kkiwango
Senior Member
- Aug 27, 2007
- 173
- 14
Mzee Chifupa: Bado tunachunguza vigogo waliomwua Amina
na Prisca Nsemwa
DUNIA imetakiwa kusimama imara na kwa nguvu ili kupinga dawa za kulevya kwa kuwa zina athari kubwa kwa jamii, hasa vijana.
Katibu wa Mfuko wa Amina Chifupa ambaye pia ni baba wa Amina, Luteni Hamis Chifupa alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), ambapo alikifananisha kifo cha mtoto wake na cha Yesu Kristo au Nabii Issa.
Alisema amemfananisha marehemu Amina na manabii hao kwa kuwa alikuwa na maajabu, hivyo kutokana na maajabu hayo pamoja na mambo mazito aliyoyafanya enzi ya uhai wake, familia imejenga kaburi lenye thamani ya zaidi ya sh milioni 3 ambalo linafanana na uzito huo.
Amina amekufa kama Nabii Issa aliyekufa na alivyozaliwa, ndiyo maana familia imejenga kaburi linalofanana na uzito wake ingawa Issa bin Mariamu hana kaburi duniani, alisema Chifupa.
Pia alisema Amina alikufa akiwa vitani akipagania vijana wanaoharibika kwa kutumia dawa za kulevya na wale wanaosambaza dawa hizo.
Akizungumzia ugonjwa uliosababisha kifo cha Amina, alisema kuwa ni kisukari na ushirikina, na kuongeza kuwa kifo chake kimeharakishwa na watu ambao hivi sasa familia inaendelea na uchunguzi na mara baada ya kumalizika watatoa matokeo.
Wakati Amina anaumwa alikuwa akitaja majina ya watu wazito ambao wengine ni viongozi na wafanyabiashara, hivyo tunafanya uchunguzi wetu wa kimya kimya kwa kuwa hatujui aliyataja majina yale kwa mazuri au mabaya, na tukimaliza tutayataja hapa hapa kutimiza maandiko yake, alisema.
Luteni Chifupa alisema kuwa kaburi la Amina ni la kihistoria nchini kwa kuwa limejengwa kwa mfano wa kaburi la Shariff Musa ambaye ana makaburi saba duniani.
Amina ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), alifariki Juni mwaka jana.