Vigogo wengine kutimkia chadema

Sina wasiwasi na mallya au Mtanzania yeyote anaye hamia CDM, kwani kuna utaratibu, uongozi na sheria za chama zikiambatana na uhuru wa kutoa maoni na kusikilizwa
 
Kwani hao wanaoruka kutoka jahazi la CCM na kuhamia la CHADEMA wanaacha itikadi zao? Ni mafisadi tu. Sina imani nao. Kwa hili, natofautiana na Mwenyekiti wangu, Freeman Mbowe. HAWA WAMETUMWA kuja kuimaliza CHADEMA. Hawana hata CHEMBE ya uzalendo kwenye nafsi zao.

Ndugu, katika siasa hili la kuhama chama kimoja kwenda kingine ni jambo la kawaida. Hapa kwetu Tanzania ni kwa sababu tumeisha-label baadhi ya watu kuwa hawawezi tena kuwa watu wazuri ndani ya vyama vyetu, CCM wanajua sana kutumia hili jambo la kuhama (japo mara nyingi tunasema CCM imenunua mtu, n.k hii siyo hoja yangu kwa sasa), hebu fikiria leo Dr. Slaa ahamie/au arudi CCM alikotoka (kitu ambacho mimi siamini kama chaweza kutokea, chukua mfano huo), je atakuwa fisadi au itikadi yake itakuwa imegeuka na kuwa ya kifisadi? Hili ni jambo la kiafya kwa demokrasia yetu. Mfano mwingine, kule Igunga CDM walipata kura nyingi walizitoa wapi kama sio miongoni mwa wana-CCM? hata mfano wa hivi karibuni Arumeru Mashariki zimetokana na wapenda haki na maendeleo bila kujali wapo chama gani. Kwa kusema hivi sipingi kuwa CDM siwe makini na wahamiaji, but isiwakatae kwa sababu zozote zile zinazotokana na past yao, kama wamejitambua na kujirekebisha watatufaa sana ili come 2015 tuwe Magogoni.

Nawasilisha.
 
Nampongeza jamaa kwa kuhamia CDM na wengine waige kwani
kama tunapingana na ufisadi na wewe sio mnafiki hama kwenye
chama kichafu nenda sehemu safi usiwe kama "chichidodo ndege mla funza wa kinyesi lakini hapendi kinyesi"
 
Factor ni muda tuu magamba yote yatapukutika! Ndo kawaida ya magamba japo ya joka yakitoka yanaota upya.
 
Mlisema leo Lowasa anapasua jipu, hadi sasa kimya. Sasa manakuja na hili. Acheni kuishi kwa kuhisihisi. JF ni ya great thinkers bwana. na hii ionekane kwa taarifa za uhakika na zenye credible sources
 
Ishu ni frontliner wao mmoja kakubali kushindwa na hiyo inawaathiri aliokuwa anawaongoza..........tahadhari muhimu ofcourse
 
Nafikiri wanaohama CCM kwenda CHADEMA au vyama vingine hawapaswi kulaumiwa. Watanzania wote kwa namna moja au nyingine tulikuwa wanachama wa CCM kama siyo TANU. CCM ilikuwa kama DINI kwa watanzania. unazaliwa kwenye familia ya wakristo unakuwa mkristo, unazaliwa kwa waislamu unakuwa muislamu. Ila kadiri unavyokuwa na kujiuliza maswali unakuwa na uhuru wa kuhamia pale ambapo kiu yako inaondolewa. Kwa wale ambao wanahama kutoka CCM basi hawapaswi kulaumiwa kwa sasa, waachiwe watafute mahali ambapo kiu yao itapatiwa dawa. Kama wanaona ni CHADEMA basi wanakaribishwa, kama ni NCCR-MAGEUZI nako wanakaribishwa.... Kuhusu tabia zao, kila chama kina mfumo wake wa kupambana na watovu wa nidhamu. Ni kama timu ya Manchester United vs. Manchester City. Tevez alikuwa Man U lakini alikuwa hasikisi, ameenda City amekuwa msumbufu wa kutupwa! Walid Kaborou alikuwa CHADEMA akaenda CCM mnajua alikoishia, Mzee wa methali na misemo John Shibuda alikuwa msumbufu sana kule CCM akahamia CHADEMA nafikiri mnajua amefikia wapi na usumbufu wake... Labda kiu yake imekoma. Tuwakaribishe wote kwa mikono miwili na misemo yao na matendo yao ndiyo yatawapandisha au kuwazamisha, ili mradi sera, itikadi na nidhamu ya chama zinasimamiwa na uongozi uliopo, hakuna haja ya kuwa na wasi wasi.
 
