Vifo hivi vya nguvukazi vitavumilika hadi lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vifo hivi vya nguvukazi vitavumilika hadi lini?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Msharika, Mar 14, 2010.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mohamed Trans laua mwanafunzi


  na Berensi Alikadi, Musoma


  [​IMG]
  WATU wawili wamefariki dunia mkoani Mara katika matukio mawili tofauti, likiwamo la mwanafunzi kugongwa na basi la Kampuni ya Mohamed Trans, pamoja na mwalimu kugongwa na pikipiki na kufariki dunia papo hapo.
  Katika tukio la kwanza, mwanafunzi mmoja wa Shule ya Msingi Mwanzaburiga, Wilaya ya Musoma Vijijini, Maragera Simon (8) wa darasa la kwanza katika shule hiyo, aligongwa na kufariki dunia.
  Ajali hiyo ilitokea juzi majira ya saa sita mchana katika Kijiji cha Mwibagi na kulihusisha basi la Kampuni ya MohamedTrans lenye namba za usajili T867ASU, linalofanya safari zake kati ya Musoma na Mwanza.
  Imeelezwa kuwa baada ya basi hilo kumgonga mwanafunzi huyo halikusimama na kwamba wananchi walipiga simu katika Kituo cha Polisi Bunda ambapo walilikamata basi hilo.
  Polisi wilayani Bunda walikiri kumshikilia dereva wa gari hilo, Hamisi Bwatani (39 ) mwenyeji wa Shinyanga na kwamba anatarajiwa kupelekwa mjini Musoma ili aweze kufikishwa mahakamani kujibu shitaka la mauaji ya mwanafunzi huyo. Na katika tukio la pili, mwalimu huyo wa Shule ya Msingi Changuge, wilayani Bunda, Joshua Bisendo, alifariki dunia baada ya kugongwa na pikipiki wakati akitoka nyumbani kwake. Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Sprian Oyeri, alisema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa moja na nusu katika eneo la Nyasura na kwamba marehemu alikuwa ni mwalimu mkuu wa shule hiyo, alikuwa akitoka nyumbani kwake Mtaa wa Bunda Stoo akielekea kazini kwake.
   
 2. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Mbona hujatuambia lengo la kuweka habari hii kwenye jukwaa hili ili tujue tunachangia kuanzia wapi.
   
Loading...