Vifo: Askari wetu wana matatizo ya Kisaikolojia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vifo: Askari wetu wana matatizo ya Kisaikolojia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Elli, Jul 10, 2010.

 1. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,829
  Likes Received: 10,141
  Trophy Points: 280
  Nimepokea kwa masikitiko sana habari za kujiua kwa askari watatu katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja, wa mwisho kajiua jana huko iringa. Ukiangalia kwa undani sababu za vifo vyao vina kila dalili kuwa wamekosa mafunzo ya Kisaikolojia huko TPC mmh sijui ndo inaitwa hivyo!!!

  Inawezekana walifundishwa kuwa bunduki ni kwa ajili ya kuuwa wengine ila wao wakijipiga hawafi ( Yaani wamechukua ile assumption kwamba Mbwa hamuumi mwenyewe) wakisahau kuwa kile ni kifaa kisichokwa na hisia.

  Nimejaribu leo asubuhi Kuongea na askari mmoja na kumuuliza juu ya mtaala( curriculum) yao imebeba nini?? Ukweli ni kwamba hakuna somo la Kisaikolojia lolote linalofundishwa katika vyuo vyetu hivi sawa na wanavyosisitiza Urefu kama tija ya kuingia huko.

  Maombi yangu, nikiwa kama mwalimu na mtaalam wa Mtaala, naona kuna haja sana ya askari wetu kupatiwa social counselling ama sivyo kuna siku hata hao wakubwa wao sijui akina International Garage Post ( IGP) na majina mengine kama dawa watakuja kujiua.

  Vipi wana -research, tuandike proposal hiyo tufanye hiyo study fasta tuwasaidie Maafande wetu

  Kwaherini
   
Loading...