Vifungo mbalimbali vya kichawi/ushirikina

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
Nawasalimu kwa iina la jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Leo nimepata kitu na ningependa kushare nanyi lakini kila mtu na imani zake sijalazimisha mtu kuamini katika uchawi/ushirikina

KIFUNGO NI NINI?

Kifungo ni hali ya mtu alie na afya sahihi kushindwa kutekeleza majukumu yaliyo ndani ya uwezo wake. Kwa mfano kifungo cha tendo la ndoa, unakuta mtu hana mapungufu ya nguuvu za kiume, hana ugonjwa wala mawazo lakini anashindwa kufanya tendo takatifu la ndoa.

Vipo vifungo vya aina mbalimbali ambavyo vimekuwa vikigharimu ndoa nyingi, lakini kwa siku ya leo tutaongelea kifungo cha tendo la ndoa kwa upande wa wanaume na wanawake.

VIFUNGO VYA WANAUME

~ Mwanaume kushindwa kabisa kufanya tendo la ndoa na mkewe lakini akiwa mbali hamu(ashqi) humjia na uume kusimama. Kifungo hiki huitwa KULLI kwa jina la kitaalam na hufungwa kwa ajili ya mwanaume asifurahie tendo na mke wake.

~ Mwanaume kufanya tendo la ndia na mkewe lakini kushindwa kushusha manii(mbegu). Hiki huitwa kifungo cha KINYAMA ili mwanaume asiweze kupata watoto na amani ikosekane ndani ya nyumba.

~ Mwanaume kushindwa kufanya tendo la ndoa na mke wake, uume kusinyaa na kulala ghafla pale tu anapotaka kumuingilia mkewe. Kifungo hiki wamekiita UCHAWI MWEUSI kwa sababu huleta aibu na fedheha ndani ya nyumba.


VIFUNGO VYA WANAWAKE

~ Mwanamke kuchukia tendo la ndoa pindi anaposhiriki na mumewe na kuhisi dhiki nafsini mwake, ute kushindwa kutoka na kumsababishia maumivu makali wakati wa tendo hilo. Kifungo hiki huitwa KIZUIZI hufungwa mwanamke ili asistarehe na mumewe.

~ Mwanamke kushindwa kumaliza tendo la ndoa na mumewe na kujikuta akipoteza ladha(hisia) na raha ya tendo hilo na kumfanya apate maumivu makali katika kuta za ndani ya uke. Kifungo hiki huitwa TABALLUDI humfanya mwanamke kumuona mwanaume kama gogo kwa kukosa hisia.

~ Kujiziba uke kitu mithili ya nyama pindi mwanaume anapotaka kumuingilia mke wake, kifungo hiki huitwa KIINI MACHO hufungwa ili mwanaume aone kero kwa mke wake.

VIFUNGO VYA KUTOKUOLEWA NA KUZAA

Washirikina wanafunga watu vifungo mbalimbali hasa vya kutokuolewa na kuzaa. Ndio maana unakuta wewe unabaki nyumbani wenzako wanaolewa wewe una kazi na maisha mazuri miaka inaenda lakini hauolewi.

VIFUNGO VYA KUTOKUOLEWA :-
Vipo vitu ambavyo washirikina hawa hutumia katika kuwafunga watu ili wasiolewe, vitu vyenyewe ni :

~ Nguo za ndani za muhusika wanaomtaka asiolewe.
~ Kumtupia majini ya kumfanya mtu amuone mzee pale anapotaka kumuoa.
~ Kumfanyia uchawi uchawi wa kuonekana ananuka wakati anuki ili mtu akimtaka amuone ananuka
~ Kumuwekea mapepo ya kukataa wanaume wa maana na kuwapenda wanaume wasio na maana.

VIFUNGO VYA KUTOKUZAA : Washirikina wanafunga watu wasizae kwa kutumia dawa pamoja na uchawi wao. Silaha za maangamizi wanazotumia kumfanya mtu asizae ni pamoja na :-

~ Taulo za kike(Pedi) za mtu wanaomtaka asizae
~ Nguo za ndani za muhusika kama vile chupi, sketi taiti, blazia au sidiria
~ Kuchota nayo na kuanza kunuizia.

Sifanyi promo za waganga(jokes)

.................NAWASILISHA...............
 
Jinsi ya kufungua hivyo vifungo, ndo madam sahihi ulitakiwa kuileta hapa, Mana naona umeleta Mbinu bila kuleta tiba
 
Ukiamua kumgeukia Mungu usimuache ishi maisha yakumpendeza Mungu fanya sala fanya toba Mungu atakupa maarifa makubwa sana yakutatua mambo makubwa na shida ndogo ndogo kama hizo za kufungwa
 
Ukiamua kumgeukia Mungu usimuache ishi maisha yakumpendeza Mungu fanya sala fanya toba Mungu atakupa maarifa makubwa sana yakutatua mambo makubwa na shida ndogo ndogo kama hizo za kufungwa
Hii unamaanisha kuokoka? umeongea kirahisi rahisi sana
 
Back
Top Bottom