Chama Cha Mapinduzi hakitaki mtoto wa mkulima na kama ukitaka kujua fuatilia kila Kiongozi mwanae ni mwana siasa je watoto wa mkulima hajui siasa?
Kama watakuja ni bora maana huko hakuna haki ya mtu wa chini
Maana viongozi wa CCM bado wamelala sitaki kuwataja kwa majina ila angalia kuanzia Marais waastafu, Makatibu wa chama, Mawaziri wakuu waastafu, Mawaziri waastafu, Wakuu wa mikoa wastaafu, Viongozi wa Usalama wastaafu nk. Hawa ni baadhi tu orodha ni ndefu lakini "VIONGOZI WAMELALA FOFOO NA HAWAONI JAPO WANAMACHO NA HAWASIKII JAPO WANAMASIKIO"
 
KADUMA ASEMA UTABIRI WA WAZEE CCM KUTIMIA, MUKAMA ASEMA WAKITOKA CHAMA KITAJUA CHA KUFANYAWaandishi WetuHATUA ya aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, James Ole Millya kujiondoa CCM na kuhamia Chadema imeanza kukitikisa chama hicho ikidaiwa kwamba wenyeviti watano wa mikoa wa umoja huo na kundi kubwa la vijana wako mbioni kumfuata.Wakati Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akisema kwamba chama chake kitajipanga endapo hilo litatokea, kada mkongwe wa chama hicho, Ibrahim Kaduma ameelezea uamuzi wa Ole Millya wa kukihama kwamba ni kutimia kwa utabiri wa wazee wa chama hicho.Hivi karibuni, Kaduma akiwa na makada wenzake wakongwe, Dk Hassy Kitine na Joseph Butiku wakihojiwa katika kipindi cha 'Je, Tutafika' kinachorushwa na Channel Ten, walikitabiria kifo chama hicho kwa kile walichosema ni kupoteza maadili yaliyoasisiwa na kiongozi wake wa kwanza, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Mbali ya wanasiasa hao, Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally alisema kuhama kwa Ole Millya CCM si jambo geni katika siasa za Tanzania, lakini akaeleza kushangazwa kwake na hatua hiyo ya kuhama kuanza kuwahusisha vijana.Wakizungumza na gazeti hili kuhusu maoni yao baada ya Ole Millya kuhama CCM, baadhi ya wenyeviti wa mikoa ambao waliomba majina yao yahifadhiwe walisema wengi wao na makatibu wa UVCCM wa wilaya, watakihama chama hicho kuanzia Juni hadi Septemba, mwaka huu wakidai hiyo ni kutokana na mwenendo usioridhisha na kupuuzwa kwa mawazo yao ya kutaka kukijenga chama.Mwenyekiti wa UVCCM kutoka mkoa mmojawapo wa nyanda za juu kusini, alisema makada wengi kutoka UVCCM watakihama chama hicho ifikapo Juni… “Watu wanamalizia vipindi vyao vya uongozi ambavyo vinakoma kati ya Juni na Septemba.”Alisema ukweli wa jambo hilo utathibitika wakati wa uchaguzi wa wenyeviti wa UVCCM wa mikoa ambao unatarajiwa kufanyika katika kipindi hicho.Mwenyekiti huyo alisema kati ya hao, yupo pia kiongozi wa juu wa jumuiya hiyo ambaye naye anasubiri muda tu akisema ni mapema mno kwake kufanya hivyo sasa.“Tumeshauri mambo mengi ndani ya chama na hata jumuiya, lakini hakuna hata moja ambalo limetekelezwa na zaidi kuna watu wamefanya hivyo wameonekana wabaya na kutengenezewa mizengwe,” alisema na kuongeza: “Kuna wenzetu ni wafanyabiashara na wengine wana nafasi nyingine za kisiasa katika mabaraza hivyo, ni mapema mno kuweza kujitoa kwa sasa, lakini kila mmoja anakerwa na mwenendo wa chama,” alisema huku akibainisha kwamba huenda wengine wakajitoa kabla ya wakati huo hasa wale ambao wana ajira zao.Akizungumzia madai hayo ya kuondoka na kundi la wana CCM hasa vijana, Ole Millya alisema wengi na wote waliokuwa wakimuunga mkono na kuchukia utendaji wa CCM, watamfuata.“Siwezi kusema ni lini, lakini subirini. Wengi wanakuja Chadema kutoka CCM na UVCCM kwani hawaridhishwi na uongozi na mambo yaliyopo sasa ndani ya CCM” alisema Millya.Mbali ya viongozi hao wa UVCCM wa mikoa, baadhi ya wenyeviti wa umoja huo katika baadhi ya kata na wilaya za Mkoa wa Arusha walisema wako njiani kujiunga na Chadema kama mapendekezo kadhaa waliyotoa ndani ya chama hicho hayatapewa uzito.