Byendangwero
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 871
- 56
Wana JF nisaidie kwa hili; Inasemekana idadi ya viti maalum hutolewa na NEC kwa chama cha siasi, kulingana na uwiano wa jumla ya kura za urais na wabunge walizopigiwa wagombea wa chama husika; kama hivyo ndivyo, kura za wabunge wanaochaguliwa bila kupingwa zinapatikanaje ili kuweza kukamilisha zoezi hilo.Jambo la pili, kwa mujibu wa ibara ya 66 ya katiba bunge la Tanzania linaundwa na wabunge wa aina nne; waliochaguliwa kuwakilisha majimbo, wa viti maalum, waliochaguliwa na Baraza la wawakilishi na Mwanasheria mkuu wa serikali. sasa hao wabunge wa kupita bila kupingwa wanao wakilisha majimbo bila ya ridhaa ya majimbo husika, wanatokana na kifungu kipi cha katiba? Isingelikuwa vyema angalau wakapigiwa za ndiyo? naomba mchango wenu.