Vigogo katika kashfa TANROADS

Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
199
KATIKA GAZETI LA RAIA MWEMA Toleo No. 132 LA TAREHE 5 MEI 2010, IPO HABARI KUWA MTENDAJI MKUU WA TANROAD NDG EPHRAIM MREMA ANAWADHARAU VIONGOZI WA WIZARA YA MUINDO MBINU.

MIEZI YA NYIUMA KIDOGO ILIWAHI KURIPOTIWA NA GAZETI HILI HILI KUWA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MIUNDO MBINU nDG OMARA CHAMBO NA WASAIDIZI WAKE HAPO WIZARANI WALILIPWA NA TANROAD MALIPO YENYE UTATA KWA KURUHUSU WAFANYAKAZI WA TANRIAD WALIPWE MISHAHARA MIPYA.

SI NI MOJA YA KAZI ZA KAWAIDA ZA KATIBU MKUU KUPITISHA MISHAHARA MIPYA KWA WAFANYAKAZI WA TAASISI ZILIZOKO CHINI YA WIZARA YAKE. SASA KATIBU MKUU NA WASAIDIZI WAKE WIZARANI NI KWANINI WALILIPWA TENA MALIPO YANAYOFIKIA MILIONO 40, KWA MTU MMOJA KWA KUTIMIZA WAJIBU WAO.

KAMA SIO RUSHWA ILI KUWAONGEZEA MISHAHARA WAFANYAKAZI WA TANROAD, KATIBU MKUU NDG OMARA CHAMABO NA WASAIDIZI WAKE WALIKUBALI VIPI KUPOKEA MALIPO MAKUBWA KIASI HICHO KUTOKA KATIKA TAASISI WANAYOIONGOZA?

kWANI WAFANYAKAZI WA TANROAD SIO WAFANYAKZI WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ALIOKUWA AKIWAZUNGIZMZIA JUZI MTUKUFU RAIS HADI AWE NA MFUMO TOFAUATIA WA MISHAHARA NA KUTOA ASANTE KUBWA KIASI KWA KUPANDISHIWA MISHAHARA?

JE NDIO MATUMIZI MAZURI YA KODI TUNAZOKATWA WANANCHI KATIKA KILA LITA YA MAFUTA YA PETROLI?

BAADA YA MTENDAJI MKUU WA TANROAD NDG EPHRAIM MREMA KUJUA BEI YA VIONGOZI WA WIZARA YA MIUNDO MBINU, SASA HAWAMUWEZI. ANAWADHARAU, HATA WAKIMWANDIKIA BARUA HAJIBU N.K. NDG OMARA CHAMABO NA WASAIDIZI WAKO MLIOCHUKUA MALIPO KUTOKA TANROAD KWA KUTIMIZA WAJIBU WENU WA KUPITISHA MISHAHARA MIPYA YA TANROAD, RUDISHENI FEDHA HIZO ZINAZOFIKIA MILIONO 40 KILA MMOJA WENU, FEDHA ZA WANANCHI NDIPO MTAPATA UDHU WA KUWEZA KUMSHUGHULIKIA NDG MREMA.

LA SIVYO ATAWEZA KUWAKAANGA KWA MAFUTA YENU WENYEWE KUTOKANA NA ULAFI!!! SOMA HABARI KAMILI HAPO CHINI

Vigogo katika kashfa TANROADS


Mwandishi Wetu
Mei 5, 2010

VIGOGO serikalini na katika Chama cha Mapinduzi (CCM), wa sasa na wa zamani, ndio wanaomkingia kifua Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Ephraim Mrema, kiasi cha kumfanya adharau mamlaka nyingine zilizo juu yake, Raia Mwema limeelezwa.

Uchunguzi wa Raia Mwema, umethibitisha kuwapo nguvu kubwa katika kumkingia kifua Mrema, kiasi sasa amekuwa akidharau mamlaka nyingine za utendaji akidai yuko katika mchakato wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Raia Mwema
lina taarifa ya kuwa Wizara ya Miundombinu imekwisha kumuandikia barua mara kadhaa ikimtaka atoe maelezo kutokana na utendaji wake usioridhisha lakini barua hizo hazijibiwi.

“Unajua Mrema anatumia majina ya viongozi wa Serikali na CCM katika kujiwekea kinga na hilo linamfanya awe na jeuri ya ajabu kabisa. Hata baadhi ya vyombo vya habari haviandiki mambo yake, nawashangaa sana (Raia Mwema) mnapata wapi ujasiri. Huyu mtu na nguvu sana,” alisema Ofisa Mwandamizi wa Wizara ya Miundombinu.

Katika barua yake ya hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Omar Chambo, alimtaka Mrema kueleza sababu za kudharau mamlaka za juu na kukiuka mkataba wa ajira yake na maelekezo ya Serikali.

