Serikali: Julai 30 mwisho wa Uingizaji wa vifaranga vya Kuku nchini

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,023
1,609
Serikali ya Tanzania imesema, haitaruhusu kuingiza vifaranga vya kuku nchini na haitatoa tena vibali vya kuingiza vifaranga hivyo kuaniza Julai 30, 2022.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi leo Jumamosi Julai 23, 2022 imesema Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema baada ya Julai 30, hakuna vifaranga vya kuku vitakavyoingizwa hapa nchini na Serikali haitoi tena vibali vya kuingiza vifaranga hivyo.

Taarifa hiyo imesema, Ulega amebainisha hayo jijini Dodoma wakati wa kikao cha wizara na wadau wa tasnia ya kuku, kujadili namna ya kukuza tasnia hiyo,

Lengo la hatua hiyo ni utekelezaji wa sheria ya mwaka 2006 ambapo Serikali imekuwa ikizuia uingizaji wa vifaranga nchini kutoka nje ya nchi ili kudhibiti ugonjwa wa mafua ya ndege kwa mifugo jamii ya ndege na kulinda wazalishaji wa kuku ndani ya nchi.

Akifungua kikao hicho kilichojadili ajenda mbalimbali zikiwemo za upatikanaji wa vifaranga vya kuku, chakula cha kuku na bei ya kuku sokoni, Ulega amesema Serikali inategemea haitaona vifaranga vinaingizwa nchini kutoka nje ya nchi.

Ametaka kuwepo kwa mfumo wa taarifa zinazohusu wazalishaji wa vifaranga vya kuku kuanzia wazalishaji wakubwa hadi wadogo ambao wamesajiliwa na kutoa taarifa serikalini ili kuiwezesha kujua kiwango cha uzalishaji na kuwa na takwimu sahihi juu ya mahitaji ya vifaranga nchini.

“Ni mategemeo yetu ni kutokuona baada ya tarehe 30 mtu anaingiza vifaranga hapa nchini kutoka mahali popote pale, jambo la pili kuwepo na mfumo ambao utasaidia serikali kujua ni kiasi gani cha uzalishaji vifaranga ndani ya nchi yetu ili kujipima uwezo wetu na mahitaji yetu ndani ya nchi,” amesema Ulega

Chanzo: Mwananchi
 
Nadhani ilitakiwa kuanza na hili jambo la pili kabla ya kuzuia uingizaji.

"jambo la pili kuwepo na mfumo ambao utasaidia serikali kujua ni kiasi gani cha uzalishaji vifaranga ndani ya nchi yetu ili kujipima uwezo wetu na mahitaji yetu ndani ya nchi,” amesema Ulega
 
Ni taarifa ya kushangaza hii iliyoripotiwa hapa.

Inawezekana mwandishi wa habari ndio kawa chanzo cha mkanganyiko kwa kutotoa taarifa kamili, maanake hii habari ilivyokaa hapa haileti maana kabisa.

Lakini kama taarifa yenyewe ndiyo hivyo ilivyoripotiwa, basi nadhani hata huyo waziri atakuwa hajui kitu kabisa.

Hajaeleza lolote kuhusu uwepo wa vifaranga vya kutosha vinavyozalishwa hapa nchini. Kinachosisitizwa tu ni kutotoa ruhusa ya kuingiza vifaranga toka nje, bila ya maelezo ya kujitosheleza kwa nini iwe hivyo.

Jambo linaloweza kudhaniwa hapa ni kuwa kuna uwezekano wa watu maalum (cartel) wanaotaka kuhodhi biashara hii kwa manufaa yao wenyewe.
 
Serikali ya Tanzania imesema, haitaruhusu kuingiza vifaranga vya kuku nchini na haitatoa tena vibali vya kuingiza vifaranga hivyo kuaniza Julai 30, 2022.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi leo Jumamosi Julai 23, 2022 imesema Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema baada ya Julai 30, hakuna vifaranga vya kuku vitakavyoingizwa hapa nchini na Serikali haitoi tena vibali vya kuingiza vifaranga hivyo.

