Mkuu ni kweli mtu anaweza kuteuliwa hata akiwa nje ya kamati kuu lakini ukiwa ndani ya kamati kuu unakuwa na advantage kiasi. Kwa mfano mimi naamini CCM ikiendelea kusumbuliwa na CHADEMA hadi kwenye 2015 basi CCM itaibuka na Dr. John Pombe Magufuli ambaye inaaminika akisimama tu basi uchaguzi utakuwa umeisha na CCM kushinda kwa kishindo.
Lakini pia kuingizwa kwa Dr. Salim Ahmed Salim kwenye CC sijui kuna maana gani. Mimi nilidhani baada ya masaibu yaliyomkuta mwaka 2005, Dr. Salim asingekubali tena kuingia kwenye siasa angeamua kujipumzisha akila pensheni yake. Lakini sasa amekubali kuingia NEC na kisha CC. Kuna nini hapa? Je Dr. Salim Ahmed Salim anaweza kuwa kete ya CCM akiwa kama compromising candidate? Mkuu
Mchambuzi hekima zako kidogo katika suala hili tafadhali, hasa kuhusu CC na mustakabali wa CCM mwaka 2015.
Haya ni maoni yangu tu:
Kwanza - CC ya awamu ya nne haina nguvu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma – mkapa, mwinyi, nyerere kwani:
Basically, moja ya kazi zake ni kutengeneza agenda mbalimbali ambazo zinapelekwa NEC na kupitishwa kama maamuzi ya Chama, misimamo n.k. Sasa kwa zamani, wajumbe wa CC walitokana na wajumbe wa NEC ambao walikuwa ni wajumbe wazito na wenye influence na heshima ya kweli ndani ya NEC na Chama kwa ujumla kwa mujibu wa kanda, mikoa na taifa; hawa walikuwa na influence, respect, followers and loyalists wengi sana kwenye NEC, kwahiyo agenda nyingi zikipitishwa CC kupelekwa NEC, kulikuwa na almost 100% guarantee kwamba zitaungwa mkono; Nyakati hizi hali ni tofauti hasa baada ya mtandao kuchukua uongozi wa nchi 2005 kwani baada ya EL kujiuzulu 2008, ambae alikuwa ni key to ushindi wa JK 2005, na ambae amekuwa mjumbe wa NEC tangia 1982, ameondoka na loyalists, followers wengi, na wale waliobaki ni loyalists and followers wa kiti, not necessarily mwenyekiti.
Pili, ingawa in theory CC ndio chombo chenye nguvu kuliko vyote ndani ya CCM, in practice ni NEC hasa kutokana na Mwalimu kuona umuhimu wa maamuzi kufanywa na watu walio wengi zaidi ndani ya chama kama njia ya kukuza demokrasia na kupunguza misuguano kimaamuzi. Wakati wa Nyerere NEC ilikuwa na nguvu kuliko bunge la CCM na hata Katiba ya JMT (1977), na hali hii bado ipo kidogo katika nyakazi hizi. Kwahiyo focus yetu iwe zaidi katika NEC kuelekea 2015, CC is almost irrelevant katika kutupatia mgombea Urais unless wale wasiotakiwa waamue kutogombea kwa maamuzi yao wenyewe.
Tatu, ni dhahiri kwamba CCM imeshindwa kuvunja makundi, badala yake, CCM imefanikiwa kusimamisha vita hivi visiwe in public huku ikifanya nothing much kuvisimamisha in private kwani vita bado ni moto na vitazidi kushika kasi kuelekea 2015. Pia tumeshaona jinsi gani uchaguzi wa NEC ni kina nani walikuwa na nguvu kati ya makundi yote tajwa yaliyopo, na jinsi gani juhudi kubwa zilielekezwa huko compared to CC; Kuzima mapenzi ya wana CCM kwa viongozi Fulani Fulani imeshindikana,
kilichobakia na kinachoendelea sasa ni kucheza tu na psychology za wana CCM lakini pia umma kwamba kiti kikikuacha kwenye cheo Fulani, basi ina maana kwamba wewe haufai, na hii ni kwa mtindo wa zidumu fikra sahihi za wenyekiti wa CCM, kwani waumini wa hizi fikra bado wapo na watasaidia kuvuruga candidacy za watu Fulani Fulani kueleka 2015. So kuelekea 2015, wapo wana CCM ambao wataamini kwamba Fulani kaachwa kwa sababu hafai na hii itafanya safari ya wahusika kuelekea 2015 kuwa na bumps kidogo. Lakini pia kama njia ya kutuma ujumbe kwamba chama kinajaribu ku-heal siasa za makundi, pia imeonekana ni busara players wote wa makundi wasiteuliwe kuingia kwenye CC, huku hoja yangu in green hapo juu ikiendelea kufanya kazi;
Nne ni suala la Magufuli na Salim; Tukianza na Salim, zote ni efforts to heal makundi, hasa kumfanya yeye na wafuasi wake waegemee zaidi mmoja, na sio upande mwingine au wasiwe wana hang hang tu kwani wakiwa wapo wapo tu, ni rahisi sana kwa wao to sympathize na upande mwingine au kuwa open kusombwa na mgombea atakayekuwa na nguvu kuelekea 2015. Will it work? That remains to be seen. Otherwise iwapo mwalimu nyerere alijaribu mara mbili na Salim na kushindwa, sioni jinsi gani uongozi wa sasa wa CCM utaweza kupitisha kugombea Urais. He first needs to sort out tatizo lake na wenye chama (CCM/ASP) upande wa Zanzibar. Kuhusu Magufuli, pamoja na potentials zake kuwa juu, tatizo ni kwamba wenye chama hawamtaki kwani wao hawaangalii utendaji wa kazi bali ni usisi na uwao. Sioni magufuli kutumika unless dakika ya mwisho analysis iwe kwamba zinahitajika kura za kanda ya Ziwa na maeneo ya Tabora ili CCM ishinde kwa urahisi 2015 dhidi ya Chadema.
Mwisho – kwa jinsi hali ilivyo sasa, mgombea yoyote ambae atakuwa anaungwa mkono na kiti, huyo ataangukia pua, mgombea mwenye nafasi ya kupitishwa na NEC May 2015 kwa kura nyingi in the top three na pia kupita uchaguzi wa Rais November 2015 ni Yule ambae atakuwa hana support ya Kiti
wakati wa mchakato wa kupata mgombea. Vinginevyo CCM itashinda urais 2015 lakini tutarajie CCM kupata ushindi wa asilimia ndogo kuliko zote katika historia ya taifa – just over 50%, na ushindi wa namna hii upo wazi kwa mgombea yoyote atae simamishwa na CCM iwe ni Lowassa, Migiro, Mwakyembe, Membe, Magufuli, Sita, Mwandosya, January Makamba etc.
Again, haya ni maoni yangu tu Bwana Kimbunga, nasimama kupingwa;