Viepuke hivi, visingizio, vimechelewesha wengi kufanikiwa kifedha

Kibenje KK

JF-Expert Member
May 28, 2016
267
380
VISINGIZIO HIVI VIMECHELEWESHA WENGI KUFANIKIWA KIFEDHA.

Achana navyo mara moja.

"visingizio ni kichaka cha watu waliojikatia tamaa ya mafanikio."

Ukiona mtu yeyote anajivunia visingizio huyo ujue alishajitoa kwenye safari ya watu wanaopambania ukuu wao.

Yaani amechagua kuwa mtu dhaifu asiye na nafasi katika Kambi ya matajiri.

Sasa visingizio hivi ni moja ya chanzo cha watu wengi kuchelewa au kushindwa kabisa kufanikiwa..

Fanya kila unaloweza kuepuka visingizio hivi, maana havitakufikisha popote..

KISINGIZIO NO 1

BIASHARA YANGU NI NDOGO SIWEZI KUFANYA MAENDELEO YOYOTE.

Hii imani inatengeneza kisingizio kinachokufanya ushindwe kabisa kufanya mambo makubwa.

Shida ya imani ni kwamba huwezi kufanikiwa zaidi ya unavyoamini.

Hakikisha hujiwekei ukomo wa imani, kwa sababu kuamini MAKUBWA hakuhitaji gharama yoyote.

Acha kujihukumu kwa hali uliyonayo, kwa sababu hali yako ya sasa siyo hatima yako ya badae.

KISINGIZIO NO 2.

MSHAHARA WANGU NI MDOGO SIWEZI KUWEKA AKIBA.

Unapokuwa na imani hii ni rahisi kujikuta siku zinaenda miaka inasogea pasipo kufanya kitu cha maana..

Tumia udogo wa mshahara kuwa chachu ya kupambana ili kuongeza kipato chako..

Lakini pia jifunze kutunza akiba kidogo kidogo ikiwezekana tenga hata 10% au 5%.

Ukifanya hivyo kwa uaminifu utashangaa sana utajikuta unaanza kuinuka taratibu.

Hakikisha haubakii hapo ulipo, jipambanie angalau utembee mdogo mdogo, bado unayo nafasi sawa na wengine.

KISINGIZIO NO 3.

NITAKUWA NA NIDHAMU YA FEDHA NIKIWA NA KIPATO KIKUBWA.

Ndugu yangu nikwambie ukweli, kuwa na kipato kidogo haipaswi iwe sababu ya kukosa..

Nidhamu ya fedha bali inapaswa kuwa hamasa zaidi ya kuwa na nidhamu ya fedha..

Kwa sababu kitu kikiwa kidogo ndipo kinahitaji umakini mkubwa katika matumizi.

KISINGIZIO NO 4

MIMI BADO NI MDOGO TENA MWANAFUNZI SITAKIWI KUUMIZA KICHWA KUHUSU AJIRA, BIASHARA WALA PESA MPAKA BAADAE ..

Ndugu yangu kumbuka Siraha za vita zinatengenezwa wakati wa amani ili Zitumike kwenye vita

Jifunze kutengeneza mazingira mazuri ungali bado huna presha ya maisha.

Kama bado ni mwanafunzi endelea kujifunza kuhusu biashara au endelea kutengeneza connection za ajira ili ukitoka shule usihangaike sana kutembeza bahasha mtaani.

KISINGIZIO NO 5.

NATEGEMEWA NA WATU WENGI SIWEZI KUPUNGUZA MATUMIZI WALA KUWEKA AKIBA WALA KUFANYA MAENDELEO.

Ukiwa kwenye hali hii tumia presha ya utegemezi kuongeza kipato chako ili usikwamishe ndoto zako.

KISINGIZIO NO 6.

KWETU SISI NI MASKINI SIWEZI KUWA TAJIRI.

Asilimia 80% ya matajiri wote unaowajua walipata utajiri wao wakitokea familia maskini..

Ni asilimia 20% tu ya watu waliorithi utajiri, waliosaidiwa na waliotengenezewa mazingira ya kufanikiwa.

Kigezo cha kutoka familia maskini kisiwe chanzo cha kukata tamaa..

Bali iwe sababu ya wewe kupambana ili utoke kwenye hayo mazingira..

Ndiyo maana tunasema kama hukuzaliwa kwenye familia ya kitajiri hakikisha familia ya kitajiri inazaliwa kutoka kwako.

Je ni kisingizio gani kwenye hivi hautakiruhusu kikurudishe nyuma?

@kelvinkibenje
 
Back
Top Bottom