Vietnam War katika kumbukumbu.

Vietnam War katika kumbukumbu.

Explainer

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2015
Posts
517
Reaction score
508
vietnam-1.jpg

Kutokana na rangi ya ngozi zao waweza fikilia ni moja wapo wa askari wetu wa JWTZ, lakini sivyo hivyo bali ni askari wa kimarekani wakiwa katika uwanja wa vita huko Vietnam.
Leo ikiwa ni siku nyingine tena, siku tulivu kabisa, napenda kuutambua uwepo wenu hapa JF maana nadhani tupo zaidi ya member 449,730 na zaidi hivi kama sikosei, pia tukiwa na wageni zaidi ya 5,054 hivi ijapokuwa idadi hubadilika badilika, nawashukuru sana kwa uwepo wenu Wakuu.
Leo ningependa nizungumzie kidogo kuhusu historia ya taifa la Vietnam na vita vilivyopiganwa na wa-vietnam na Wamarekani katika miaka ya 1955 na kuendelea kwa miaka kadhaa mbele.
Habari hii itakuwa na muendelezo kutokana na upana wake katika maelezo na mafafanuzi katika historia kuhusu Vietnam.
Wakati Vietnam ya kaskazini ikiingia ulingoni kupambana na Marekani, Marekani wakati huo ilishapigana vita dhaidi ya tisa, ambapo tunakumbuka Revolution war ambapo walikufa askari 4,435
war of 1813-waliokufa 2,260
Mexican war- 13,283
civil war -498,332
spanish American war- 2,446
World war (i)- 116,516
World war (ii)- 405,399
Korean war -54,246

Ndipo ikafuatia Vietnam war, na mission nyingine nyingi zilizofanywa na Wamarekani.


Vietnam likiwa ni taifa lililopo kusini mashariki mwa bara la Asia, wakati huo likiwa chini ya utawala wa kikoloni wa Kifalansa tangu karne ya 19.
Kwa wale wapenzi wa movie za kivietnam mnakumbuka jinsi hawa jamaa walivyokuwa noma sana katika medani ya mapambano vitani.
d97e08e17c50a3377317a3d4bf0cbb22--vietnam-history-viet-cong-1.jpg
Pichani juu ni"askari wa kivietnam wakiwa katika uwanja wa vita"
Tunakumbuka pia wakati vita vikuu vya Dunia (world war ii ) vikiwa vimepamba moto, vikosi vya japani vilitiananga Vietnam na kuivamia ili kupigana na utawala wa kikoloni wa Kifalansa, lakini kufuatia kwa kushindwa japani mwaka 1945 katika vita kuu ya pili, japani iliondoa vikosi vyake kutoka Vietnam na kuacha Mfalme aliyefundishwa na wafalansa waliokuwa watawala wa kikoloni dhidi ya wa-vietnam alieitwa Bai Dai. Unajua wakati ule kulikuwa na mapigano makali kati ya vikosi vya Marekani na wajapani, ambapo kuna makala nyingi, movie na documentaries kuhusu sehemu ya vita vikuu vya pili vya Dunia vilivyo ghalimu maisha ya watu wengi zaidi kuliko katika vita vikuu vya kwanza.
Hivyo kuifanya Japani kuonekana kama moja wapo ya taifa Sumbufu sana katika wakati huo.
Tukirudi kwa upande wa Vietnam, baada ya mfalme Bao kukabidhiwa nchi, kulitokea mgawanyiko ndani ya nchi ya Vietnam, baadhi ya viongozi wakiongozwa na bwana Ho, Ho Chi Minh, huyu jamaa kwa heshima yake jina lake limepewa mji mmoja wapo mkubwa wa Vietnam pale Ho Chi Minh city, mji mzuri kweli kweli kwa utalii na historia ya Vietnam.
Sasa baada ya mgawanyiko huo bwana Ho na wafuasi wake waliondoka mara moja huku wakichukua mji wa kaskazini mwa Vietnam, mji ulioitwa Hanoi na kisha kutangaza kuwa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Vietnam (DRV) na bwana Ho akiwa kama Rais.
220px-Ho_Chi_Minh_1946.jpg
"Huyu pichani ndie Ho Chi Minh mwenyewe,mtu ambaye watu wa Vietnam wanamkumbuka vyema kwa matendo yake na maneno mazito yenye sumu kali'
kuna baadhi ya misemo yake ambayo inakubalika sana kama vile

