Vijana 5 wanahitajika

Kazi Inayokushinda ww mwingine anaiweza. Ukiona pesa iliotajwa ni ndogo kwako kwa mwingine ni kubwa. Ni sawasawa na ww ukaona Mshahara wa milion moja afadhali unakidhi mahitaji kuna mwingine hiyo kwake ni ndogo sana. Tujaribu kubadilika. Hii ni biashara mtu unataka chukua, kama hutaki unaacha wengine wanachukua. Halafu mtu unataka maendeleo wakati maendeleo ya kichwani tu hauna. Tusipende kutupia maneno ya ovyo, badala ya kukatishana tamaa kwanini tusipeane moyo?
Watu tatizo chuki nyingi sana na wivu wakijinga.
 
Bado umeng'ang'aniapo kwa kuwa kuna a/c au?

Mkuu sio kila mtu ana network na sio kila graduate atapata kazi ya kulipwa milioni.. wako watu na degree zao wako mtaani huu mwaka wa tatu ameamua awe anapika vitu vidogo vidogo na kuuza, sio kwa sababu hapendi kulipwa hiyo unayodhani wewe kuwa ni.pesa nzuri ila hana jinsi ya kupata hiyo kazi keshatembeza cv hakuna uchochoro hajakatisha ila hakubahatika kupata kazi, leo apate mahali.pa kumlipa 106,000 akatae kwa kuwa tu ye ni graduate akikaa nyumbani hiyo ela ataipata? Mimi nilivolunteer mahali miaka mitatu silipwi mia kipande ila ndiko mahali nilikopatia uzoefu na kupata network. Usimkalie kooni kana kwamba alimwomba Mungu ampe kazi ya mshahara huo.
 

Nimekuelewa mkuu, nafuta kauli yangu
 
Mshahara wa elfu themanini bora nitembeze Mitumba yangu au.maji ya kandoro kwenye foleni.
 

Acha kelele ni PM kijana nitumie vyeti vyako nikupe ajira uje ujenge NDOTO zangu maana naona zako umeshindwa kujenga,degree horder unaamka SAA 12 unarudi 10jioni kwa mshahara wa 100000÷30= 3300/day na bado unaona fahari kuajiriwa!!
 

Unatafuta wafanyakazi au watumwa?! Mzazi haswa au ndugu mtu amdhamini mwanae kwa shiling 80k?! you must be jocking! yaani hata kima cha chini cha serikali hufiki?! a joke of the century!
 
Wajameni tuwe na shukrani, mbona mara nyingi tu kuna mabandiko humu yanasema "natafuta kazi yoyote". SASA HUYU jamaa kakosea nini. tena mimi amenifuhasisha coz hajasema tumeni kwanza elfu70.
 

Kweli ndgu,umeongea point tupu.
 
Acha kelele ni PM kijana nitumie vyeti vyako nikupe ajira uje ujenge NDOTO zangu maana naona zako umeshindwa kujenga,degree horder unaamka SAA 12 unarudi 10jioni kwa mshahara wa 100000÷30= 3300/day na bado unaona fahari kuajiriwa!!

Mkuu,haina haja ya kutambiana.Hongera kwa mafanikio uliyonayo kutokana na kujiajiri.Keep it up.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…