Vijana 69 waitosa CHADEMA Mbeya

TandaleOne

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2010
Posts
1,644
Reaction score
709
Chadema Kata ya Mwakibete, jijini Mbeya imepata pigo baada ya vijana wake 69 kuamua kukitosa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Vijana hao walisema wamefikia uamuzi huo baada ya Diwani wa Kata hiyo, Lucas Mwampiki (CHADEMA) kushindwa kukisaidiankikundi chao kama alivyoaihidi kwenye kampeni zake, licha ya kumfuata mara kadhaa kumuomba msaada na kumkumbusha juu ya ahadi yake.

wakizungumza mbele ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya, Dk Mary Mwanjelwa walisema Diwani Mwampiki amekuwa kikwazo kwao katika kujiinua kiuchumi na kuondokana na Utegemezi.
 
Katika kundi la mamba pia kenge wamo. Kwa hiyo kwa kujitoa wametatuaje hilo tatizo ?Kwa hiyo huo msaada wamepewa na CCM na for how long?.
 
Ni wakati sasa wa vijana kuamka kutoka kwenye usingizi mzito ili waondokane na wingu zito vichwani mwao kuwa chadema ni chama cha ukombozi.

Vijana hongereni kwa maamuzi sahihi na ya kuigwa.
 
Kwani walitegemea diwani awape nini? Kama aliwapa idea ya kuunda kikundi si walitakiwa wakakope hela benki au diwani ni benki? Sipati tabu kuamini hao ni vijana wa magamba waliojivisha U-CHADEMA!
 
Ni wakati sasa wa vijana kuamka kutoka kwenye usingizi mzito ili waondokane na wingu zito vichwani mwao kuwa chadema ni chama cha ukombozi.

Vijana hongereni kwa maamuzi sahihi na ya kuigwa.

hata kama chadema sio chama cha ukombozi, lakini sio chama cha kuteka na kutesa watu, kuwang'oa meno na kucha kama ilivyo kwa NYINYIEMU
 

Walitaka diwani awasaidie kuwapa hela..? ccm wanakumbuka Mwalimu alivyokuwa anahimiza kutokuwa kupe lakini..? Kwamba wananchi wajitegemee badala ya kutegemea..? Ingalikuwa mie niko ccm nisingejaribu kuposti uzi kama huu.. Huku ni kujidhalilisha kwisha kazi..
 
Kwani nani alimwambia atoe ahadi za uongo..? Na nyie bila kutafakari wala kujitafakari mnamtetea huyo Diwani.
 
Kwani nani alimwambia atoe ahadi za uongo..? Na nyie bila kutafakari wala kujitafakari mnamtetea huyo Diwani.
Una uhakika Diwani aliwaahidi pesa..? Unataka kusema waliopiga kura ni hao 69..? Mbona hatujawasikia wengine wakijitokeza kulalamika kwamba waliahidiwa pesa lakini hawatimiziwa ahadi zao..? Na kwanini hayo yatokee wakati mbele ya kiongozi wa ccm..?
 
Maneno ya cdm ni matamu sanaaa. Tutawapa ajira, maisha safi, elimu bure mpk chuo kikuu. Kwenye utekelezaji ni ziroooo. Kila heri vijana
 
uyo mbunge unae msema siyupo kugawa pesa hapa mjini na watu wanashida na pesa lazima wamfaliji alipita kata ya maanga dau lilikua dogo akakosa watu
 
Mkuu hao hawakuwa CHADEMA ila wana SACCOS fulani ya kutafuta misaada.
 
Ni wakati sasa wa vijana kuamka kutoka kwenye usingizi mzito ili waondokane na wingu zito vichwani mwao kuwa chadema ni chama cha ukombozi.

Vijana hongereni kwa maamuzi sahihi na ya kuigwa.
Anza kuamka wewe mbulula
 

Source? Nape? ama tunatupia tu vitu bila source?
Pleasae, mods mfundisheni huyu mwenezi kufanya kazi yake vema...
cc PainKiller Paw
 
Last edited by a moderator:


hakuna mwanachama mwenye akili wa chadema anaweza kuhamia ccm
 
hawa vijna wajinga kweli nani aliwaambia kwamba chadema husaidia vijana au wanachama wake,wanachojua chadema ni kuwatumia vijana na kuwatelekeza daima.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…