Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 123,559
- 234,136
Taarifa kutoka vyanzo vya Uhakika ndani ya Chadema vinaeleza kwamba, Tayari tarehe ya kujadili rufaa ya Mgombea Uenyekiti wa Kanda ya Nyasa aliyeshindwa, Peter Msigwa imepangwa.
Inaelezwa kwamba hata kama Bwana Msigwa kaunga mkono Juhudi, bado rufaa yake hiyo itajadiliwa, Hii ni kwa sababu wote aliowatuhumu bado wako Chadema na wanapaswa kujitetea mbele ya Kamati Kuu na kwamba wakibainika kumhujumu Msigwa watachukuliwa hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine wataojaribu kuhujumu chaguzi zijazo.
Kwa mujibu wa Taarifa hiyo watakaohojiwa na Kamati Kuu yumo Freeman Mbowe, Joseph Mbilinyi, John Mrema, Benson Kigaila, William Mungai , Peter Msigwa pamoja na wajumbe wawili wanaodaiwa kuzuiliwa kupiga kura, Imeelekezwa kwamba iwapo Msigwa atakatazwa na chama chake kipya kuja kwenye rufaa yake, basi video zake wakati akiongea na waandishi wa channel ten na TBC aliowaita nyumbani kwake zitatumika.
Habari nyingine inaeleza kwamba Tayari Chadema inao ushahidi wa miamala iliyonaswa, ambayo inatajwa kutoka kwa mtu anayeitwa "Mama Abdul" kama iliyoelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu, Majina ya Wahusika hao wote yatawekwa hadharani na wahusika wote watachukuliwa hatua.
Hutakiwi kukosa Taarifa hii muhimu ya kusafisha Chama