“Tunasema kama wanataka tubaki, kwanza wamuondoe Katibu wa CCM Mkoa Arusha, Mary Chatanda kwani ndiye chanzo cha vurugu zote za Arusha na pia chama kitusikilize katika madai mbalimbali kuhusiana na makundi,” alisema mwenyekiti wa wilaya moja.Katibu wa CCM Wilaya ya Musoma, Feruz Bano ambaye amekuwa kiongozi wa UVCCM Arusha na maeneo mengine zaidi ya miaka 20 sasa, alisema kujiondoa kwa Millya ndani ya CCM kuna sura mbili.Alizitaja sura hizo kwamba ni kuonyesha jinsi vijana wanavyokosa uvumilivu na pia kutaka hatua zichukuliwe mapema ili kumaliza mpasuko wa viongozi Mkoa wa Arusha.Alisema wanachama wa CCM Mkoa wa Arusha, wanapaswa kuulizwa ni kwa nini migogoro inazidi ndani ya CCM katika mkoa wao ili kuhakikisha amani na utulivu vinarejea Arusha.“Mimi nimekuwa kiongozi wa UVCCM Arusha nakumbuka Arusha ilikuwa ni ngome ya CCM, tulikuwa na umoja na mshikamano, lakini inapaswa kujiuliza sasa tumekosea wapi hadi Arusha kuwa ngome ya Chadema?” alihoji.Mukama: Tutajua cha kufanyaAkizungumzia suala hilo jana, Mukama alisema hakuwa amepata taarifa hizo, lakini akasisitiza kwamba endapo itatokea, chama kitajua cha kufanya.“Hatujapata taarifa za wenyeviti wengine kujiondoa lakini, tukizipata tutajua tutafanya. Sasa hivi nipo katika kikao cha sekretarieti,” alisema na kukata simu.Utabiri wa wazeeKaduma ambaye aliwahi pia kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Kwanza, alisema ameshazungumza mambo mengi katika kitabu chake alichokiandika kiitwacho, 'Maadili ya Taifa na Hatima ya Tanzania.' “Ndiyo nilisema hivyo kwenye kipindi, sasa kama yametokea wewe mwenyewe utaona. Nenda kasome kitabu changu, nimeeleza kwa kina. Kama chama kimepoteza maadili unategemea nini?” alisema. Kwa mujibu wa kitabu hicho cha Kaduma, chanzo cha CCM kuporomoka kimaadili ni kuiacha misingi ya maadili iliyoasisiwa na TANU. Mtazamo wa wasomiBaadhi ya wasomi nao walisema kwamba kitendo hicho cha Ole Millya kukihama chama hicho tawala kuwa, ni mwanzo wa kusambaratika.“Hili ni zao la mizozo na makundi yaliyomo ndani ya CCM,” alisema Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Azaveri Lwaitama.Dk Lwaitama aliitaja baadhi ya mizozo hiyo kuwa ni ule uliozuka siku za hivi karibuni baina ya Ole Millya na Chatanda na msigano wa makundi.“Mizozo hiyo ndiyo iliyochangia CCM kupoteza kiti cha ubunge cha Arumeru Mashariki ambacho kimechukuliwa na Chadema,” alisema.Dk Lwaitama alisema hakushangaa aliposikia Ole Millya ametangaza kung’oka CCM, kwa sababu kwa jinsi mikwaruzano ndani ya chama hicho tawala inavyozidi kukua, asingekuwa na namna nyingine.Bashiru Ally kwa upande wake, mbali ya kushangazwa hatua ya kijana kuhama chama tawala alisema: “Kigeni kingine hapa ni kwamba Ole Millya amehama CCM wakati chama hicho na Chadema vikiwa kwenye uhasama na ushindani mkubwa.”Mshauri wa Chadema, Profesa Mwesigwa Baregu alisema CCM kimekuwa kikitabiriwa kufa na kusema hizo ni dalili kwamba kinameguka vipande kabla ya kusambaratika kabisa.“Picha ni moja tu, CCM inabomoka. Haijaanza leo. CCM ilitabiriwa kifo kwa sababu hiyo inaweza kufa au kupungua nguvu tofauti na watu wanavyofikiri,” alisema Profesa Baregu.Alisema jambo hilo ni zuri katika kukuza demokrasia ya nchi na hata utawala bora.Habari hii imeandaliwa na Mussa Juma, Arusha, Frederick Katulanda, Mwanza, Leon Bahati, Elias Msuya.Source: Mwananchi
 

