Vifaa Vya Samsung Galaxy S4

Vifaa Vya Samsung Galaxy S4

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159
23/03/2013

Samsung Galaxy S4 inatarajiwa kuingia madukani mwezi ujao, simu ambayo tayari imeshatabiriwa kufanya mauzo makubwa mno mwaka huu kutokana na uzuri wake. Hata hivyo uhondo wa simu hiyo utaongezeka iwapoutaiongezea vikorombezo kadhaa ili kuweza kuitumia vizuri na salama zaidi. Tutazungumzia vikorombwezo mbali mbali vitakavyo ifanya Galaxy S4 izidi kuwa ya kipekee. Bila ya shaka Samsung wamegundua kwamba iPhone inawazidi mno kwa vifaa mbali mbali vinavyotumika na simu hiyo, hivyo badala ya kuachia kampuni nyngine zitengeze vifaa hivyo, Samsung wameamua kutengeneza wenyewe.
​
Chaji isiyo na Waya: Chaja hii ni inatumia teknolojia ya Qi sawa na ile iliyotumika kwenye Palm Touchstone miaka kadhaa iliyopita. Ingawa Samsung walithibitisha uwepo wa gajeti hii tangu siku ya uzinduzi, bei yake bado haikutangazwa rasmi. Pia Samsung hawakuthibitisha ni lini hasa chaja hizi zitaanza kupatikana madukani. Kwa kawaida chaja hizi huwa zina chaji simu kwa kasi ndogo, yaani huchukua muda mrefu zaidi, lakini ukizingatia matatizo ya micro USB katika kuchaji basi inakhalisi kuinunua ili kuipa usb port yako maisha marefu zaidi.

​
Samsung Gamepad: Hii ni sherehe kwa wacheza game kwenye simu, tukizingatia kwamba Galaxy S4 ina skrini yenye ukubwa wa karibu 5", bila ya shaka wacheza game wataburudika. Pad hii inafanya kazi na simu yoyote yenye bluetooth 4.0 au near field communication (NFC), kwani yoyote miongoni mwa teknolojia hizo huweza kutumika kuunganisha na simu yako na kupata hisia za vifungo halisi katika game badala ya skrini mguzo, bei ya gajeti hii ni $113. Gajeti hii inaweza kutumika na simu ambayo haizidi 6.3" kwa ukubwa, hivyo si kwa ajili ya Galaxy S4 peke yake bali hata wenye S3 wataweza kuitumia. Kwa pad hii unaweza ukapata hisia halisi za PS Vita.
​
Mizani ya Samsung: Mizani hii ambayo imetengenezwa na Samsung inakuwa ni sehemu ya matumizi ya app ya Samsung S Health, ambapo bila ya kutumia waya kila unapojipima mizani hii itapeka taarifa ya uzito wako kwenye app ya S Health iwapo utaiunganisha kwa teknolijia ya bluethooth, hivyo kuweza kuhifadhi historia ya uzito kwa muda mrefu na hivyo kujua mwelekeo wa uzito wako kama unazidi au kupungua kwa haraka mno bila ya kujali kuandika andika kila unapojipima. Mizani hii inaweza kuhifadhi taarifa za watumiaji saba mbali mbali bila ya kuwachanganya.

​
S Band: Mwaka 2013 ni mwaka wa mfumuko wa gajeti za kuvaa, fununu kuhusu iWatch zimesambaa, Samsung wamewatangulia Apple kwenye hili, S Band ni bangili itakayokuwa inakusanya taarifa za kiafya na kuzipeleka kwenye app ya S Health, yaani hii hufanya kazi mfano wa Nike Fuelband, hivyo inatoa kalori ulizounguza kwa usahihi, hatua ulizotembea au kukimbia wakati wa mazoezi na kulinganisha kama umefikia malengo ya mazoezi yako, pia iwapo itaingiza taarifa za chakula ulichokula utaweza kujua kuzidi au kupungua kwa kalori mwilini. Taarifa zote hizi zitahifadhiwa kwenye app ya S Health.
​
S View Cover: Hili ni gamba la simu ambalo huhitaji kufungua gamba lako kabla ya kutambua ni nani anayekupigia simu, hii ni kwa sababu lina sehemu ya kidirisha chenye plasitki inayoonyesha (transparent) na hiyo ndio sehemu inayotoa taarifa za namba au jina la anayekupigia simu. S View inatarajiwa kupatikana siku ambayo simu itatolewa kwenye mwezi April. Kwa wale watakaokuwa hawakulipendelea gamba hili Samsung pia watatoa gamba la aina ya kipochi na protective cover ambalo ni aina ya mfunguko wa kitabu.
​
S Heart Rate Monitor: Huu ni mkanda unaovaliwa kifuani na pia ni sehemu ya S Health app, hutoa taarifa za mapigo ya moyo ili kuepusha mambo yaliyomkuta Fabrice Muamba mwaka jana wakati Bolton Wanderer wanapambana na Tottenham Hotspurs. Moyo wa Muamba ulisimama ghafla wakati wa pambano hilo. Kwa kutumia mkanda huu unaovaliwa kifuani utaweza kutambua mwenendo wa mapigo ya moyo na kuhifadhi historia ya mwenendo wa moyo wako kwenye S Health.

​
Premium Headset: Mbali na headphone za kawaida zitakazokuja ndani ya box la simu hiyo Samsung watatoa pia headset zenye nguvu na sauti bora zaidi, headset hizi zimetengenezwa zikiwa na woofer pamoja na tweeter ili kuboresha sauti na hasa bezi. Pia kwa nyuma zina tundu ya kutoa hewa ili sauti isichafuke.

Kwa wale ambao muziki sio jambo kubwa basi headset zinazokuja na simu yenyewe zinatosha kutumika na Samsung Galaxy S4 bila ya matatizo yoyote.
​
Chaja na Betri ya Ziada: Iwapo utanunua na kutumia vifaa vyote hivi bila shaka betri yako haitadumu zaidi ya masaa 8, hivyo chaja hii itakupa betri ya ziada na uwezi wa kuchaji betri bila ya betri kuwemo kwenye simu. Pia hii kwa wale ambao macho hayabanduki kwenye simu kila baada ya muda mfupi (heavy users) basi huenda wakaihitaji mno, hasa ukizingatia ukubwa wa skrini ya simu hii.

Iwapo unajirayarisha kununua vifaa vyote hivi huenda vifaa hivi vikagharimu fedha nyingi zaidi kuliko simu yenyewe.

Chanzo:
Gajetek Habari: Vifaa Vya Samsung Galaxy S4
​
 
ahsante Miller kiukweli unafanya makubwa sana kutujuza habari za technolojia mimi sina comment zaidi ya kukupongeza
 
Dah!!ama kweli kuna watu wanafaudu....wakina rizimoko kazipanga kama tano hivi mezani,sisi wagonga ulimbo tutazisoma kama hivi jf tu...ubarikiwe mleta uzi walau nimejua ya dunia!!!
 
Back
Top Bottom