Vigogo kumvua ubunge Shibuda

Vigogo kumvua ubunge Shibuda

macho_mdiliko

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2008
Posts
28,237
Reaction score
56,881
MBUNGE wa Maswa Magharibi, John Shibuda, anaweza kupoteza ubunge wakati wowote , Raia Mwema, limeelezwa.

Hiyo inatokana na chama chake, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kumtuhumu kwa kukihujumu na hivyo kupanga kumvua uanachama. Mbunge akikoma kuwa mwanachama wa chama kilichomsimamisha, anakoma kuwa mbunge...

More: Raia Mwema - Vigogo kumvua ubunge Shibuda
 
Wamuache tu, kwani wachawi tunao, tunaishi nao tunawajua lkn tunawapotezea tu, wampotezee akiondoka kimoja
 
Anasubiri tu mkimvua anakimbilia kortini ,nae anaendelea kuwa mwanachama na mbunge wa Mahakama!hadi week kabla uchaguzi mahakama inaridhia kuwa kweli alistahili kufukuzwa uanachama!basi anatoka rasmi anahamia chama kingine
 
Hakuna Mbunge atakayeefukuzwa CHADEMA ....!
Suala zima la kupunguza ruzuku ndilo linaloangaliwa
 
Mimi naunga mkono hoja, madame tumeshamjua na hila zake, njia sahihi ni kumpuuza. Tukimfukuza atalitumia jukwaa atatuumiza. Chadema, kwa hili tumieni busara kubwa Shibuda ana nguvu sana kwa wasukuma na huu ndio ukweli
 
MBUNGE wa Maswa Magharibi, John Shibuda, anaweza kupoteza ubunge wakati wowote , Raia Mwema, limeelezwa.

Hiyo inatokana na chama chake, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kumtuhumu kwa kukihujumu na hivyo kupanga kumvua uanachama. Mbunge akikoma kuwa mwanachama wa chama kilichomsimamisha, anakoma kuwa mbunge...

More: Raia Mwema - Vigogo kumvua ubunge Shibuda

Shibuda sawa na fisi mwenye chongo, anatumia zaidi pua kupata ufahamu wa kuona, hivyo asisumbue, 2015 siyo mbali ndo utakuwa mwisho wake, sababu hasa ameishajulikana, hawezi kujificha katk shamba la njugu kwani mgongo unaonekana.
 
Baadhi ya magazeti na kundi moja lililoko ndani ya CHADEMA linakuwa na fikra za kilevi pale wanapofikilia Mh. John Shibuda ni weakest link katika msuguano na mnyukano ndani ya CHADEMA unachagizwa na ubinafsi wa kiwango cha kidikteta.

Hakuna nguvu imara za kisiasa ndani ya kamati kuu ya CHADEMA zitakazo kitikisa kizingiti cha Mh. Shibuda bila kuomba msaada.

Mh. John Shibuda hana cha kupoteza kama ataondoka CHADEMA na kama ikitokea kuwa hivyo, CHADEMA itakuwa matatani.

Huu ndiyo ukweli na wenye macho wanauona.
 
Kwa watu makini hawawezi kupoteza muda kushugulika na mtu kama Shibuda ambaye madhara makubwa anayoweza kuyafanya ni kwenda kinyume na maazimio ya pamoja ya kichama. Kwakua "matatizo yake" yalijulikana tangu alipopewa nafasi ya kugombea kwa tiketi ya chadema hapa wanachohitaji ni uvumilivu wa kisiasa na sio kumfukuza.
 
Mimi naunga mkono hoja, madame tumeshamjua na hila zake, njia sahihi ni kumpuuza. Tukimfukuza atalitumia jukwaa atatuumiza. Chadema, kwa hili tumieni busara kubwa Shibuda ana nguvu sana kwa wasukuma na huu ndio ukweli
Labda wasukuma wa juzi na sio wa leo,Asante Kwa chama pendwa kwa kutuamsha
 
Mimi naunga mkono hoja, madame tumeshamjua na hila zake, njia sahihi ni kumpuuza. Tukimfukuza atalitumia jukwaa atatuumiza. Chadema, kwa hili tumieni busara kubwa Shibuda ana nguvu sana kwa wasukuma na huu ndio ukweli

Ananguvu kwa wasukuma?Unajidanganya kama yeye anavyojidanganya wasukuma sio mabwege wanaakili sana hawawezi kushikiwa akili na mtu kama yeye,miaka yote ya Shibuda na CCM yake madarakani vilio vya wasukuma ni vile vile wasukuma wanajitambua.
 
