Vigogo wanaoichafua CCM kulimwa barua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo wanaoichafua CCM kulimwa barua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lilombe, Apr 15, 2011.

 1. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HALMASHAURI Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imemuagiza Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama, kuwaandikia barua viongozi wanaotakiwa kujiuzulu kuwafahamisha kwamba, kama hawatafanya hivyo kikao kijacho cha NEC kitawafuta uongozi.

  Watuhumiwa hao wa rushwa na ufisadi wakiwemo wajumbe wa NEC taifa, wamepewa muda wapime uzito wa tuhuma zinazowakabili, wajiuzulu.


  Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa, amesema NEC imeamua kubadili muonekano wa viongozi wake hivyo watuhumiwa wa rushwa, wabinafsi, waliojilimbikizia mali, na wanaojitafutia umaarufu watawajibishwa ipasavyo.


  “Tulisema tuwape muda, wao wenyewe, watafakari, wajipime, wajiuzulu… lakini wasipofanya hivyo, chama kitatoa maamuzi ya kuwawajibisha chenyewe”
  amesema Msekwa mjini Dodoma wakati wa mkutano wa kuwatambulisha wajumbe wa sekretarieti akiwemo Katibu Mkuu, Wilson Mukama.

  Kwa mujibu wa Msekwa, ufisadi umeathiri taswira ya CCM, na kwamba chama hicho kilifanya kosa la kuwakubali wafanyabiashara wasio waaminifu katika vikao vya CCM.


  “Bado wananchi wengi wanaionyooshea kidole CCM kuwa inakumbatia wala rushwa” amesema Msekwa na kubainisha kwamba rushwa imekuwa ni mzigo mkubwa sana katika chama hicho.


  “CCM imepoteza sifa yake ya awali ya kuwa ni chama kinachojali maslahi ya wanyonge na sasa inabebeshwa mzigo wa kuwa ni chama cha matajiri”amesema Msekwa.


  Amesema, CCM imejivua gamba, kimekuwa chama kipya, na kwamba jogoo amewika hivyo waamke. Msekwa amesema, maamuzi ya NEC CCM ilikuwa ni utekelezaji wa kufanya mageuzi ndani ya chama hicho kwa kujivua gamba mithili ya nyoka.


  Kwa mujibu wa Msekwa, NEC ilifanya maamuzi katika maeneo manne ikiwa ni pamoja kna kufanya mageuzi ya kuiwezesha CCM kupambana na ukoloni mamboleo unaoathiri siasa za nchi yetu.


  Amesema, CCM imefana mageuzi ya kubadilisha muonekano hasi wa chama hicho kwa wananchi, kujipanga upya ili kujiimarisha kishinde uchaguzi, na mageuzi ya kukiwezesha kupambana na maovu ukiwemo ufisadi na rushwa.


  Kwa mujibu wa Msekwa, CCM imeamua kusahihisha makosa ya nyuma kwa kubadili masuala mengi ikiwa ni pamoja na kutoteua wagombea wasiokubalika, na pia kitafanya mageuzi ili kuongeza wigo wa kuwa karibu na makundi ya watu.


  CCM pia imeamua kubadili utaratibu wa kumpata mgombea wake wa urais ili kuzuia matumizi makubwa ya fedha zinazonunua kura za wajumbe wa vikao vya uchujaji na vya uteuzi wa mwisho katika mchakato huo.


  “Makundi ya vinara wanaowania urais yamewagawa wanachama wetu na kuathiri umoja na mshikamano ndani ya chama kwa kiwango kikubwa sana” amesema Msekwa.


  “Tatizo hili ni kubwa na lina athari kubwa kwa chama chetu” amesema Msekwa na kubainisha kwamba, CCM pia imesitisha utaratibu wa kutoa kadi za uanachama za papo hapo.


  “Tumefanya mageuzi ya kubadilisha utaratibu wa kuingiza wanachama wapya kwa kufanya uamuzi kwamba, chama katika ngazi ya matawi kitenge siku moja maalumu katika mwezi ambapo wanachama wapya watapokea kadi zao kwa sherehe rasmi” amesema.


