Vigezo kujiunga na JKT

Vigezo kujiunga na JKT

tommyzo

Member
Joined
Aug 14, 2012
Posts
65
Reaction score
9
Jamani hili ni ombi kwenu Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), NI KUHUSU SWALA LA KUJIUNGA NA JKT, SWALA LA KIGEZO CHA UMRI PALE NI TATIZO, MIAKA 18-23, WATANZANIA WANAOMALIZA DIGRII YA KWANZA UKIFATA UTARATIBU WA KUANZA SHULE UKIWA NA MIAKA 7 WENGI WANAMALIZA WAKIWA NA UMRI WA MIAKA 24(UKIHESABU NA MUDA WA KUSUBIRIA KWENDA LEVEL NYINGINE), JE WASOMI HAWAITAJIKI JESHINI? WENGINE WANGEPENDA KWENDA JWTZ ILA LAZIMA UPITIE JKT LAKINI UMRI NI TATIZO, KAMA NI SWALA LA CHEO NA KUKOSA UZALENDO BASI IFANYIKE KAMA POLISI WANAVYOFANYA UNAKAA BILA CHEO LAKINI UNALIPWA MSHAHARA KULINGANA NA ELIMU YAKO, UPATIKANAJI WA CHEO UWE KWA PENDEKEZO. JAMANI HUU NI USHAURI TU NA MAONI YANGU KAMA MTANZANIA.

Masharti ya kijana wa kujitolea kwa ajili ya kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa
1.Awe raia wa Tanzania
2.Awe na Umri kati ya miaka 18-23
3.Awe amemaliza darasa la saba na kuendelea
4.Asiwe ameoa au kuolewa na asiwe na mtu yeyote anayemtegemea
5.Awe tayari kufuata sheria zote za kijeshi zitazokuwa juu yake wakati akiwa jeshini(kutoroka,wizi,ulevi,uvutaji bangi, madawa ya kulevya na upatikanaji wa mimba n.k) Jeshini ni makosa makubwa na utaweza kushtakiwa na kufutiwa mkataba na JKT
6.Awe tayari kurudi nyumbani baada ya kumaliza mkataba wake na Jeshi la Kujenga Taifa
7.Awe na tabia na mwenendo mzuri.
 
Yaani mi nashangaa sana hii nchi ina maaana wenye huo umri wengi wao ni waliomaliza form 4 na form 6 au certificate na diploma kwa hyo haohao ndo wanaenda kuajiriwa na TIS, UHAMIAJI, MAGEREZA, JWTZ, PCCB na POLICCM. Kwa kigezo cha umri wanatubagua sis tuliomaliza vyuo vikuu na kuchukua hao wenye ufaulu mdogo na elimu ndogo na wakishafanya kaz kwa muda mfupi wanaomba kwenda kusoma na serikali inaingia gharama tena kwenda kuwasomesha na kuacha magap na kusababisha utendaji mdogo. Hiv kweli hawa watu wanaopanga kweli wanatumia vichwa kufikiria au wanafikir kwa kutumia matumbo na miguu yao. Yaani mpaka sasa hiv natamani litokee kundi la waasi mi nikajiunge nimeshachoka na hii hali ngumu ya maisha.
 
Kama ni tatizo linaongelewa kwa utaratibu, sasa ukishajiunga na hao waasi? Au ndio kuanza kukimbizana wakati nchi ni yetu, tunatoa hoja kisomi hata kama tumechoka, ingekua vyema tupate ufafanuzi. Au chombo husika kutupa ufafanuzi wa swala hilo.
 
Kama ni tatizo linaongelewa kwa utaratibu, sasa ukishajiunga na hao waasi? Au ndio kuanza kukimbizana wakati nchi ni yetu, tunatoa hoja kisomi hata kama tumechoka, ingekua vyema tupate ufafanuzi. Au chombo husika kutupa ufafanuzi wa swala hilo.

Mkuu hili tatizo la ukosefu wa ajira nadhani halijakukumba vijana huku mtaani tuna hali ngumu sana wengine tunakarbia kuchanganyikiwa
 
Ajira nitapata wapi kwa stahili hii wakat vigezo vyenyewe ndo hivyo? Na sis graduates tunapenda kutumikia hizo Idara, wanatubana ili waweke watoto wao waliofeli jambo ambalo sio zuri katika ujenz wa Taifa ambalo linahitaji wasomi ili liwe na maendeleo.
 
Ajira nitapata wapi kwa stahili hii wakat vigezo vyenyewe ndo hivyo? Na sis graduates tunapenda kutumikia hizo Idara, wanatubana ili waweke watoto wao waliofeli jambo ambalo sio zuri katika ujenz wa Taifa ambalo linahitaji wasomi ili liwe na maendeleo.

