Vigogo CCM watafuna mamilioni ya mradi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo CCM watafuna mamilioni ya mradi

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by EMT, Apr 2, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Dodoma , kimeingia kwenye malumbano kuhusu mamilioni ya fedha za mradi wa hosteli ya CCM zinazodaiwa kutafunwa na baadhi ya vigogo wa chama hicho mkoani hapa. Akizungumza jana mjini Dodoma, Katibu Mwenezi wa CCM wa Mkoa, Donald Mejiti alisema, Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Dodoma, imeunda Tume ya watu watatu kuchunguza na kutoa taarifa ya upotevu wa fedha za mradi wa ujenzi wa hosteli kiasi cha Sh milioni 373 zinazodaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

  Fedha hizo ni sehemu ya fedha za ujenzi wa mradi huo unaomilikiwa na CCM mkoani Dodoma uliowekwa jiwe la msingi hivi karibuni na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete. Mejiti alisema mradi huo ulipangwa awali kugharimu Sh milioni 298, gharama zinazoonekana kuongezeka kwa kiasi cha Sh milioni 75 ambazo hazina maelezo zimeongezeka kutoka wapi na kutumika kwa kazi gani huku Katibu wa CCM wa Mkoa, Kapteni John Barongo, akituhumiwa kuhusika na matumizi ya fedha za mradi huo bila kushirikisha Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma.

  Kwa mujibu wa Mejiti, taarifa ya tume hiyo ambayo wajumbe wake ni Wales Lusingu, Hydar Gulamali na Anthony Mavunde, inatarajiwa kuwasilishwa ndani ya wiki mbili kwenye kikao cha Halmashauri ya CCM mkoani hapa, kitakachofuatiwa na kikao cha Kamati Kuu ya CCM, itakayojadili hali ya hewa ya kisiasa na taarifa za mikoa yote nchini zinazohusu tathmini ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

  Kwa upande wake, Kapteni Barongo, alisema ameshangazwa na taarifa hiyo na kudai inakatisha tamaa kutokana na ubunifu wake wa mradi uliokwama kutekelezwa tangu mwaka 1984 ulipoanzishwa, na baada ya kuingilia kati, ili kuufufua kwa lengo la kukuza uchumi na kipato cha chama kupitia mradi huo.

  Alitoa ufafanuzi kuwa jumla ya Sh 322,204,710 zilipangwa kutumika katika ujenzi wa hosteli hiyo iliyopo eneo la Airport karibu na Dodoma Inn na kwamba hadi sasa mkandarasi ambaye ni kampuni ya Ebenezer Destefano, amelipwa kiasi cha Sh 155,786,147 ikiwa ni malipo ya ujenzi yaliyofanyika baada ya kukamilisha ujenzi huo kabla ya kufanya marekebisho mapya ya vifaa vya kupaulia.

  Alisema uamuzi wa kufanya marekebisho ya vifaa vya kupaulia ulifanywa na kupitishwa na kamati ya siasa ya mkoa, ambapo kiasi cha Sh 47,602,565.26 zinadaiwa na mkandarasi huyo ili kukamilisha kazi hiyo. Alifafanua kuwa kutokana na malalamiko yaliyoibuliwa kwenye kikao cha kamati ya siasa Machi 26 na kulazimika kuunda tume yenye jukumu la kuchunguza maendeleo ya mradi huo na kuandaa ripoti itakayowasilishwa kwenye kikao kijacho.

  Barongo alisema ni kweli yapo madai kutoka kwa mkandarasi, kwa sababu chama hakina fedha na tayari kimefanya mazungumzo na Benki ya NMB ili kupata mkopo utakaotumika kulipa deni hilo. Alisema deni hilo limecheleweshwa, kutokana na masharti yaliyotolewa na benki hiyo ya kutaka hati ya kiwanja na mpango wa mradi, ambavyo vimeshashughulikiwa kutokana na nyaraka zilizopelekwa NSSF na viongozi wa CCM waliopita, na walioomba taasisi hiyo kuipa CCM mkopo. Kwa hiyo hati hiyo itawasilishwa benki, ili kupata mkopo utakaotumika kukamilisha ujenzi wa jengo hilo la mradi wa hosteli ya CCM.

  Aidha, Barongo alifafanua kuwa fedha za ujenzi wa hosteli hiyo zilitokana na malipo ya pango la benki ya NMB kwenye jengo la CCM, baada ya makubaliano ya kulipwa Sh 182,574,000 kwa miezi 42, fedha ambazo ziliwezesha mradi kuanza kutekelezwa Februari 8 mwaka jana, hadi jengo lilipofikia ambapo mkandarasi bado anadai jumla ya Sh 166,418,563. Mradi huo uliwekewa jiwe la msingi Novemba 25 mwaka jana na Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete ambaye alipongeza ubunifu wa vyanzo vya mapato ya chama na kutaka mikoa mingine kuiga hatua hiyo.

  HabariLeo
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Apr 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280

  sijaelewa na wala sitaki kuelewa.
   
 3. Landala

  Landala JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 940
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Ufisadi ni sera ya CCM,ndio maana kila mwanachama na kiongozi yoyote wa Chukua Chako Mapema ukitokea mradi mbele yake lazima achakachue.Hiyo ndo CCM.
   
 4. M

  Mr zam Member

  #4
  Apr 2, 2011
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe hujui kama CCM na UFISADI ni baba mmoja.
   
 5. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Katibu huyo hivi karibuni alikuwa anachunguzwa na TAKUKURU kwa kukodisha gari ya CCM kwaajili ya kusambaza mitihani na kujichukulia fedha za mwajiri wake zilizotokana na ukodishaji huo wa gari ya chama; uchunguzi huo uliishia wapi, au ndiyo tayari umetupwa kapuni! Si unajua CCM kulindana ndiyo jadi yao, na Barongo anasemekana kuwa chanda na pete na viongozi wote wakuu wa CCM kitaifa
   
 6. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180

  Hata ingekuwa kwa NCCR, Tadea, CDM?
   
 7. C

  CHESEA INGINE Senior Member

  #7
  Apr 2, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hivi kwa nini waunde tume wasiripoti polisi?
   
 8. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Hapo sasa, lakini polisi ipi - hii ya Mwema?
   
Loading...