Views za YouTube zinahesabiwaje? Video ina Views Billion 10 na Dunia ina watu 7.9B

Boss Man

JF-Expert Member
Feb 10, 2022
458
991
Duniani tupo watu 7.9B lakini Baby Shark Ina views Billion 10 (10B) Hawa watu billion 1.2 wametoka wapi ni wakina nani hao wame view?

Hili swala limegawa watu kwenye makundi mawili na kila kundi likiamini wao ndio wako sahihi na wanachokiongea na hadi Sasa Mimi Binafsi sijajua jibu sahihi ni lipi

(1) Kundi la kwanza wanasema Views ni idadi ambayo video imetazamwa, ila viewers ni idadi ya namba ya watazamaji.

Kwa mfano mm Boss Man is one viewer so nikitizama YouTube video mara 7, that is counted as 1 viewer but its 7 views.
Yani mtazamaji 1 ametazama mara 7, so kama video isipotazamwa na mtu mwingine nikatazama mm mwenyewe mara milioni 1 basi hiyo video itakuwa na 1 milioni views

(2) Kundi la pili wanasema kwamba 1 viewer brings 1 view, No matter how many times you re-watch it will forever remain 1 view.. It only counts to 2 if and only if you watch again from a different account.

Yani hata kama Ukiangalia video mara milioni moja kwa kutumia Google account Ile ile basi view itahesabika moja tu,

Sasa kama Kuna ukweli kwenye hayo maelezo ya kundi la pili, je hiyo Video ya Baby Shark imepataje views billion 10?

MUNGU NI MWEMA

Picsart_22-06-24_13-29-32-465.jpg
 
Hujui mtu anaweza tazama Mara kumi ?,kwa mfano,Mimi Kuna videos YouTube nimezitazama zaidi ya Mara 30
Viewers wa YouTube sio mtu mmoja mmoja Bali wanahesabu Ni Mara ngapi hiyo video imetazamwa
 
Mbona rahis hiyo nenda youtube funguo video ya zaman kidogo ambayo haiko kwenye trending kisha angalia view zao kisha angalia wewe ujione utakua wangap kwenye view kisha ngalia mara tano uone je view imekuaje.
 
Katuni ndo zinaongoza kwa viewers.
Kuna jamaa anajiita D Bilioni yeye video zake huwa viewers si chini ya bilioni moja.
 
Hujui mtu anaweza tazama Mara kumi ?,kwa mfano,Mimi Kuna videos YouTube nimezitazama zaidi ya Mara 30
Viewers wa YouTube sio mtu mmoja mmoja Bali wanahesabu Ni Mara ngapi hiyo video imetazamwa
Hiyo mara 30 kama ulitumia google account 30 sawa, ila kama ulitumia google account 1 u'r wrong
 
Hata kama views ni 1 view = 1 account basi ujue kuwa kuna watu wana views videos bila ku sign in na kuna wengine wana more than 1 account
 
Back
Top Bottom