Dar es Salaam. Kashfa ya kupanga matokeo na hatimaye kushushwa daraja kwa timu nne imechukua sura nyingine baada ya watendaji waandamizi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kudaiwa kuomba fedha.
Watendaji hao, Juma Matandiko na mwenzake ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya TFF wanadaiwa kuomba Dola 25,000 (zaidi ya Sh54 milioni) kutoka kwa uongozi wa Geita Gold ili waisaidie timu kupanda daraja.
Viongozi hao, sauti zao zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii wakishawishi ili wapewe fedha, huku timu hizo zikilalamikia kitendo hicho.
“Wao wamemwaga mboga, sisi tutamwaga ugali, ushahidi tunao walitaka tuwape Dola 25,000 ili watusaidie kuhakikisha tunapanda daraja na isitoshe kuna muda Matandika alipigiwa simu, akasema anamalizia kazi ya jamaa, ameagizwa na rais (Jamal Malinzi) aikamilishe, huyo jamaa ni nani?
“Yeye aliingia kwenye kamati kama nani? alihoji kiongozi mmoja ambaye ni mwathirika katika sakata hilo.
Aliongeza: “Tunasubiri tupewe hukumu yetu ndiyo tumwage mboga, tuna vielelezo.”
Chanzo: Mwananchi