Mimi naunga mkono hoja, madame tumeshamjua na hila zake, njia sahihi ni kumpuuza. Tukimfukuza atalitumia jukwaa atatuumiza. Chadema, kwa hili tumieni busara kubwa Shibuda ana nguvu sana kwa wasukuma na huu ndio ukweli

Adui yako ukimjua wala hata haina shida , hata mimi sipendi afukuzwe , bali hilo la kwamba sijui ana nguvu sana kwa wasukuma haliwezi kupita bila kupingwa , turudi nyuma kwenye uchaguzi 2010 , bila CDM Shibuda was nothing , Mbona hao Wasukuma hawakumuokoa na kesi ya kusingiziwa ile ya mauaji ? Bali Mabere marando on behalf of CDM ndiye aliyeokoa jahazi , Angalizo , Ni kashfa kubwa sana kulihusisha kabila lolote lile na utukufu wa mtu binafsi .
 
Baadhi ya magazeti na kundi moja lililoko ndani ya CHADEMA linakuwa na fikra za kilevi pale wanapofikilia Mh. John Shibuda ni weakest link katika msuguano na mnyukano ndani ya CHADEMA unachagizwa na ubinafsi wa kiwango cha kidikteta.

Hakuna nguvu imara za kisiasa ndani ya kamati kuu ya CHADEMA zitakazo kitikisa kizingiti cha Mh. Shibuda bila kuomba msaada.

Mh. John Shibuda hana cha kupoteza kama ataondoka CHADEMA na kama ikitokea kuwa hivyo, CHADEMA itakuwa matatani.

Huu ndiyo ukweli na wenye macho wanauona.

Japo hakuna sababu yoyote nzito mpaka sasa iliyothibitishwa kutosha kumfukuza John Shibuda , lakini nakupa angalizo kuwa hizo nguvu unazosema Shibuda anazo , hana ! Na ukiambiwa thibitisha unachokisema hutaweza , kwani Cdm ina Majimbo Mangapi kwenye hiyo kanda ya ziwa ? Usisifie usichokijua , kwa taarifa yako bila Cdm huyo Shibuda wako angefungwa jela 2010 ( kwa hisani ya Robert Kisena ) ! You know the name ? Fisadi wa UDA aliyediriki kumchapa vibao OCD , lakini hadi leo anadunda ! Fuatilia utajua , Ndiyo maana wahenga wanashangaa John Shibuda anakopata ujasiri wa kuponda CDM ! Amesahau au amesahaulishwa ?
 
shibuda hana lolote mchumia tumbo nyama na bia tu utampa kazi yeyote.tumuache watu wa type hiyo ni wengi bongo.ana bwana zenz
 
Mtu mwenye hekima hujifunza kwa makosa ya mwenzake,mjinga hujifunza kwa makosa yake mwenyewe lakini mpumbavu halifunzi lolote,Shibuda ameshindwa hata kujifunza kwa makosa yake mwenyewe,kasahau kwanini CCM ilimtosa leo tumuitaje?Mjinga anaweza vumilika,mpumbavu havumiliki.Sio kila mbwa anayebweka ni mkali wengine ni koko ukiokota jiwe anafyata mkia na kukimbia.
 
kwanza ni aibu chama kuwa na member wa design hii, arudi tu kwa wenzakw CCM, siku wakimtimua nitachinja kuku nile na ugali, anatia aibu kwenye chama makini
 
Shibuda hana nguvu yoyote kwa wasukuma na hata jimboni mwake wameshamuelewa ni kichwa maji
 
Back
Top Bottom