Vijana 500 waliotapeliwa ajira Moshi wapata ahueni, Meya Raibu na Dstv wawamwagia ajira za kutosha.

Aug 21, 2021
16
20
MEYA RAIBU AFANIKISHA AJIRA KWA VIJANA WALIOTAPELIWA MOSHI, 60 WAANZA KAZI DSTV

Na Mwandishi wetu, Kilimanjaro

Mapema leo Mstahiki meya Wa Manispaa ya Moshi Mhe Juma Raibu amefanikiwa kuwasaidia vijana 60 miongoni mwa vijana 500 waliokumbwa na kadhia ya kutapeli fedha zao na watu waliojitambulisha kuwa maafisa wa kampuni ya Alliance Global na kisha kutokomea kusikojulikana.

Meya Raibu amewaunganisha vijana hao na kampuni ya visimbuzi vya DSTV ambapo tayari wameanza kazi ya mauzo ya visimbuzi hivyo vinavyosifika kwa ubora hapa nchini, lakini pia Meneja wa kanda ya Kilimanjaro wa DSTV ametoa rai kwa vijana hao wanaorejea makwao wafike ofisini kwake ili awaunganishe na matawi ya mikoa wanayokwenda wakapatiwe ajira hiyo mikoani huko.

Akizungumza kwa uchungu mwenyekiti wa kijiji cha langoni Mama Shirima amempongeza mstahiki meya Juma Raibu kwa kuliibua na kufanikisha ajira hizo kwa vijana hao kwani hiyo ni kama sadaka aliyowekeza kwa mola, nanukuu " Meya wetu tunajua watu huangalia sana yale madhaifu madogomadogo ili wamchafue mtu lakini mimi nasema wewe una mema yako mengi uliyotufanyia wana-Moshi toka ukiwa diwani wa kawaida, ipo siku watu watapigwa butwaa wakilikuta jina lako kwenye vitabu vitakatifu vya dhahabu paradiso" mwisho wa kunukuu

Nae mhanga wa tukio hilo ndugu Isaya Ngoroko amemshukuru Meya Raibu kwa kutokuchoka kuwasaidia na kuwasikiliza ;nanukuu " Umekuwa kiongozi watofauti sana toka tukio hili litokee, unapokea simu hadi usiku wa manane, umeamua kutubeba kama wadogo zako wa tumbo moja, leo tulijua umekuja kutukamata tukaanza kukimbia lakini kumbe umetuletea habari njema, umeleta vyakula na umelipa nauli za watu 15 wa mikoa ya mbali fedha ambayo ungeweza kula na familia yako, hakika kama Meya ubarikiwe sana" Mwisho wa kunukuu.

KAZI IENDELEE NA IKAMILIKE
 
Kwahiyo kuwa king'asti wa DStv nako ni kupata ajira?.
Hizi kazi za uwakala ziko nyingi na huombwi hata cheti.
Hapa watawatesa tu hao vijana
 
Walichokuwa wanafundishwa ili wafanye.... na hiki wanachofanya sasa kina tofauti ?

Hapo wamekuwa ma-salespeople au wamepata ajira wanalipwa basic pay hata wasipouza ? Ukiniuliza mimi kuuza dawa za virutubisho huenda ni rahisi kuliko kuuza Dish...., Utauza mangapi kwa siku?
 
Back
Top Bottom