  Kwa mujibu wa Msekwa,
  CCM pia imebadili salamu yake, mtu akisema ‘ Kidumu Chama Cha Mapinduzi’ unaitikia ‘ Idumu CCM mpya’. CCM pia imebadili utaratibu wa utoaji kadi za uanachama wakati wa kura za maoni.

  “Tumefanya mageuzi ya kuweka muda wa mwisho wa utoaji wa kadi za wanachama kwa ajili ya upigaji kura za maoni uwe tarehe 31 Desemba ya mwaka unaotangulia mwaka wa uchaguzi mkuu husika” amesema Msekwa na kuongeza kuwa, CCM pia imebadili utaratibu wa uchaguzi wa chama na jumuiya zake


  “Kuanzia sasa tutakuwa tunafanya uchaguzi wa chama na jumuiya zake katika mwaka mmoja” amesema na kubainisha kwamba, uamuzi huo utaiwezesha CCM kupata muda wa kutosha wa kufanya kazi za chama ndani ya chama na kwa umma.


  Amesema, CCM pia imebadili utaratibu wa uteuzi wa wagombea wa CCM wa ubunge na udiwani, na kuanzia sasa watachujwa ili kupata wagombea wasiozidi watatu ambao watapigiwa kura za maoni.


  Msekwa amesema, CCM pia itaangalia uwezekano wa kuanzisha viwango vya ada vinavyotofautiana kulingana na kipato cha wanachama, kampuni za chama hicho ambazo hazifanyi kazi vizuri zitafutwa, na pia chama kitaangalia uwezekano wa kuuza baadhi ya mali zake ili kiwekeze kwenye miradi yenye tija.

  TAFAKARI!
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Nani msafi wa kumlima barua mwenzie?
  Nawashauri EL ra AC wasijiondoe ccm tuone kama wana ccm wanaudhubuti wa kuwasuta.
  Otherwise wakomae na JK kwa sababu walikula wote.

  Hivi Mkapa,Meghi wanafanya nini pale CC?
  jk mwenyewe gamba sasa sectetariet imlime barua kama haijipendi
   
 3. A

  Awo JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  CCM maneno meeeeeeeengi - hakuna cha maana. Sasa mbona hawawataji hao wa kulimwa barua. Dr Slaa alitaja mafisadi kumi na mmoja. Wawili wameshafikishwa mahakamani, tisa bado wanadunda ndani ya CCM irrespective of kujiviua gamba. Mengi alitaja watano, wote members wa CCM. Nani ataandikiwa barua? Acheni longolongo.
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  VIONGOZI WA UMMA WALIOKO KATIKA ORODHA HII WAMEKIUKA NA/AU KUVUNJA MASHARTI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO NA SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA KAMA IFUATAVYO:


  A. WALIOSHIRIKI MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI

  [​IMG]
  1. DR. DAUDI T.S. BALALI


  Dr. Daudi Balali amekuwa na bado ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania tangu mwaka 1997. Katika kipindi hicho cha miaka kumi, Gavana Balali amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:
  • Kufuatana na barua ya wataalamu wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali, ameruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia ufujaji wa fedha za umma unaodaiwa kufikia Shilingi 522, 459, 255,000 katika ujenzi wa majengo ya Benki Kuu ya Tanzania yaliyoko barabara ya Mirambo, Dar es Salaam na Gulioni, Zanzibar. Aidha taarifa kutoka vyanzo vingine zinaonyesha kwamba mwaka 1998 kampuni ya Skanska Jensen ya Sweden ilituhumiwa kutoa hongo ya Dola za Marekani milioni 5 kwa Gavana Balali tuhuma zilizopelekea kampuni hiyo kupigwa marufuku kushiriki tenda ya ujenzi wa majengo hayo. Hata hivyo, katika mazingira yanayoashiria ufisadi mkubwa, kampuni ya Group 5 ya Afrika ya Kusini ambayo ni kampuni tanzu
   
 5. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  2. ANDREW J. CHENGE

  [​IMG]

  Mheshimiwa Andrew Chenge ni Mbunge wa Bariadi Magharibi na Waziri wa Miundombinu katika Serikali ya sasa ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Kabla ya hapo, Mheshimiwa Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa miaka yote kumi ya utawala wa Rais Benjamin W. Mkapa. Kwa wadhifa huo, Mheshimiwa Chenge ndiye alikuwa "mshauri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo ya sheria na … aliwajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu mambo yote ya kisheria, na kutekeleza shughuli nyinginezo zozote zenye asili ya au kuhusiana na sheria…."[6] Katika kipindi hicho cha miaka kumi na mbili, Mheshimiwa Chenge amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:
  • Kama Mkurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited alishiriki na/au kufaidika na malipo haramu ya dola za Marekani 13,736,628.73 ambazo zimeelezewa kwa kirefu katika sehemu inayomhusu Gavana Balali;
  • Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki kuishauri vibaya na/au kutokuishauri vizuri Benki Kuu ya Tanzania na kusababisha ufujaji wa mabilioni ya fedha za umma ambayo yameelezewa katika sehemu inayomhusu Gavana Balali;
  • Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki moja kwa moja katika kutoa ushauri kwa Serikali na/au Wizara ya Nishati na Madini kuingia mikataba mibovu na makampuni mbali mbali ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limepoteza mabilioni ya fedha za kigeni. Kwa mfano, katika hotuba yake Bungeni tarehe 6 Novemba 2006, aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Bernard Membe alitoa taarifa kwamba katika kipindi cha miaka mitatu hadi kufikia 2006, makampuni ya uchimbaji dhahabu yaliyoko Tanzania yaliuza dhahabu yenye thamani ya shilingi bilioni 2,340 wakati ambapo makampuni hayo yalilipa mrahaba na kodi nyinginezo kwa Serikali za shilingi bilioni 72. Katika kikao cha Bunge la Bajeti la mwaka huu, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja aliliambia Bunge kwamba katika kipindi cha kuanzia mwaka 1998 Mgodi wa kwanza wa dhahabu wa Lusu Nzega ulipofunguliwa hadi mwaka huu, makampuni ya uchimbaji dhahabu yaliuza nje dhahabu yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 2.614 wakati Serikali ikiambulia mrahaba wa dola milioni 78 tu! Endapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Chenge angeishauri vema Serikali ya Jamhuri ya Muungano kama alivyotakiwa na Katiba ya nchi yetu, taifa lisingekuwa linapoteza utajiri wake wa madini kwa kiasi kikubwa namna hii.
   
 6. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  3. BASIL P. MRAMBA

  [​IMG]

  Mheshimiwa Basil Mramba ni Mbunge wa muda mrefu wa Jimbo la Rombo na Waziri wa Viwanda na Biashara na kwa miaka kumi ya utawala wa Rais Mkapa alikuwa ndiye Waziri wa Fedha. Katika kipindi hicho cha miaka kumi, Mheshimiwa Mramba amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:
  • Kwa kutumia wadhifa wake kama Waziri wa Fedha, alishinikiza kampuni ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation ya Washington DC, Marekani kupewa kazi ya kukagua mahesabu ya makampuni ya uchimbaji dhahabu. Chini ya mkataba wake na Serikali ya Tanzania, Kampuni hiyo inalipwa asilimia 1.9 katika ya asilimia 3 za mrahaba inaolipwa Serikali ya Tanzania na makampuni ya madini ya dhahabu. Kufuatana na barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, katika mwaka wa fedha 2005/06, Alex Stewart (Assayers) walilipwa shilingi 14,175,753,189.46 kama malipo ya ukaguzi wa mahesabu ya makampuni ya dhahabu, ijapokuwa "hakuna ripoti za ukaguzi zilizowasilishwa na wakaguzi hawa kuhusu ukaguzi uliofanywa katika mwaka 2005/06"! Vile vile Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu alisema katika barua yake kwamba "hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kwamba wakaguzi hawa wa dhahabu walipatikana kwa kufuata utaratibu wa zabuni ya ushindani."
   
 7. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  4. GRAY S. MGONJA

  [​IMG]
  Bwana Gray Mgonja ni Katibu Mkuu wa siku nyingi wa Wizara ya Fedha. Vile vile ni Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania na anashikilia nafasi ya ukurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited ambayo maelezo yake tumeyatoa kuhusiana na ufisadi unaomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge. Kwa kuzingatia nafasi yake kama Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Mkurugenzi katika Benki Kuu na vile vile Mkurugenzi katika Tangold Ltd. iliyolipwa mabilioni ya fedha za umma katika mazingira yenye utata mkubwa, ni wazi kwamba kumekuwepo mgongano mkubwa wa kimaslahi unaomhusu Bwana Mgonja.
   
