, kwani ni ijumaa?
 
Ukishaona source: Uhuru Publications ujue maandamano hayo yameandaliwa na CCM nyuma ya mgongo wa Lyatonga Mrema na huyo kijana. Hakuna jipya. Watanzania watakaoandamana watakuwa ni wajinga wa kwanza kwa mwaka huu.
 
Haya maandamano ya kesho yameandaliwa kwa mwavuli wa kile ki NGO Cha Thomas Ngawaiya ,chenye ofisi yake pale Mazenze zamani ofisi za NCCR Mageuzi[jengo la Ngawaiya]...kwa ufadhili wa CCM na Ikulu
Yanaanzia Mnazi Mmoja na yataishia Manzese......barua za mwaliko zimetumwa kwenye matawi ya CCM na magari ya kuwapeleka wananchi Mnazi Mmoja yameshaandaliwa na kutakuwa na Posho..kiasi baada ya maandamano......pia wanasiasa kama mrema na wengine wa aina hiyo wamealikwa.....

Nina imani haya wala hayahitaji kibali wala taarifa za kiinteligesia....
 
Nashauri mwana JF ambaye ni mwandishi wa habari atakayeenda kuandamana kikazi..awe anaturushia updates za maandamano ya CCM..leo
 
CCM ina vijana tangu lini? ni mpuuzi gani leo aandamane kubaliki maangamizi yake? mimi nitakuwa wa mwisho kuamini kama kuna kitu cha namna hiyo.
 
wewe unafikiri vijana wote wako tayari kutumika na wanasiasa uchwara wanaojiita wapinzani?? kila mtu anao uhuru wa kuchagua upande gani ausopoti,we unafikiri hali ngumu ya maisha itaisha kwa kuandamana?

Haya mheshimiwa 'mpenda amani', tuambie hali ngumu ya maisha itaisha kwa kufanya nini, ukizingatia yale ambayo Rais mnayemuunga mkono ameyafanya hadi sasa kuiondoa ama kuiongeza hali hiyo!!
 
MAANDAMANO ya kuunga mkono hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa mwishoni mwa mwezi uliopita, yanatarajiwa kufanyika Dar es Salaam Machi 16, mwaka huu, yakiwa na ujumbe ‘amani yetu bado tunaipenda’. Akizungumza na waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana wa Tanzania, wapenda amani, Said Mwaipopo alisema, pia maandamano hayo yatahusisha kupinga kauli viongozi wa CHADEMA zinazochochea kutokea kwa vurugu nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti huyo, inaeleza kuwa, vitendo na kauli za viongozi vya chama hicho vina lengo la kupandikiza chuki kwa Watanzania dhidi ya serikali iliyopo madarakani, ambavyo mavuno yake ni umwagikaji wa damu.

Alisema, maandamano yanayofanywa na CHADEMA huvishwa sura ya kupanda kwa gharama za maisha, wakati huohuo yakiwa na lengo la kuipinga na kutaka kuing’oa serikali.

Maandamano hayo yatafanyika kuanzia viwanja vya Mnazi Mmoja mpaka uwanja wa Bakhresa Manzese, na Mwenyekiti wa TLP Augustino Mrema anatarajiwa kuyaongoza.

source: www.uhurupublications.com

Okay........... kumbe wako na huyo aliyepotezaga dira akawa anangoja huruma ya wananchi!!! na waendeelee tu. All the best vijana wachache msiyo na akili hata ya kunywea maji!!!!
 
Back
Top Bottom