• WAMO WENYEVITI WA MIKOA, WILAYA

na Waandishi wetu

WIMBI la viongozi na makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutimkia upinzani, limeanza kushika kasi baada ya jana diwani mmoja na katibu mwenezi wa UVCCM kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


Mjini Dodoma, Diwani wa CCM Kata ya Sombetini jijini Arusha, Alphonce Mawazo, alitangaza kuachana na CCM na kujiunga na CHADEMA kwa madai ya kuchoshwa na uonevu na udharimu wa viongozi wa chama hicho.

Aidha, taarifa za uhakika zimebainisha kuwa baadhi ya viongozi wa CCM kwa siku kadhaa sasa wamekuwa wakifanya mawasiliano na baadhi ya viongozi wa CHADEMA ili kujulishwa taratibu za kujiunga na chama hicho.


Mmoja wa watu waliotajwa kuwa katika maandalizi ya kukihama CCM ni mwenyekiti mmoja wa mkoa wa Kanda ya Ziwa ambaye, amedai kuwa msimamo wake umekuwa ukiwasumbua baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho.


Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi mpya ya CHADEMA, Diwani Mawazo alisema kuwa ameamua kuachia nafasi yake na kujiunga na CHADEMA ili aweze kuendeleza harakati zake za kuwatetea Watanzania maskini ambao wananyonywa na viongozi wa CCM.


“Nimeondoka mwenyewe katika CCM , nimeachia nafasi ya udiwani, natangaza kujiunga rasmi na CHADEMA, sijalazimishwa na mtu yeyote wala kuahidiwa kitu chochote, ila mimetambua sehemu muhimu ambayo inaweza kuwa ya sauti ya ukombozi kwa Watanzania ni kupitia katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo.


“Nataka kusema kuwa hakuna kiongozi hata mmoja ndani ya CCM ambaye ana dhamira ya kweli ya kuwasaidia Watanzania na badala yake viongozi wengi ndani ya chama wamekuwa wakijinufaisha wenyewe.


Diwani huyo alidai kuwa viongozi wengi ndani ya CCM wapo kwa jili ya kujinufaisha wao, na kwamba chama hicho kimepoteza matumaini kwa Watanzania kutokana na kutotatua matatizo ya wananchi, ndiyo maana ameamua kuingia katika chama ambacho kinahangaika kutetea masilahi ya watu.


Alisema amekuwa akijengewa chuki na baadhi ya viongozi wa CCM, pale anapojaribu kuwatetea Watanzania ambao ni wanyonge.


Mawazo aliifananisha CHADEMA kama sauti ambayo inawalilia Watanzania wengi maskini ili waweze kuneemeka na rasilimali zilizopo.


Kwa upande wake aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA) akitoa salamu zake kwa waandishi wa habari alisema kuwa kwa sasa CCM kinakaribia kufa.


“Nataka niwaambie kuwa katika Jiji la Arusha mambo ni shwari kabisa na msishangae kusikia hata Lukuvi anatuhunga mkono kwa kuwa mwanachama wetu,” alisema Lema.


Katibu mwenezi UVCCM naye atimka

Kutoka Arusha, Katibu wa Uhamsishaji wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) wilayani Longido, Yohana Laizer naye ametimka na kujiunga na CHADEMA.

Laizer alipewa kadi na Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani hapa, Samson Mwigamba, yenye namba 0445402 baada ya kukabidhi ile ya CCM yenye namba 683025 iliyotolewa Mei 04, 2004 Tawi la Kiserian, Monduli.