 8. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  5. PATRICK W.R. RUTABANZIBWA

  [​IMG]
  Kwa miaka mingi Patrick Rutabanzibwa alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini wakati mikataba mibovu ya madini inasainiwa na kashfa kubwa ya IPTL inatokea. Kwa sasa Bwana Rutabanzibwa ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na vile vile Mkurugenzi wa kampuni ya kigeni ya Tangold Limited. Ufisadi unaomhusu umeelezewa kwa kina katika maelezo yanayomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge. Hapa pia kuna mgongano mkubwa kati maslahi yake binafsi kama Mkurugenzi wa kampuni binafsi iliyopokea mabilioni ya fedha za umma na maslahi ya umma aliyotakiwa kuyalinda akiwa kama kiongozi wa umma
   
 9. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #9
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  6. NIMROD ELIREHEMA MKONO

  [​IMG]
  Mheshimiwa Nimrod E. Mkono ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijiji na Mshiriki Mkuu wa kampuni ya mawakili ya Mkono & Company Advocates ya Dar es Salaam. Barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali inaainisha kuwa Benki Kuu imekuwa ikilipa malipo makubwa kwa Mkono & Co. Advocates hasa yale yanayohusu kesi ya Valambhia ambapo Benki Kuu inadaiwa jumla ya shilingi bilioni 60. Kwa mujibu wa barua ya wakaguzi tayari Mkono & Co. Advocates wamekwishalipwa shilingi 8,128,375,237 kwa fedha taslimu kwa kesi hiyo ambayo bado iko mahakamani. Malipo haya ni sawa na asilimia 13.5 ya deni lote inalodaiwa Benki Kuu. Hoja ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu ni kuwa kesi hii haina muda maalumu wa kumalizika na hivyo inawezekana kabisa malipo ya wanasheria yakazidi kiasi cha fedha inachodaiwa Benki Kuu.
   
 10. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  hapa ccm imefika patamu yaani kama harusi basi wako kwenye kulishana keki hapa kuna watakaoumbuliwa ambao wanadhani historia hufutika kama uliwahi kunufaika na ufisadi kwa namna yoyote na wewe fisadi .
  Kikwete kama unania ya kuirudishia ccm heshima basi tangaza kuvunja baraza la mawaziri na wewe ujiuzulu kwani fedha zilizokuweka madarakani ndizo zinatutesa watanzania mpaka leo .
  Epa ndiyo ikazaa Richmond na sasa sijui inataka kutaga nini yarabi
  jk huna pa kutokea katika hili wewe ni gamba kama alivyo RA EL na EC
   
 11. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #11
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  7. NAZIR KARAMAGI

  [​IMG]
   
 12. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #12
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  8. ROSTAM AZZIZ

  [​IMG]
   
 13. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #13
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  9. EDWARD LOWASSA

  [​IMG]
   
 14. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #14
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  10. BENJAMIN WILLIAM MKAPA


  [​IMG]

  Benjamin William Mkapa alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 alipomaliza kipindi chake cha pili. Ufisadi wote ulioelezewa katika waraka huu ulitokea wakati wa utawala wa Rais Mkapa na anawajibika nao moja kwa moja ama kwa kuubariki au kwa kuunyamazia. Zaidi ya hayo, kuna ushahidi unaoonyesha kwamba wakati akiwa madarakani Rais Mkapa alishiriki moja kwa moja au kwa kutumia ndugu na/au washirika wa karibu wa familia yake katika ufisadi mkubwa na uliolipotezea taifa fedha nyingi. Kwa mfano, wakati akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mkapa alitumia wadhifa huo kuhakikisha kwamba kampuni iitwayo Tanpower Resources Limited inamilikishwa asilimia 85 ya hisa za kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd. inayochimba mkaa wa mawe huko Kiwira Mkoani Mbeya. Hisa zilizobaki asilimia 15 zinamilikiwa na Serikali. Tanpower Resources Ltd. ni kampuni iliyoanzishwa kwa ajili ya kuinuifaisha familia ya Rais Mkapa na washirika wake wa karibu. Taarifa za BRELA zinazonyesha kwamba wakurugenzi wa Tanpower Resources Ltd. ni Anna Mkapa, mkewe Rais Mkapa, Nicholas Mkapa, mtoto wa Rais, Bwana Joseph Mbuna, wakili wa kujitegemea na baba mkwe wa Nicholas Mkapa, Daniel Yona, Waziri wa Nishati na Madini wakati wa utawala wa Rais na bwana Joesph Mapundi. Baada ya Tanpower Resources Ltd. kutwaa umiliki wa Kiwira Coal Mines Ltd. kwa nguvu za Ikulu ya Rais Mkapa, iliingia mkataba na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini TANESCO wa kujenga mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mkaa wa mawe na kuiuzia umeme TANESCO. Mkataba huo utainufaisha kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd., na kwa hiyo Rais Mkapa, familia na washirika wake wa karibu kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 271 kwa wakati wote wa mkataba.
   
