Vigogo waliomuua Amina Chifupa

Huyu Mzee aache kujikanyaga sasa. Yaani ameamua kuanza kutafuta umaarufu kwa nguvu kupitia kifo cha mtoto wake???!!!!

Eti amekufa kama Nabii Isa......KUFURU hii. Amina si ndo huyo tunasikia alikuwa anarukaruka kama kindege tu .... anafananishwa vipi na manabii???!!!

Alikuwa na maajabu.... Maajabu ya kutangaza redio au ya kufanyaje??? Huyo mtoto hata shule alishindwa kusoma ...halafu leo alikuwa wa ajabu.

Huyo mzee anatakiwa kushauriwa. Kila mtu angependa kumuona mtoto wake wa ajabu. Lakini kama wewe unamuona wa ajabu uwe unashangaa uajabu wake ndani kwako. Unaita waandishi wa habari kutoa pumba

Eti kaburi la milion tatu linafanana na Amina.... ama kweli alikuwa mtoto wa ajabu !!! Kama alikuwa anafanana na kaburi ni ajabu na kweli. Mzee anatakiwa kushauriwa nini anaongea kwenye vyombo vya habari sio kukurupuka tu.
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha
 
tuwe macho na hizi fikra za ushrikina, zinalipeleka taifa mahali pabaya! fikra za ushirikina ndo chanzo cha mauaji ya wazee wetu vikonngwe huko shinyanga

kuhusisha kifo cha amina ambaye mnasema alikuwa kiruka njia(mimi sina uhakika) ni mwendelezo wa yale yale ya kutoamini kuwa mwenyezi MUngu, Bwana wa Majeshi, ndo mwamuzi wa uhai kutokuendelea.

Ripoti ya Kifo cha amina inaweze kupatikana wazi pale hospitalini alikokuwa amelazwa. ukiniambia ni nani aliharakisha kifo hiki ninaweza kusema kuwa ni huyu mzee, kwa kutompa nafasi mwanawe atoe mafundo yaliyokuwa moyoni

haya ya kujenga makaburi ya 3m nakadhalika ni kuchanganyikiwa,

hivy mumewe amina yule mtaka masifa sana, yuko wapi siku hizi? angekuja hapa ajibu.
Mpaka njia ameshakufa zamani
 
Amina hajazaliwa Lugalo, na zaidi ya hayo hakuzaliwa Dar es Salaam. Alizaliwa kijiji cha Lupembe au jina kama hilo huko Iringa. Na mimba yake kweli ilikuwa na mizengwe mizengwe.

Ni wewe ndo uliingiz mimba yake nini?
Okay,hongera zako!
 
Hakuuwawa na mtu, alijiuwa mwenyewe kwa ulimbukeni wa uchangu, kwani hukumbuki mme wake Med Mpakanjia, au ulikuwa bado unanyonya?
 
Mzee kwishine! Amekuwa kama yule jamaa Wa gazeti baada ya kudhurumiwa alivyorusha vijembe! Cheza na wazungu! Huyo nabii ukienda mkuta sijui utamwambia nini, maana umemfananisha na mwanao!
 
Mungu amlaza mahali pema ..amin
lakini nina masuali ..mara nyingi kumekuwa na maneno kuwa Amin alikua ndio pekee alijitolea kupigana na wauza unga..well fine..
jee mapambano yake ni yapi ?
jee aliwahi kuwataja watu wanao husika ?
jee aliwahi kupeleka orodha ya wauza unga bungeni au polisi ?
ugonjwa wake ulianza mara baada ya kupewa talaka na mumewe kwa sababu za wivu
jee Mumewe alikua akitajwa kwa Title maaruf 'Mpakanjia mfanabiashara maaruf' ni biashara gani akifanya mumewe ?
kuna ugomvi wake alowahi kuutaja na UVCCM
hebu mwenye maelezo kamili ya vipi alipigana au kujitolea kupugana na madawa..maana sioni katika kumbukumbu zaidi ya hotuba bungeni..Hata huyu cheki bobu wetu wa Dar kajitolea kweli kutaja watu mashuhuri japo ni uongo..Amina sijawahi kuona alifanya nini
kwa mujibu madaktari amina alikufa kutokana na depression ...
 
haya ndiyo mambo gani sasa... tulipopiga kelele mumpeleke hospitali nyie mkampeleka kupigiwa ramli!

Mimi nimesoma katikati ya misitari na nimeelewa kuwa anafanya fund rising ya huo mfuko Wa Amina Chifupa.Na vile vile amejaribu kutoa report ya matumizi kwa kusema wamejenga Kaburi kwa 3mls na kwamba kuna "kamati" iko engaged kwenye investigation ya chanzo cha kifo.Hiyo investigation hadi leo haimaliziki? Amina ana muda gani toka afariki dunia? Hiyo "kamati/tume" inaundwa na watu Wa aina gani? Haya anasema probable cause ni ushirikina na labda poisoning.Sasa atuambie hiyo kama chunguzi ina forensic chemists na wagangua uchawi? Hivi kwa nini nchi hii watu huongelea mambo mazito kimzaha mzaha tu? Hivi uchunguzi Wa kifo unaweza kufanywa kurahirahisi hivyo tu? Hili Taifa let us go back to the basics of our education failure.It is until and unless we rediscover that we are mentally corrupted then no any remarkable development will be scored as a nation and individuals.Anasema wachawi? Hao wachawi wako wapi? Nguvu zao ziko wapi? Kuna makontena pale Bandarini zimejaa dhahabu kama hao watu walipata uwezo Wa kumuua Amina kwa nini wasiende kuchukua mapande ya dhahabu toka kwenye makontena yale? Hao wachawi wameridhika na maisha? Hawataki kutajirika? Nonsensical!
 
Back
Top Bottom