Vifaranga vya kuku 6,400 vyateketezwa kwa moto baada ya kukamatwa vikiingizwa nchini kinyume na sheria kutoka Kenya

a71539407cc1cb8c7823f3fc7d05d973.jpg
d5c3065e8e7d773a5acb54baf7a963d7.jpg


Wizara ya Mifugo kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani Arusha, imeteketeza kwa moto vifaranga vya kuku wa kisasa 6,400 wenye thamani ya shilingi milioni 12, wanaodaiwa kuingizwa nchini kutoka Kenya kupitia mpaka wa Namanga kinyume na sheria. Vifaranga vilivyoingizwa nchini kinyemela kuteketezwa

My take
Hizi si akili za kawaida hakika, na huenda nchi hii hupata laana kutokana na baadhi ya viongozi kama hawa. Unachoma kifaranga kwa maana gani? Hii siyo haki kabisa na ni ukatili kwa kiumbe hai kisichokuwa na hatia wala utambuzi.
Mijitu mingine Mingese daima na daima...Laana iwe Juu yao

Sifa zingine za kutaka kuonekana mtu unafanya kazi kwa bidiii mwsho wa siku ni Umaku kama huuu..Sina tu kauli ila sijui yani.
 
Daaaaaah! Kifaranga nae anaadhibiwa kwa kosa gani?Hapo akili haikutumika kabisaaa.
Hao ni viumbe hai jamani, hata huruma hawakuifeel?
Hao ni mashetani.
Walikosa hataa akili ya kuvipiga mnada ili vikafugwe wachukue hiyo pesa ikajenge taifaa?

Sent from my TECNO-C5 using JamiiForums mobile app
 
Kama ni kweli huu ni ujinga wa hali ya juu, nathani bunge linatakiwa litunge sheria za kulinda viumbe hai, isiwe tu wanyama pori. Mtu kama huyu anatakiwa afungwe miaka hata mitano ajifunze kuheshimu viumbe vya Mungu. Mungu aliumba kwa siku sita akasema ni vyema tena vyapendeza halafu mtu anafanya ukatili huu kweli
 
Busara ingetumika Zaidi kuliko kuteketeza vifaranga Hivyo Inchi imepata hasara x2 imekosa kodi au faini pili imekosesha Vijana ajira tumekosa vitu tena Zaidi ya viwili wengine mtajaza au kuainisha Zaidi hasara hizo
 
Wangevirudisha vilipotoka au wangeviuza hela ingetumiwa kwa kazi zingine.
Daaaaahhhh. Inauma sana
 
Hiy hasar *2 wot walioshrk ktk hil mung anawaon mjue vile n viumb kma viumbe wengne wahuck wa i kitu mlifny kw kushnkizw am kw akli zenu tmamu.....assume wtnznia wnkamtw nchi jrn fln af uamuz wa mwisho kwa kukuw wmeingia nch fln kinyum ch sheria bhc WACHOMWE MOT je hii n saw...wahck wa hak za wanyam mko wap!!!!inasikitish san lkn co mbay i ndiy TZ.
 
Kwa watu wenye hofu ya mungu ni ngumu kufanya kitu kama hicho, hii inaonesha ni kwa namna gan watu waliopewa mamlaka wanavyoweza kuwa makatili wakipata nafasi ya kufanya hivyo
 
Naomba haki za wanyama na viumbe hai waingilie hili swala si la kawaida hata kidogo
 
Kwa upande mwingine kuviteketeza ni sahihi kwa sababu hatujui afya ya hivyo vifaranga. Vikiachwa vinaweza kuleta magonjwa kama mafua ya ndege ambayo ni hatari kwa ndege wote na kupambana na ugonjwa huo ni ghali sana

Mkuu who gives you the right to assume?? Na wahamiaji haramu nao, Wachomwe moto? Maana hatujui wamebeba magonjwa gani. Kumbuka all this happened kwa assumptions.. If anything walitakiwa kuwapima magonjwa alafu ndiyo watoe maamuzi ila si kuwachoma tuu moja kwa moja, wale ni wanyama na wana uhai, wana haki ya kuishi. Huu ni ukatili sana tena mkubwa mno.

'fumbokuu' nakuomba sana tena sana, siku nyingine jaribu kutumia angalau commonsense kwanza kabla ya kutoa maoni.
 
Haya, mliodhani huu ujinga na ukaidi wa mtu mmoja au wawili hautaligharimu taifa hebu someni hii hapa:

Kenya imewasilisha malalamiko rasmi kwa Tanzania, kuhusiana na kile serikali mjini Nairobi, inachokieleza kuwa "mabadiliko ya Kisera" yanayopuuza vitendo vya uhasama dhidi ya raia wa Kenya na maslahi yao ya kibiashara. Hii inafuatia kitendo cha kuteketezwa vifaranga 6400 vilivyoingizwa nchini Tanzania pamoja na tukio jingine la kupigwa mnada hivi karibuni ng'ombe kiasi 1325 kutoka Kenya. Kenya imemuita balozi wa Tanzania Nairobi kutoa maelezo kuhusiana na tukio hilo. Hata hivyo waziri wa mifugo na Uvuvi wa Tanzania Luhaga Joelson Mpina anasema ng'ombe waliopigwa mnada hawana mwenyewe na hatua walizozichukua zinazingatia sheria ya Tanzania.
Source: DW

dw.jpg
 
Back
Top Bottom