 15. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #15
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  11. RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE


  Rais Jakaya Kikwete amekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Desemba 2005. Kabla ya kuwa Rais, Mheshimiwa Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo Nje na Uhusiano wa Kimataifa kuanzia 1995 hadi 2005, Waziri wa Fedha 1994 hadi 1995 na Waziri wa Maji, Nishati na Madini kuanzia mwaka 1990 hadi 1994. Kama Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mheshimiwa Kikwete alishiriki moja kwa moja katika kusaini mikataba mibovu ya madini na makampuni ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limeendelea kupoteza utajiri mkubwa na kuinyima Serikali uwezo wa kifedha wa kuhudumia wananchi. Kwa mfano, mnamo tarehe 10 Aprili 1990, Major Jakaya Mrisho Kikwete aliingia mkataba wa madini ya kampuni ya SAMAX Limited ambapo kampuni hiyo ilipewa leseni ya kuchimba dhahabu katika eneo la Lusu, Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora. Matokeo ya mkataba huo, maelfu wa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu waliokuwa eneo hilo waliondolewa kwa nguvu na vikosi vya FFU na bila ya kulipwa fidia yoyote. Hadi leo wananchi hao hawajalipwa fidia yoyote licha ya miaka zaidi ya kumi ya kufuatilia haki zao. Baada ya kutwaa utajiri wa dhahabu wa eneo hilo, SAMAX Limited iliuza eneo hilo kwa kampuni ya Ashanti Goldfields ya Ghana kwa dola za Marekani milioni 253. Ashanti Goldfields nao wakauza eneo kwa kampuni ya Resolute Limited ya Australia kwa kiasi kisichojulikana cha fedha za kigeni. Resolute Limited ndio waliojenga na wanamiliki Mgodi wa Dhahabu wa Golden Pride ulioko eneo la Lusu, Nzega hadi sasa na ambao ulifunguliwa mwezi Novemba 1998. Mnamo tarehe 5 Agosti 1994 Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete aliingia tena mkataba na kampuni ya madini Kahama Mining Corporation Ltd., kampuni tanzu ya kampuni ya Sutton Resources ya Canada. Ijapokuwa mkataba huu unaonyesha wazi kwamba ulikuwa unahusu eneo la Butobela Wilaya ya Geita Mkoani Mwanza, mwezi Agosti mwaka 1996 Kahama Mining Corporation wakisaidiwa na vikosi vya FFU walivamia eneo la Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga na kuwaondosha kwa nguvu watu takriban laki nne waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika eneo hilo. Baada ya kutwaa eneo hilo kwa nguvu za kijeshi, Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na Bulyanhulu kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada kwa dola za Marekani milioni 280. Leo hii Bulyanhulu ni moja ya migodi tajiri kwa dhahabu katika Bara la Afrika.
   
 16. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #16
  Apr 15, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,374
  Likes Received: 3,137
  Trophy Points: 280
  maneno mbofumbopfu................wafie mbele huko hatutaki chama kilichokosa ubunifu na fikra pevu za kuisogezA NCHI KUTOKA HAPA TULIPO
   
 17. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #17
  Apr 15, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Naomba wasijiuzulu ili tuone watafanyaje
   
Loading...