Vifo vya watu maarufu Iringa vinastusha sana!!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
17,871
33,235
Kwa takribani siku kumi zilizopita vimetokea mfululizo vifo kadhaa vya watu maarufu hapa Iringa hadi kuzusha maswali mengi sana.

Inawezekana Mungu ameamua kuchukua watu maarufu wanaofahamika hapa Iringa ili kuleta watu wengine maarufu wa kizazi hiki. Lakini inafikirisha sana!!
 
Mkuu Allen kwa manufaa ya Wana Iringa tulio mbali na hapo stone town ingependeza walau ungekuja na majina tuweze na sie tulio mbali kufahamu nini kinajiri
 
Sio vizuri kutaja majina ya wafu wa watu.

Lakini jana tena tumempoteza Askari Polisi maarufu sana aliyekuwa ana marafiki wa kila rika na hali. Siku tano Kabla yake aliyekuwa Dereva wa OCD naye alipoteza maisha katika staili inayofikirisha sana.
 
Bwashee sasa hao askari ndio watu " maarufu' kweli?

Ingekuwa enzi za akina Nsangalufu sawa!
 
Juzi kati nilikwenda kumtembelea rafiki yangu anakohoa, anatapika, anaishiwa pumzi, ana homa na zaidi ya yote anaishiwa nguvu. Kaambiwa kwenye Hospitali aliyokwenda kwamba hawajaona ugonjwa wowote.

Kuna diwani kaniambia alikuwa kwa siku tano nyumbani kwake anadungwa sindano za kristapeni (Benzyl penicillin Injection) na dawa zingine mbali mbali.

Sielewi ni kwa nini magonjwa wanayoumwa watu hayasemwi.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom