Vigelegele vyageuka vilio

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
NYIMBO za furaha na vigelegele vilivyosindikiza safari ya kwenda kuoa, vimegeuka vilio baada lori walilokuwa wakisafiria kupinduka na kusababisha vifo vya watu wanane papohapo, huku wengine 91 wakijeruhiwa.
Ajali hiyo ilitokea jana saa 4:00 asubuhi Kijiji cha Muumbaka, Kata ya Marika, Wilaya ya Masasi,mkoani Mtwara na kuhusisha lori aina ya Canter.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, walisema gari hilo lilianza kupoteza mwelekeo wakati lilipojaribu kukata kona likiwa kwenye mwendokasi barabara kuu itokayo Masasi kwenda Newala.
Mashuhuda hao walisema watu hao walikuwa wanatoka Kijiji cha Mkaseka, Kata ya Lulindi kuelekea Kijiji cha Mandiwa, Kata ya Chigugu kwenye sherehe za harusi.

Inadaiwa kuwa bwana harusi, Juma Mwamed, alinusurika na amelazwa Hospitali ya Mkomaindo kwa matibabu, huku dereva wa gari hilo akidaiwa kutoroka.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Dk George Kumwembe, alisema wamepokea maiti wane majeruhi 61 na kwamba, hali zao ni mbaya na Hopitali ya Misheni Ndanda ilipokea majeruhi 30.

“Maiti tulizopokea ni nne, utingo wa gari hilo, Mbaraka Athuman, Thawabu Makathali, Nasra Saidi na Mwanahawa Saidi…hakuna majeruhi aliyeruhusiwa, wote wamelazwa. Pia, tunayo taarifa za Hospitali ya Misheni Ndanda imepokea majeruhi 30,” alisema Dk Kumwembe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Stephen Buyuya, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba, watu wanane wamepoteza maisha.
 
NYIMBO za furaha na vigelegele vilivyosindikiza safari ya kwenda kuoa, vimegeuka vilio baada lori walilokuwa wakisafiria kupinduka na kusababisha vifo vya watu wanane papohapo, huku wengine 91 wakijeruhiwa.
Ajali hiyo ilitokea jana saa 4:00 asubuhi Kijiji cha Muumbaka, Kata ya Marika, Wilaya ya Masasi,mkoani Mtwara na kuhusisha lori aina ya Canter.


Tunawapa pole wote waliofikwa na matatizo haya.

lakini wakati mwingine tunashindwa kufanya uamuzi sahihi on a personal level, matokeo yake tunajiingiza kwenye ajali ambazo tungeweza kuziepuka!
Fikiria hapo juu (in red) wamesema lori aina ya canter; jamani kweli canter inaweza kubeba abiria 91 ??
Kwa nini uingie kwenye gari iliyopakia abiria kuzidi kiwango chake?? Unawahi wapi/ kwani ukichelewa ndio utakuwa mwisho wa dunia?
 
aisee hawa watu zaidi ya 90 watapandaje canter!!canter ni tani 3 na nusu tu sasa sipati picha watu zaidi ya 90!!......bwana ametoa na bwana ametwaa
 
Back
Top Bottom