Vigogo CHADEMA ndani ya kashfa nzito

Status
Not open for further replies.

Shebbydo

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
1,174
1,937
VIGOGO wa juu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wameingizwa ndani ya kashfa ya kutumia madaraka na ofisi za chama hicho vibaya. RAI lina taarifa kamili.

Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu na mmoja wa wakurugenzi wa chama hicho anayeshughulikia masuala ya Bunge (jina tunalihifadhi), wanadaiwa kuomba rushwa kwa baadhi ya makada wa chama hicho ili wawasaidie kupata nafasi ya ubunge wa jimbo na ile ya viti maalumu wakati na hata baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Tayari tuhuma hizo zimeshawasilishwa kwenye Kamati Kuu ya chama hicho na inayotarajiwa kukutana wakati wowote kuanzia sasa.

Mwalimu anatajwa kufanya hivyo katika kipindi alichokuwa akikaimu nafasi ya Ukatibu Mkuu, ambapo anadaiwa kuwaomba rushwa baadhi ya makada wao waliokuwa wakitaka ridhaa ya chama ya kuwania ubunge.

Wakati Mwalimu akipewa tuhuma hizo, mwenzake anadaiwa kuwaomba rushwa baadhi ya makada wa kike wa chama hicho ili awasaidie kupata nafasi ya ubunge wa viti maalumu.

Taarifa kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu waliokutana Machi mwaka huu, jiji Dar es Salaam kabla ya kwenda jijini Mwanza kwenye kikao cha Baraza Kuu, zililiambia RAI kwamba Mwalimu anadaiwa kufanya hivyo kwa nia ya kujinufaisha.

Tuhuma hizo zilifikishwa mbele ya Kamati Kuu ya Chadema na Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.

Ilidaiwa kuwa Mwalimu aliomba kiasi cha Sh. Milioni 10 kwa Mbunge wa jimbo la Ndanda, Cesil Mwambe.

RAI lilimtafuta Mwambe kuzungumzia suala hili, hata hivyo hakukubali wala kukataa, lakini zipo taarifa zisizo na shaka zinazothibitisha mbunge huyo kuwasilisha madai yake kwa maandishi ikiwa ni sehemu ya kiambatanisho kwenye madai ya Mbilinyi.

Kiambatanisho hicho cha ushahidi kinaonyesha namna ambavyo Mwalimu, alitoa maelekezo ya kuwazuia viongozi wa Chadema kumnyima ushirikiano Mwambe, kutokana na kukaidi ombi lake.

Mbilinyi alipoulizwa na gazeti hili kuhusu malalamiko aliyopeleka kwenye Kamati Kuu, alikiri kufanya hivyo na kusema kuwa kazi hiyo ameiachia kamati hiyo kuwachukulia hatua zinazostahili viongozi hao kwa mujibu wa taratibu na katiba ya chama hicho.

“Taarifa nimeshafikisha hivyo kama hadi sasa umeona kimya ujue kabisa siku viongozi wakiamua kutoa uamuzi wa jambo hilo naamini hata ninyi (waandishi) mtajua,” alisema Mbilinyi.

Kwa upande wake Mwalimu alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa sababu kama litakuwa mikononi mwa Kamati Kuu ni wazi hana mamlaka ya kulitolea ufafanuzi.

“Siwezi kutolea ufafanuzi taarifa ambazo mnasema zimeshafika kwenye Kamati Kuu, kwa sababu Mwenyekiti ndiye mwenye mamlaka wa kuzungumzia jambo hilo. Hata hivyo siamini kama kweli nimemuomba Mwambe hizo fedha,” alisema Mbilinyi.

RAI liliwasiliana na Mkurugenzi aliyehusihwa katika tuhuma hizo bila mafanikio, mara zote alizokuwa akipigiwa simu alikuwa akiikata na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi, hakujibu.

Alipotafutwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ili kuzungumzia madai hayo, nae hakuweza kupatikana si ofisini kwake wala kwenye simu.

Chanzo: Rai
 
kama ni kweli wanahusika na hizo shutuma wachukuliwe hatua ila kama ipo hii habari kwa njia nyingine mnayoitaka mtakuwa hamjatenda haki hatupend watenda maovu taifa mbele maslahi binafsi mwiko.
 
hahaha hii nchi inatakiwa uwe na wazimu kidogo uweze kuwa sambamba na mambo yanayoendelea
 
Elimu elimu elimu mweshimiwa alikuwa anamaanisha wewe mtoa mada unaacha kuangali mambo yaliyoshika kazi ufisisadi uliokithiri mno unazungumzia habari za chama za kina mwalimu eti milioni 10 na wakati kuna mambo mazito hii nchi ambayo magu mwenyewe analewa nayo fikiria kwanza kabla kulera uzi .
 