Taarifa hiyo imesema, Ulega amebainisha hayo jijini Dodoma wakati wa kikao cha wizara na wadau wa tasnia ya kuku, kujadili namna ya kukuza tasnia hiyo,

Lengo la hatua hiyo ni utekelezaji wa sheria ya mwaka 2006 ambapo Serikali imekuwa ikizuia uingizaji wa vifaranga nchini kutoka nje ya nchi ili kudhibiti ugonjwa wa mafua ya ndege kwa mifugo jamii ya ndege na kulinda wazalishaji wa kuku ndani ya nchi.

Akifungua kikao hicho kilichojadili ajenda mbalimbali zikiwemo za upatikanaji wa vifaranga vya kuku, chakula cha kuku na bei ya kuku sokoni, Ulega amesema Serikali inategemea haitaona vifaranga vinaingizwa nchini kutoka nje ya nchi.

Ametaka kuwepo kwa mfumo wa taarifa zinazohusu wazalishaji wa vifaranga vya kuku kuanzia wazalishaji wakubwa hadi wadogo ambao wamesajiliwa na kutoa taarifa serikalini ili kuiwezesha kujua kiwango cha uzalishaji na kuwa na takwimu sahihi juu ya mahitaji ya vifaranga nchini.

“Ni mategemeo yetu ni kutokuona baada ya tarehe 30 mtu anaingiza vifaranga hapa nchini kutoka mahali popote pale, jambo la pili kuwepo na mfumo ambao utasaidia serikali kujua ni kiasi gani cha uzalishaji vifaranga ndani ya nchi yetu ili kujipima uwezo wetu na mahitaji yetu ndani ya nchi,” amesema Ulega

Chanzo: Mwananchi
Haya ndio mambo sasa ,inatakiwa tupromote wajasiriamali wetu bidhaa zao na kuacha utegemezi WA bidhaa za nje zinazoua soko la bidhaa zetu
 
Hiyo Ni Roho mbaya Nchi haina uwezo wa kuzalisha vifaranga vya kuyosheleza soko na pia hakuna mbegu Bora ya vifaranga .
Kenya ,Malawi,Zimbabwe , Botswana nk. Huzalisha vifaranga vya kutosheleza masoko Yao ya ndani na kuuza Nje ss tumekalia siasa ,siasa ,siasa mpyuuuuu
 
Nchi za kijamaa / kikomunisti akili zao matope Sana ninyi hata sukari ya ndani ya Nchi haiwatoshi mkiingiza ya Zambia au Malawi mnapiga kelele Roho za kichawi mtaacha lini ??
Kuna mlevi mmoja alichoma vifaranga toka Kenya
Hatimaye Mungu Kaamua ugomvi...
 
jambo la pili kuwepo na mfumo ambao utasaidia serikali kujua ni kiasi gani cha uzalishaji vifaranga ndani ya nchi yetu ili kujipima uwezo wetu na mahitaji yetu ndani ya nchi,” amesema Ulega
Unapigaje marufuku uingizaji wa vifaranga toka nje kabla hujafanya tathimini na kuwa na taarifa sahihi kama uzalishaji wa vifaranga ndani ya nchi unatosheleza mahitaji ya ndani?
Maamuzi ya ajabu sana haya!
 
Nchi za kijamaa / kikomunisti akili zao matope Sana ninyi hata sukari ya ndani ya Nchi haiwatoshi mkiingiza ya Zambia au Malawi mnapiga kelele Roho za kichawi mtaacha lini ??
Kuna mlevi mmoja alichoma vifaranga toka Kenya
Hatimaye Mungu Kaamua ugomvi...
Una akili fupi mno , kama hujui effects za excessive importation na trade imbalance inavyoathiri wajasiriamali wengi na kunufaisha wachuuzi wachache kaa kimya ,
Pumbav
 
Wajasiriamali WA ndani lazima walindwe Kwa mustakabali mwema WA ajira na survival ya hao wajasiriamali +economy ya nchi .
We unafikiri Marekani ni mpumbav alivyopiga marufuku baadhi ya bidhaa toka China na nchi nyingine ili kuilinda soko la wajasiriamali na ajira za watu wake ? , Bidhaa kama agricultural equipments ,machineries ,fire arms nk

Nchi zote zilizoendelea ziko sensitive kwenye kuprotect wazalishaji WA ndani , sasa Tz hapa wazalishaji WA ndani WA kuku na bidhaa za poultry wapo kibao Ila bado tunaincourage uchuuzi WA bidhaa hizo ambazo kiufupi zinaua biashara za hao wazalishaji WA ndani ,yet hatutakuwa na uwezo WA kuwapa mazingira mazuri ya kutanuka na kuweza kuexport kitu ambacho kitakuwa na advantage kubwa ya Sisi kuearn fedha za kigeni .
Huwezi kuendelea Kwa kutengeneza uchumi WA kuconsume Tu na uchuuzi bila wewe kuwa strategic na wewe kuzalisha na kuuza nje , trade imbalance ni economy killer
 
Ni taarifa ya kushangaza hii iliyoripotiwa hapa.

Inawezekana mwandishi wa habari ndio kawa chanzo cha mkanganyiko kwa kutotoa taarifa kamili, maanake hii habari ilivyokaa hapa haileti maana kabisa.

Lakini kama taarifa yenyewe ndiyo hivyo ilivyoripotiwa, basi nadhani hata huyo waziri atakuwa hajui kitu kabisa.

Hajaeleza lolote kuhusu uwepo wa vifaranga vya kutosha vinavyozalishwa hapa nchini. Kinachosisitizwa tu ni kutotoa ruhusa ya kuingiza vifaranga toka nje, bila ya maelezo ya kujitosheleza kwa nini iwe hivyo.

Jambo linaloweza kudhaniwa hapa ni kuwa kuna uwezekano wa watu maalum (cartel) wanaotaka kuhodhi biashara hii kwa manufaa yao wenyewe.
Unashangaa hili wakati kipindi cha jiwe, vifaranga vilikuwa vikikamatwa na kutiwa moto? Tena kulikuwa hakuna hata hiyo notisi ya siku 30, ni ghafla tu
 
Haya ndio mambo sasa ,inatakiwa tupromote wajasiriamali wetu bidhaa zao na kuacha utegemezi WA bidhaa za nje zinazoua soko la bidhaa zetu
Hadi uzalishaji wa vifaranga wajasiriamali wa ndani wanahitaji kulindwa?
Hivi kuna ntu mtu ataagiza vifaranga nje ambavyo ni gharama zaidi kama kuna wazalishaji wazuri wanawe kutosheleza soko? Mbona tunakuwa tunadeka sana? Hadi kuzalisha vifaranga tulindwe?????
 
Una akili fupi mno , kama hujui effects za excessive importation na trade imbalance inavyoathiri wajasiriamali wengi na kunufaisha wachuuzi wachache kaa kimya ,
Pumbav

Kwani biashara yetu na China imekaaje? Hivi kuna trade balance kati yetu na China? Unampiga majungu na roho mbaya muafrika mwenzako wakati India na China wapo wanalipopoa soko letu kama ndege aina ya tai mbele ya mzoga hiyo inakua akili au Takataka
 
Hiyo Ni Roho mbaya Nchi haina uwezo wa kuzalisha vifaranga vya kuyosheleza soko na pia hakuna mbegu Bora ya vifaranga .
Kenya ,Malawi,Zimbabwe , Botswana nk. Huzalisha vifaranga vya kutosheleza masoko Yao ya ndani na kuuza Nje ss tumekalia siasa ,siasa ,siasa mpyuuuuu
Kwani kuna ugumu gani kuzalisha vufaranga bora? ,
 
Back
Top Bottom