" Watu wa Vietnam kwa undani wanapenda uhuru, uhuru na amani. Lakini katika uso katili wa Marekani wamefufuka, wameungana kama mtu mmoja. Kumbuka dholuba ni fursa nzuri kwa pine (aina ya mti) na cypress (aina ya mti pia) kuonyesha nguvu zao na utulivu wao, ilikuwa ni patriotism, si ya kikomunisti ambayo imeniishia."
Bwana Ho aliamini sana katika falsafa za kikomunisti za uchina pamoja na Soviet ya wakati huo, ndio maana katika vita vya Vietnam tunaona baadhi ya askari wa kirusi wakisaidia upande mmoja wa Vietnam ya kaskazini. Pia Ho walianzisha Viet Minh au unaweza kuita ligi ya uhuru wa Vietnam.
Sasa wakati Vietnam ikigawanyika katika pande mbili yaani upande wa Mfalme Bao na upande wa kaskazini wa bwana Ho aliejitangazia Jamuhuri ya kidemokrasia ya Vietnam kwa upande wa kaskazini katika mji wa Hanoi, Hapo ndipo Ufalansa lililokuwa koloni la zamani kuamua kumuunga mkono Mfalme Bao ili kudhibiti tena mkoa huo wa Hanoi hivyo kuanzisha state ya Vietnam mnamo mwezi julai 1949 na mji mkuu ukawa Saigon.
Wakati huo pande zote mbili za wa-vietnam zilihitaji kitu kimoja, Vietnam yenye umoja na nguvu, lakini wakati huo huo bwana Ho Chi Minh na wafuasi wake wakiitaji taifa kusimamia katika misingi ya kikomunisti kama ilivyo kwa uchina na Soviet, huku Mfalme Bao na wafuasi wake wakiitaji Vietnam iendeleze uhusiano wa karibu wa kiuchumi na kitamaduni wa kimaghalibi yaani kule kwa watawala wao.
Hapo sasa ndipo msuguano ulipoanzia, baada ya Majeshi ya kikomunisti ya Bwana Ho kudhibiti eneo la kaskazini mwa Vietnam, migigoro na mapigano yalizuka baina ya Majeshi ya kaskazini ba kusini, vita hivyo viliendelea hadi mwezi Mei 1954 ambapo vilimalizika kwa kushindwa kwa vikosi vya mfalme Bao. Hivyo Kufanya mfalme Bao na mshirika wake mkubwa ufalansa kushindwa vita huko Indochina.
lakini licha ya kushindwa kwa Mfalme Bao, mkutano wa pamoja wa wa-vietnam uliweka mkataba uliosainiwa mnamo julai 1954 kati ya makubaliano ya Ho kudhibiti kaskazini na Bao kudhibiti kusini, pia mkataba huo ulitaka kufanyike uchaguzi wa kitaifa wa kuunganisha ambapo ungefanyika mwaka 1956.
Lakini kabla ya mwaka huo wa uchaguzi wa pamoja uliopangwa ufanyike mwaka 1956,mwaka 1955 mwanasiasa mkuu wa kupambana na kikomunisti bwana Ngoja Doing alimfukuza Mfalme Bao na yeye kuwa Rais wa serikali ya Jamuhuri ya Vietnam kusini (GVN) hivyo kukawa na Jamuhuri mbili kinzani.
Hapa sasa ndipo msingi wa vita vya Vietnam kupamba moto kwa miaka mingi baada ya ndugu zetu wale wa America First kuona fursa dhidi ya kuvunja umoja wa usoviet popote pale duniani utakapo jitokeza. Kama utakuwa ulipitia Thread yangu iliopita iliyobeba jina la Patrice Lumumba utakuwa umefahamu kidogo jinsi ya Marekani na washirika wake walivyojitahidi kudhibiti jitihada za Patrice katika kule kuomba kwake msaada kwa Soviet, maana wakati huo kulikuwa na sekeseke kubwa la cold war hivyo kuifanya Marekani kuwa macho na taifa lolote au mtu aliejaribu kuunganisha nguvu na usoviet, na katika jitihada zake kuna maeneo waliyoweza kuyaendesha vyema ila hapa kwa wa-vietnam waliipata joto ya jiwe
Ho Chi Minh biography2_fadd83cd.jpg
"Bwana Ho Chi Minh akiwa na wafuasi wake"
( Itaendelea katika sehemu ya pili, pale ambapo vita rasmi vilipoanzia na kwa pamoja tutaingia hadi ndani kabisa ya uwanja wa vita) #La Nuit


"Si kazi rahisi"
#SEHEMU YA PILI INAPATIKANA KATIKA POST NAMBA 26:
 
itaendelea 😑😑😑
itaendelea😐😐😐
itaendelea 😟😟😟
itaendelea 😠😠😠
skuizi jf inauandishi kama hadithi za shigongo full kuitaendelea.
 
Back
Top Bottom