Vigogo wa Uhamiaji Wapanguliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo wa Uhamiaji Wapanguliwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shadow, Feb 8, 2012.

 1. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Leon BahatiMAKAMISHNA watatu wa Idara ya Uhamiaji nchini, wamesimamishwa kazi ikiwa ni siku 20 tangu Waziri wa Mambo ya Ndani , Shamsi Vuai Nahodha atangaze kufanya mabadiliko ya kiutendaji ndani ya idara hiyo.

  Januari 17 mwaka huu, Nahodha alitangaza kufanya mabadiliko katika idara hiyo ili kuongeza tija na kukabiliana na mambo mbalimbali ikiwemo kudhibiti uingiaji nchini wa wahamiaji haramu.

  Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi, umebaini kwamba makamishna hao watatu (majina tunayo) jana walipewa barua za kuondoka kwenye nafasi zao na kutakiwa kuripoti wizarani ili kupangiwa kazi nyingine.

  Hata hivyo, baadhi ya watumishi wa idara hiyo wamechukulia uamuzi huo wa kusimamishwa kazi makamishna hao kama wa kisiasa."Uamuzi huu umefanywa kisiasa.

  Nafikiri hawa wakubwa wana watu wao ambao wanataka kuja kuwaweka kwenye nafasi hizo," alisema mmoja wa watumishi wa Idara ya Uhamiaji, kwa ombi la kutotajwa gazetini.


  Source: Mwananchi
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Sina imani na Mzanzibar kutuongoza sisi watanganyika.
   
 3. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Wanao fanya kazi uhamiaji tupeni habari Pls.
  Na sikia mmoja wapo ni Bashiri.m. Kapelekwa Mtwara.
  Alikuwa anahusika na utoaji vibali vya kuishi.
  Cha ajabu kama kweli Ni kuruka mkojo na kukanyaga kinyesi.
  Maana mtwara ni mpakani na ataendelea na libeneke yake.
   
 4. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Wanao fanya kazi uhamiaji tupeni habari Pls.<BR>Na sikia mmoja wapo ni Bashiri.m. Kapelekwa Mtwara.<BR>Alikuwa anahusika na utoaji vibali vya kuishi.<BR>Cha ajabu kama kweli Ni kuruka mkojo na kukanyaga kinyesi.<BR>Maana mtwara ni mpakani na ataendelea na libeneke yake.
   
 5. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  jamani waziri alisema wale wote waliokaa kituo kimoja cha kazi kwa zaidi ya miaka 8 watahamishawa, sasa tunaona kimya vp? mliopo jikoni tupaeni habari kama kuna barua za uhamisho zinakuja.
   
 6. K

  Kampemba Member

  #6
  Feb 8, 2012
  Joined: Jul 24, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kapigwa changa Mpemba nivisasi tu wengi walio hamishwa ni kwa husda tu si kwa tija kama anavyo tarajia:Mfereji vuta subira nadhani utakuwa Mtwara wewe Rukwa tayari
   
 7. k

  kajunju JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Wameshindana kwenye deal au alikuwa hapewi 10%.
   
Loading...