Vigogo halmashauri Sengerema wasimamishwa kazi kupisha uchunguzi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela amewasimamisha kazi wakuu wa idara watatu wa halmashauri ya Sengerema kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo.

Waliosimamishwa kazi ni Tabwe Seleman ambaye ni kaimu mweka hazina wa halmashauri hiyo, Renatus Shule (kaimu ofisa manunuzi) na William Wandu (kaimu mhandisi wa halmashauri).

Watatu hao wamesimamishwa kazi kuanzia jana Jumanne Aprili 20, 2021 saa kadhaa tangu Waziri wa Tamisemi kumsimamisha kazi mkurugenzi wa halmashauri ya Sengerema, Magesa Mafuru kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo wilayani humo.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole ameithibitisha Mwananchi Digital kuwa wakuu hao wa idara wamesimamishwa kazi na Mongela kuanzia jana.

1618998043731.png
 
Nchi ya ajabu sana. Kila anayesimamishwa tuhuma ni ubadhirifu wa fedha, sijasikia hv karibuni mtu kasimamishwa kwa tuhumu za utovu wa nidhamu. Upigaji ndio kila kitu kwa viongozi
 
Back
Top Bottom