We acha tu, siku hizi ni kujuana tu sio taasisi za serikali mpaka za binafsi, ndio maana waafrika tunadharaulika sana.
 
Kuna watu wana majibu mepesi sana ikizingatiwa hoja ni nzito mno. Swala la ajira ni kubwa aisee ,nadhani hapa jkt wamechemka vibaya! Mi najiuliza ilo jeshi la wasomi litatokea lini ikiwa wamewapunguza wasomi kwa kigezo cha miaka?


Tanzania nakupenda nchi yangu.
 
Lengo lao kubwa ni kusiwe na degree holders wanajeshi sijui? Vijana kibao tupo mtaani tunataka enda jeshi, kulitumikia Taifa na.pia kama kazi. Mtaani kugumu sana. Walegeze masharti yasiyo ya msingi kama ilo la umri. Itakuja.kuuma.zaidi utakaposikia.fulani na umri wake wa miaka 28 kaingia jeshini kisa ana undugu na fulani..
 
kwa mujibu wa sheria huwa ni adi miaka 33 , kuanzia form six wa mwaka huu waliohairisha mafunzo mpaka watakapograduate watakua na advantage yakuajiriwa uko.
 
Majeshi uliyoyataja yanapohitaji professionals fulani fulani huwa wanawapata kwa utaratibu wanaoujua wenyewe, usifikiri kwenda JKT na degree yako ya History ndio tiketi ya kuingia JWTZ au kwingineko jiulize inahitajika jeshini? Mbona polisi kwa mfano wanaajiri graduates kila mwaka, wale wanapitia JKT? Kuweni makini, msije kuforce kuingia huko mkapoteza time tu.
 
Majeshi uliyoyataja yanapohitaji professionals fulani fulani huwa wanawapata kwa utaratibu wanaoujua wenyewe, usifikiri kwenda JKT na degree yako ya History ndio tiketi ya kuingia JWTZ au kwingineko jiulize inahitajika jeshini? Mbona polisi kwa mfano wanaajiri graduates kila mwaka, wale wanapitia JKT? Kuweni makini, msije kuforce kuingia huko mkapoteza time tu.[/QUOTE


Jaribu kufuatilia mara ya mwisho JWTZ wamechukua graduates asee ni muda kidogo, majeshi mengine yana ajiri direct + ma service man toka JKT, JWTZ wanawachukua vijana toka JKT tuuuu, wengine sio kuteseka ni kutu mtu uli dream of, Ushawahi kutamani kua mtu flan alafu ukaona ndoto hazitimii, MM sijamaliza chuo bt kwa huo mtindo sioni kama nitafika ninapopataka, bt nikishindwa sio mbaya najua siwez kosa kaz milele ila nitakosa kazi ninayoitaka.
 
Wakuu Mtuijuze nafasi zinatoka lini? Hata kama hakueleweki nibora nijaribu tu!
 
jkt wa2 wa ajabu kwl miaka inapaswa isogezwe hadi 29,ili wa2 wapate fursa ya kwenda huko bt Gvt is just prayng a loten Game with educated civilian until when my country with wakubwa wa vyombo hv watatambua hlo?na kulitilia maanan?shame on them
 
Ingetakiwa JKT iwe miaka mwisho ni 30 maana tunabaniwa sana tulip na vigezo vyetu vya kutosha
 
Wakuu Mtuijuze nafasi zinatoka lini? Hata kama hakueleweki nibora nijaribu tu!

Nafasi zimeshatoka,watu wameshapewa barua ya kureport kambini.wanareport mwezi wa 12
 
Nafasi zimeshatoka,watu wameshapewa barua ya kureport kambini.wanareport mwezi wa 12

Kwa mujibu wa nani maana tuko na watu wa jikoni hapa wanajua kila kitu wewe unawarusha roho vijana kwa mantiki ganii??
 
Kwa mujibu wa nani maana tuko na watu wa jikoni hapa wanajua kila kitu wewe unawarusha roho vijana kwa mantiki ganii??

Mimi sibishani,na why niwarushe roho??nimeshuhudia barua kwa macho yangu,mshkaji wangu kaambiwa akareport 841 kj kigoma.endelea kuwaamini hao watu wa jikoni mkuu
 
Mimi sibishani,na why niwarushe roho??nimeshuhudia barua kwa macho yangu,mshkaji wangu kaambiwa akareport 841 kj kigoma.endelea kuwaamini hao watu wa jikoni mkuu

Au mkuu labda unaongelea wale wa kwa mujibu.?
 
Back
Top Bottom