Hivi huyu Mwalimu na mwenzake siyo CCM hawa?????[sic]
 
Elimu elimu elimu mweshimiwa alikuwa anamaanisha wewe mtoa mada unaacha kuangali mambo yaliyoshika kazi ufisisadi uliokithiri mno unazungumzia habari za chama za kina mwalimu eti milioni 10 na wakati kuna mambo mazito hii nchi ambayo magu mwenyewe analewa nayo fikiria kwanza kabla kulera uzi .
Sijaelewa unamaanisha nini. Kama upande mwingine usiposemwa juu ya rushwa haitakuwa mapambano dhidi ya rushwa bali mapambano ya chuki. Wala rushwa wote lazima wawekwe wazi haijalishi ni rushwa kubwa ama ndogo, iwe CCM ama CHADEMA. Tunataka mawazo ya rushwa yaondoke katika akili ya Watanzania wote bila kujali itikadi za vyama.
 
Hatutatoka kwenye track kwa maneno ya magazeti yanayofahamika mrengo wake.
Sisi bado tuna taka majibu ya Lugumi Enterprise na NSSF maana hayo yana direct impact kwa wananchi walio wengi wa kawaida.
Huu mtindo wa kijinga ambao unatumika pale kunapojitokeza swala zito la uhujumu nchini wa kuchomekea viissue vidogovidogo ili kupotezea mambo mazito sasa hautakubalika. Ni kutuona wajinga.
Unamaanisha hii habari ni ya kutunga kama hadithi? Kama ni ya kutunga basi tutasikia majibu ya waliotungiwa.
Mimi nadhani tusiwe na upande juu ya mapambano dhidi ya rushwa. Iwe kubwa ama ndogo, iwe CCM ama chama chochote. Kama rushwa itaruhusiwa ndani ya chama matokeo yake ni viongozi wabovu.
 
Hayo ya chama yabaki kwenye chama, tunahitaji mambo ya kitaifa kwanza, LUGUMI na hela zetu wachumia juani, kwa nini iwe ngumu kwake kushughulikiwa? Katoroka au kasafiri atarudi? Hii ndio habari ya mjini kwa sasa.
Rushwa mahali popote inastahili kukemewa kwa kuwa vyama ndivyo vinavyotoa viongozi wa kisiasa.
 
NSSF na Lugumi is no excuse kwa madudu yanayoendelea mtaa wa Ufipa. Kila jambo lazima lisemwe. Uchafu ni uchafu!

Tusitumia kashfa za mikataba ya Lugumi na NSSF kuficha maovu yanayoendelea huko Ufipa.

Nilidhani watetezi wangejikita kueleza ni kwa namna gani taarifa hii haina ukweli badala kujificha kwenye kashfa zingine. Jiepushenina double standard. Ni tabia hii iliyowaponza kiasi cha 'kubadili gia angani' na kupoteza mwelekeo.

Aibu!
 
Hatutatoka kwenye track kwa maneno ya magazeti yanayofahamika mrengo wake.
Sisi bado tuna taka majibu ya Lugumi Enterprise na NSSF maana hayo yana direct impact kwa wananchi walio wengi wa kawaida.
Huu mtindo wa kijinga ambao unatumika pale kunapojitokeza swala zito la uhujumu nchini wa kuchomekea viissue vidogovidogo ili kupotezea mambo mazito sasa hautakubalika. Ni kutuona wajinga.

Mzee hilo ni Rai mzee, gazeti la mgombea wa urais kwa tiketi ya UKAWA
 
Hiyo ya chama haijaongelewa na serikali. Ni habari ambayo imeandikwa na gazeti hivyo basi ni vyema kujuzana yanayoendelea kote ili Wananchi tuelewe ni aina gani ya Viongozi tulionao. Isije kuwa ya Kangi Lugola kupiga kelele ili wajitengenezee ulaji.
 
Lugumi na wahusika wa kampuni ya Infosy wakamatwe hata kama waziri anahusika.Na kama Lugumi ametoroka na kukimbilia nje ya nchi wizara ya Mambo ya ndani ina la kujibu .Maana nao ni sehemu ya watuhumiwa.

Haya maswala ya kutumia media ku-divert attention yatawashika mbumbumbu wachache tu.Werevu watang'amua

Turudi kwenye ajenda ya ufisadi uliohusisha Mambo ya ndani.Sio kututoa kwenye reli kama vile sisi sote ni manyumbu
UOTE]
Yakija maswala ya Lichama lenu mnakimbia kivuli chenu mnaanza kuongea mambo ya ku divert attention, Lugumi liongelewe na mauozo ozo yenu pia, msichagulie watu nini cha kuzungumza hamna mamlaka hayo.
 
Labda si wanatuona maboya wanaacha kuandika mafisadi wanaoliangamiza taifa wanaongea mambo yasiyo Na mana

Kuomba rushwa ili kumpa mtu bunge nalo si jambo zuri, nao huo ni ufisadi unaojenga misingi zaidi ya ufisadi. Hili na la Lugumi yote yanaweza kujadiliwa pamoja hakuna ubaya wowote kama uwezo wa vichwa tunao
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom