EasyFit
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 1,269
- 1,082
BARAZA la Vijana wa Chadema (Bavicha ) limemtaka Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, kutoingilia masuala ya chama hicho huku likitamba kuwa nguvu ya umma ndiyo iliyotumika kupambana na mafisadi na kuchangia ongezeko la kasi ya uwajibikaji serikalini.
Kauli ya vijana hao imekuja siku chache baada ya kiongozi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, kukaririwa akikemea matumizi ya nguvu ya umma, yanayoendeshwa na baadhi ya vyama vya siasa nchini kushinikiza mambo mbalimbali, na kuonya kuwa tabia hiyo hailifikishi taifa popote badala yake nguvu hiyo ingetumika kuhamasisha maendeleo.

Akijibu kauli ya Lowassa jana, Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Heche, alitamba kuwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya ufisadi nchini, yametokana na nguvu hiyo ya umma inayobezwa na Lowassa.
Alisema nguvu ya umma ndio iliyotumika kuanika orodha ya watuhumiwa wa ufisadi mwaka 2007 katika Viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam na kusababisha baadhi yao wawajibishwe.
Katika orodha hiyo ya Chahema iliyokuwa na majina 11, Lowassa ni miongoni mwa wanasiasa waliotanjwa na chama hicho kikuu cha upinzani.
Heche alisema kutokana na vitendo hivyo, wananchi waliweza kuonyesha nguvu zao kwa kuwataka mafisadi kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kujiuzulu nafasi zao, jambo ambalo lilifanyika.
Lowassa alijiuzulu Uwaziri Mkuu Februari 2008, kutokana na kashfa ya Mkataba wa Richmond baada ya Bunge la Tisa kuunda Kamati Teule, chini ya Mbunge wa Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, kuchunguza suala hilo na kutoa mapendekezo yake.Heche alisema, Bavicha itaendelea kutumia nguvu ya umma ili kuleta maendeleo kwa wananchi na kumulika mafisadi, ikiwa ni pamoja na kuwaanika hadharani ili wananchi waweze kuwatambua na kuwachukulia hatua stahiki za kisheria.
Alifafanua kwamba, kufanya hivyo si kutishia amani ya nchi bali amani ya watuhumiwa wa ufisadi ndiyo inakuwa shakani kutokana na matendo yao maovu.
Heche aliongeza kwamba wananchi wanapandwa hasira juu ya viongozi wenye matendo kama hayo, kwa sababu wanachangia kuliingiza taifa katika dimbwi la umaskini kwa kujali maslahi yao binafsi.
Kwa mujibu wa Heche,Lowassa anapaswa kuonyesha mfano hai kwa wananchi ili aweze kujenga imani, jambo ambalo linaweza kuwabadilisha taswira.
Alisema, kama Lowassa anaamini nguvu ya umma inapaswa kutumika katika kazi za maendeleo alizozitaja, basi awe wa kwanza kufanya hivyo yeye na chama chake badala ya kuzunguka katika nyumba za ibada na kuchangia fedha nyingi, ambazo vyanzo vyake havijulikani na Watanzania wangependa kujua hilo.
::Mwananchi