Vigogo wanaingilia mgawo wa umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo wanaingilia mgawo wa umeme

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Petiro, Mar 12, 2011.

 1. Petiro

  Petiro JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Saturday, 12 March 2011 10:29

  Fredy Azzah
  WAFANYAKAZI wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wameishutumu Wizara ya Nishati na Madini kwa kutoa maagizo ya upendeleo wa kutokata umeme katika baadhi ya maeneo wanayoishi vigogo wa serikali katika utekelezaji wa mpango wa mgawo wa umeme nchi nzima.
  Hayo yalibainishwa jana kwenye mkutano wa wafanyakazi wa Tanesco wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani uliofanyika makao makuu ya shirika hilo, Ubungo, Dar es Salaam jana.

  Mkutano huo ulitokana na maazimio ya Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Viongozi wa Matawi ya Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha na Huduma za ushauri (Tuico) Tanesco, uliofanyika Januari 12 mpaka 15 mwaka huu mjini Dodoma.

  “Kuwe na usawa wa mgawo wa umeme kwani kwa kuzingatia maeneo fulani fulani na mwingiliano wa njia zetu za umeme, mitaa ya jirani huonekana kupata umeme kila siku hali hiyo inasababisha wafanyakazi kuonekana wanakula rushwa na kutoa mgawo kwa upendeleo,” alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Maazimio hayo, Abdul Mkama na kuongeza; “Kuna maeneo wanakaa waheshimiwa, tunaambiwa tusikate umeme. Hii siyo sawa! Kwani wao siyo watanzania?"

  Alisema wakati wakubwa hao wanaambiwa wasikatiwe umeme, baadhi yao majumbani mwao kuna jenereta za umeme zilizonunuliwa na Tanesco ili zitumike nyakati za dharura. Vilevile wafanyakazi hao walipinga vikali kitendo cha wateja wa shirika hilo waliopo Zanzibar kutoingizwa kwenye mgawo.

  Walisema licha ya kutoguswa na mgawo pia wanalipa fedha kidogo ikilinganishwa na inayolipwa na wateja wa Tanzania Bara... “Tunaikumbusha Serikali kuhusu tariff ilipwayo na Shirika la Umeme Zanzibar kwamba ni ya kibiashara au msaada? Kwani pamoja na kutolipwa ipasavyo pia haihusiki na mgawo wa umeme.”

  Mkama alidai kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ndiyo mdaiwa sugu akisema hadi Mei mwaka jana, ilikuwa ikidaiwa Sh56.3 bilioni.Alisema mkutano huo unaitaka Wizara ya Nishati na Madini kurejesha mali za shirika hilo ikiwa ni pamoja na Chuo cha Morogoro na Kidatu, Jengo la Hospitali ya Tumaini, Kiwanda na Shamba la Miti Mbeya na Jengo la shirika hilo lililopo Mtaa wa Samora ambalo kwa sasa linatumiwa na wizara hiyo.

  “Naye, (Waziri wa Ujenzi John) Magufuli anatutishia anasema atavunja hili jengo (la Makao Makuu ya Tanesco) lakini tunamtaka wakati katapila lake likiwa hapa nje, ahakikishe kuwa Waziri (William Ngeleja (Wizara ya Nishati na Madini) naye awe ameanza kutoka kwenye jengo letu analolitumia kuwa ofisi yake kwa sasa. Tumechoshwa na mitizamo ya kisiasa ambayo ndiyo imelifikisha shirika hili hapa lilipo,”

  Azimio jingine la mkutano huo wa Dodoma ni kuwa serikali inasimamia madeni yote ya shirika, ikiwa ni pamoja na madeni ya serikali. Mkama alisema katika mkutano huo walikubaliana kuwa serikali kupitia Wizara ya Nshati, iwaeleze wananchi kisa cha bei ya umeme kuonekana kubwa kwamba inachangiwa na makusanyo ya kodi ya Serikali VAT ya asilimia 18, asilimia moja ya Ewura, huku Rea wakikata asilimia tatu.

  “Waziri pia awaeleze mchango wa capacity charge (gharama za uendeshaji) inayolipwa na Tanesco na Serikali kwa kampuni binafsi zinazozalisha umeme," alisema. Alisema kampuni hizo zimeingia mikataba mibovu na Serikali na sasa inakuwa lazima kulipa hata kama hazizalishi. Alitoa mfano wa mikataba hiyo mibovu akisema Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) inalipwa Sh 3bilioni kwa mwezi na Songas Sh 6.4 bilioni: "...Serikali isipofafanua hilo tutachukua jukumu hilo na kuweka bayana kwa Watanzania."

  Wafanyakazi hao wameitaka serikali kupitia upya mikataba ya IPTL na Songas kwani ni mzigo mkubwa kwa shirika hilo... “Hivi mtu unakwenda kwa mama lishe, anakwambia leta unga, moto, mafuta, mboga, nikupikie ugali mimi nina sufuria, unakwenda kununua akija akishakupikia anakuuzia tena kile chakula...! Ndivyo Serikali inavyofanya kwa mashirika haya.
  Hii ni biashara kichaa.” Mkama alisema azimio jingine ni kuitaka serikali kutoa tamko juu ya Kampuni Tanzu ya Artumas –Umoja Light Ltd, ambayo imeshindwa kufanya biashara ya umeme katika Mikoa ya Lindi na Mtwara kama ilivyotakiwa.

  “Artumas pamoja na kuwezeshwa na Serikali kwa kupatiwa vitendea kazi hususan magari, hawajafanya chochote mpaka sasa. Hii imezua migogoro baina ya wafanyakazi wa Tanesco na wananchi,” alisema Mkama.


  Source: Vigogo wanaingilia mgawo wa umeme
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli ukisoma habari hii utabidi ubebwe kwenye machela kupelekwa kwa Babu Loliondo haingii akili kabisa jinsi watu wanavyochezea nchi yetu mbaya sana
   
 3. Kiwi

  Kiwi JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Msimamo wa vigogo wa Tanzania ninauona hauna tofauti na walivyoamua nguruwe mwitu (hogs) kwamba "We Are Equal, But Some Are More Equal Than Others" - Animal Farm

  Enzi zetu tulikuwa na Imani za TANU, na tulikuwa tunakiri kwa sauti kila siku asubuhi. Kwa waliosoma enzi hizo kila siku asubuhi kabla ya kuingia madarasani tulisimama assembly na kutamka kwa sauti yenye uhakika wa kile tulichokuwa tunakisema. Ninakumbuka kiasi ingawa sio zote, labda wengine wenye umri kama wangu na kunizidi pia watakumbuka

  Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja
  Kila mtu anastahili heshima
  Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote
  Cheo ni dhamana, sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu
  Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa

  Mlolongo ulikuwa mrefu mara tu baada ya Azimio la Arusha tuliimba imani ya TANU kwa moyo mmoja.
  Ikaja CCM tukaendelea na mawazo hayo hayo.
  Leo kuna ccm, who cares?
  Wakisema CDM wanaambiwa wanavuruga amani.

  Mungu Ibariki Tanzania!
   
Loading...