Akiongea jana na waandishi wa habari kwenye ofisi za mkoa za CHADEMA, Laizer alisema kuwa alifikia hatua hiyo ya kujivua uanachama na nyadhifa zote alizokuwa akishikilia baada ya kutoridhishwa na utaratibu wa viongozi kubebana huku wakiwakandamiza wananchi wa kawaida.


Kwa upande wake Mwigamba alimkaribisha Laizer kujiunga na kundi la wapambanaji huku akiwataka wananchi wengine kujitokeza na kujiunga na chama hicho alichodai kuwa kinaendelea kuongeza nguvu kwa ajili ya kushika dola kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.


Mwigamba alisema kuwa wao kama chama hawataacha kupokea watu wanaotaka kujiunga na CHADEMA ili mradi wawe na sifa za kufanya hivyo, ikiwemo kuhakikisha kuwa wana umri unaozidi miaka 18, akili timamu na wasiwe wanachama wa chama kingine cha siasa.


Alisema kuwa wanaelewa kuwa tatizo haliko kwa mwanachama mmoja mmoja bali ni mfumo wa chama hicho ambao umejikita katika misingi mibovu, ikiwamo kutafuta uongozi kwa kutumia rushwa na hila.


“CCM haiwezi kushinda uchaguzi wowote hapa nchini bila rushwa na hila kwani wananchi wamechoshwa nayo, maana hakuna jambo la kujivunia walilowafanyia wananchi hivyo inawalazimisha viongozi na wanachama wake kufanya mambo yasiyo halali ili iweze kushinda.


“Hawa wanaoamua kukataa kufanya kazi za kutumwa ndio wanakimbilia huku CHADEMA tufanye kazi ya kupigania wananchi, hivi mtu akiwa mpagani akaenda kanisani au msikitini kutubu na kubadilika watakataliwa eti kwa sababu alishakuwa mpagani?” alihoji Mwigamba.


Alisema kuwa yeye yuko tayari kumpokea hata mwenyekiti wa taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, na hata Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, endapo wataamua kufanya uamuzi wa kubadilika na kujiunga na CHADEMA.


“Lowassa akiamua kuondoka CCM ni lazima atakuwa na sababu za kufanya hivyo, lakini na sisi ni lazima atatueleza juu ya tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa kwake, tutamsikiliza, tukimwelewa hatutakuwa na sababu ya kumnyima uanachama,” alisema mwenyekiti huyo wa CHADEMA mkoani hapa.


Hata hivyo, aliwaponda viongozi mbalimbali wa CCM wanaotoa kauli za kumbeza aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM mkoani hapa, James Millya, ambaye alijiunga na CHADEMA wakidai kuwa alikuwa mzigo ndani ya CCM, kwa kuhoji kuwa kama alikuwa ni mzigo kwanini hawakuutua mpaka alipoamua kuondoka yeye mwenyewe.


“Mimi leo niko ndani ya CHADEMA ni kamanda, si kwa mavazi, bali matendo ya kupigania wananchi lakini nikihamia CCM nageuka fisadi kwa matendo, kwani kuna mambo nitayapigania kwa masilahi ya CCM ambayo yatawaumiza wananchi walio wengi,” alisema Mwigamba.



 
Wenyeviti Wa Mikoa na Wilaya Ndio NGUZO ya Chama Cha CCM na Wananchi; kama hizo Nguzo zikihama kuhamia Chadema,
CCM itakuwa na kazi kubwa kuwashawishi wananchi kukitambua CCM na kukichagua na kupata Mwakilishi wake...

Are we starting to view the wind of change which hit KANU it comes form the small mountain called Mt. Kenya
 
Naomba CDM waichukue NEC, CC na Cabinet yote!
Tujipange na Chama chetu.
 
karibu Lowasa chadema if and only if u tell us the truth with evidences kuhusu tuhuma zote dhidi yake.
 
Wenyeviti Wa Mikoa na Wilaya Ndio NGUZO ya Chama Cha CCM na Wananchi; kama hizo Nguzo zikihama kuhamia Chadema, CCM itakuwa na kazi kubwa kuwashawishi wananchi kukitambua CCM na kukichagua na kupata Mwakilishi wake... Are we starting to view the wind of change which hit KANU it comes form the small mountain called Mt. Kenya

yetu macho
 
Back
Top Bottom