Katika barua hiyo ambayo nakala yake imepelekwa Ikulu, Chambo alimzuia Mrema pia kufanya mabadiliko katika nafasi mbalimbali za uongozi bila kufuata taratibu kama ambavyo amekuwa akifanya mara kwa mara na alifanya hivyo siku moja tu baada ya kuandikiwa barua ya kuzuiwa kufanya mabadiliko na uteuzi wowote.

"Kutekeleza mabadiliko hayo kinyume cha maelekezo yangu kunaashiria dharau,” inaeleza sehemu ya barua hiyo ya Chambo iliyonukuliwa pia kwa Waziri Mkuu, Utumishi na Ikulu.

Katika maelezo yake, Mrema amekuwa akidai kwamba mabadiliko yote aliyoyafanya TANROADS aliyafanya kwa mamlaka aliyopewa na Rais Jakaya Kikwete, ikiwa ni pamoja na kuteua Wakurugenzi na Mameneja wa Mikoa wa TANROADS.

"Mrema anadai pia kwamba aliitwa na Rais na na kupewa kibali cha kufanya mabadiliko hayo ndani ya TANROADS lakini ukweli umekuja kubainika kwamba amekuwa akimsingizia Rais mambo mengi ambayo si vyema kuyazungumza hapa hata kama ingekuwa kweli,” anasema ofisa mwingine mwandamizi wa Serikali aliye karibu na Wizara ya Miundombinu.

Katika moja ya maamuzi aliyoyachukua Mrema ni pamoja na uteuzi wa Isaack Kamwela, kutoka Wizara ya Miuondombinu kuwa ofisa mwandamizi wa TANROADS wakati ofisa huyo alikuwa mmoja wa wajumbe katika kamati iliyoshiriki kuhalalisha uteuzi wake kuwa Mtendaji Mkuu wa wakala.

Mwaka 2008, Mrema aliingia katika mgogoro na Mamlaka ya Manunuzi (PPRA) kuhusiana na ukiukwaji wa taratibu za zabuni baada ya kudharau ushauri na mapendekezo ya wataalamu wa mamlaka hiyo kuhusiana na mradi wa upanuzi wa barabara ya Bagamoyo-Makurunge-Saadani-Pangani-Tanga.

Tayari Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kupitia ofisi ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo, ametaka kupewa maelezo ya kina kuhusu uongozi wa TANROADS kupoteza mwelekeo na kushuka kwa kiwango cha ufanisi, ikiwa ni siku kadhaa baada ya gazeti hili kufichua pamoja na mambo mengine, hasara iliyosababishwa kutokana na kuyumba kwa wakala huo.

Raia Mwema
limethibitisha kuwapo kwa uchunguzi rasmi wa vyombo vya dola kuhusiana na nyendo za uongozi wa TANROADS ikiwa ni pamoja na uteuzi tata wa Mrema kuwa Mtendaji Mkuu.

Habari za ndani ya Serikali zimeeleza kwamba baada ya juhudi kubwa za kumuokoa, hali sasa imebadilika na vyombo vya dola vimeanza kumchunguza Mrema ambaye anadaiwa uteuzi wake ulikuwa na utata.

Vyombo vya dola vinaelezwa kuchunguza pia utata katika mkataba wa ajira ya Mrema baada ya kubainika kutofautiana hata na barua ya uteuzi uliofanywa na aliyekuwa Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge, ikiwamo kipengele muhimu kinachozungumzia kipindi cha mkataba na suala la kodi mbalimbali za Serikali ambavyo vimebadilishwa katika mazingira ya utata.

Habari za ndani ya Serikali zinaeleza kwamba uchunguzi huo unaoanzia mbali mwaka 2007 ambako Serikali, kupitia Wizara ya Miundombinu, iliajiri mshauri mwelekezi, kampuni ya Price WaterhouseCoopers kufanya mchakato wa kumtafuta Mtendaji Mkuu wa TANROADS, kabla ya Chenge kuamua kushinikiza kutupiliwa mbali kwa mapendekezo ya mshauri huyo na kuunda timu mpya ya uteuzi ambayo ilipokea maelekezo kutoka wizarani.

Katika barua ya ajira ya Mrema iliyosainiwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Enos Bukuku, inatajwa kwamba Mtendaji Mkuu huyo ameteuliwa na Chenge kwa kipindi cha miaka mitatu na kwamba “mapato yote yatalipiwa kodi kwa mujibu wa sheria”, lakini mkataba wa ajira uliosainiwa Juni 2007, unaonyesha kwamba ni mkataba wa miaka mitano na kwamba hatolipa kodi kutoka katika mshahara wake wa Sh 10, 900,000 na marupurupu mengine.
 
Back
Top Bottom