Vigogo wapya wa urais 2015

Vigogo wapya wa urais 2015

Mkuu ni kweli mtu anaweza kuteuliwa hata akiwa nje ya kamati kuu lakini ukiwa ndani ya kamati kuu unakuwa na advantage kiasi. Kwa mfano mimi naamini CCM ikiendelea kusumbuliwa na CHADEMA hadi kwenye 2015 basi CCM itaibuka na Dr. John Pombe Magufuli ambaye inaaminika akisimama tu basi uchaguzi utakuwa umeisha na CCM kushinda kwa kishindo.

Lakini pia kuingizwa kwa Dr. Salim Ahmed Salim kwenye CC sijui kuna maana gani. Mimi nilidhani baada ya masaibu yaliyomkuta mwaka 2005, Dr. Salim asingekubali tena kuingia kwenye siasa angeamua kujipumzisha akila pensheni yake. Lakini sasa amekubali kuingia NEC na kisha CC. Kuna nini hapa? Je Dr. Salim Ahmed Salim anaweza kuwa kete ya CCM akiwa kama compromising candidate? Mkuu Mchambuzi hekima zako kidogo katika suala hili tafadhali, hasa kuhusu CC na mustakabali wa CCM mwaka 2015.
Nilimtabiri zamani!!
 
Back
Top Bottom