Vigogo Chadema kizimbani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo Chadema kizimbani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngongo, Aug 26, 2011.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 99%, align: left"]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody"]KATIBU wa Jumuiya ya Vijana ya Chadema (BAVITA), Anold Kamunde na aliyekuwa Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema, Gervas Mgonja wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa kutumia silaha na kupora vitu na fedha vyote vikiwa na thamani ya Sh milioni 3.5.

  Mbali na hilo pia askari Polisi, Salumu Idefonce (23) wa Kituo kikuu cha Polisi Mkoa wa Arusha amefikishwa mahakamani kwa madai ya mauaji ya mlinzi wa kampuni ya kuuza na kununua madini ya Classic Gems, Joseph Kisuda.

  Wakisomewa mashitaka na Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Agustino Kombe, ilidaiwa mahakamani hapo, kuwa Mgonja na Kamunde, walifanya hayo wakitumia bunduki aina ya SMG na bastola katika tukio lililotokea Ngarenaro jijini hapa Juni 8.

  Kombe alidai hivyo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Arusha, Rose Ngoka, kuwa
  watuhumiwa hao walitenda kosa hilo kwa kumpora Elizabeth Mkuka, fedha taslimu Sh milioni 1.8 na simu mbili.

  Aliendelea kudai kuwa Mgonja na Kamunde walitenda kosa hilo saa 3 usiku kwa kiasi hicho cha fedha na simu mbili za Sumsung na BlackBerry zote zikiwa na thamani ya Sh milioni 1.6.

  Viongozi hao walikana mashitaka yao na kesi yao itatajwa Septemba 8 na walirudishwa rumande kwani upelelezi haujakamilika na walinyimwa dhamana kutokana na uzito wa kesi yenyewe kisheria.

  Katika kesi ya Idefonce, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Sabina Slayo, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Arusha, Devotha Msofe, alidai kuwa mtuhumiwa anashitakiwa kwa mauaji pamoja na wenzake wawili katika tukio la Mei 21 katika kampuni hiyo ya madini.

  Wenzake ambao wako rumande ni Abdul Philipo ‘Baba Salimu’ na Prosper Saimoni ‘Otieno’.

  Mshitakiwa hakutakiwa kujibu lolote kwani Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji ila Mahakama ya juu yake.

  Kesi hiyo itatajwa mahakamani hapo Septemba 6 na alirudishwa rumande hadi siku hiyo.

  Habari za nje ya Mahakama zilidai kuwa viongozi wa Chadema wataunganishwa na washitakiwa wengine waliokuwa walisomewa mashitaka juzi katika Mahakama hiyo kwa mashitaka hayo hayo.


  Source: Habari leo

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Text"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Baba Collin

  Baba Collin JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hao si viongozi wa cdm,full stop!
   
 3. l

  lebadudumizi Senior Member

  #3
  Aug 26, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha unazi wa kipuuzi Anold Kamunde ni katibu wa BAVITA mkoa wa Arusha Gervas Mgonja alikuwa katibu wa mbunge Arusha G Lema.

   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ngongooooooooooooooooooo!!!!!!!!!!!!!!!!! hahah ahaha ahaha ahah!
   
 5. l

  lebadudumizi Senior Member

  #5
  Aug 26, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ngongo aliwatuma !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.

   
 6. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kumbe kuna wanazi wengi sana humu JAMIIFORUM EEHH
   
 7. l

  lebadudumizi Senior Member

  #7
  Aug 26, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Gervas Mgonja alikuwa katibu wa Godbless Lema hadi June mwaka huu issues za ujambazi zipoanza kuibuka Lema akamtosa kiujanja barua ya kumtosa akaipeleka RPC na OCD.
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,861
  Trophy Points: 280
  ccm wanatafuta pa kutokea kila sku
   
 9. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  si viongozi wa chadema hao

  kafanye utafiti kwanza ndo uje upost tena
   
 10. l

  lebadudumizi Senior Member

  #10
  Aug 26, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku hizi ni rahisi kutetea dhambi kwa mgongo wa CCM ?.

  Kama si viongozi wa CDM tuambie ni viongozi wa chama gani na walikuwa karibu na kiongozi gani CDM.
   
 11. l

  lebadudumizi Senior Member

  #11
  Aug 26, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Magwanda wameshikwa pabaya hawana pa kukimbilia.Ngoja niwaandalie juisi ya pilipili.
   
 12. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Chadema wezi,
  Chadema vigeugeu,
  Chadema adui wa waislamu
  Chadema adui wa wakristo(Jana Regia Mtema(mb CDM) kasema Yesu alikuwa na mapungufu kibao)
   
 13. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ngongo,
  Wakiitwa Vigogo wa Chadema, hao wenye kesi nao watatoka?
   
 14. ntagunga

  ntagunga JF-Expert Member

  #14
  Aug 26, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  ni kiongozi mmoja na aliyekuwa katibu. kwa sasa ni nani?

  kiongozi wa BAVICHA hastahili kuitwa kigogo wa CDM, wala aliyewahi kuwa katibu wa mbunge. sema tu kiongozi wa BAVICHA inatosha.
   
 15. l

  lebadudumizi Senior Member

  #15
  Aug 26, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vigogo wana alama gani ?.

   
 16. l

  lebadudumizi Senior Member

  #16
  Aug 26, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mshauri ulinzi na usalama wa mbunge wa Arusha mjini.

   
 17. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #17
  Aug 26, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Lebadudumizi=Ngongo!...doubtless!
   
 18. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #18
  Aug 26, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  vigeugeu kama kikwete!?
  mmh kwa hiyo ni chama kisichokuwa na dini si uislam wala ukristo hahahah!
  MAGAMBA BANA!
   
 19. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #19
  Aug 26, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kikwete ni Great Thinker, anafanya kila kitu kwa reason!
  Hakurupuki!
   
 20. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #20
  Aug 26, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,015
  Likes Received: 2,663
  Trophy Points: 280
  Hawa wanatafuta jinsi ya kupoteza inshu muhimu masikioni kwa WATZ,tunataka kusikia hatima za hawa,JAIRO+MEGAWATI+LUHANJO NK sio kutuletea habari za kipuuzi hapa.
   
Loading...