vidonda mji wa uzazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

vidonda mji wa uzazi

Discussion in 'JF Doctor' started by tunyi, Jun 17, 2012.

 1. t

  tunyi Member

  #1
  Jun 17, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mke wangu alijifungua mtoto mkubwa 5.5kg bahati mbaya, toka december 2011, anasema kuna mabadiliko asiyoelewa kama: 1)akikaribia kupata hedhi joto linapanda sana na anajisikia kama anaumwa akipima malaria hana
  2)masaa machache kabla ya hedhi anajisikia kama kuna kitu kinajizungusha chini ya kitovu ambayo yana ambatana na maumivu
  3)siku 3 za mwanzoni anatokwa na damu nyingi siku ya 4 na kwendelea damu inatoka kidogo kidogo yaani haikatiki, alipima hospitali akaambiwa ana vidonda kwenye mji wa uzazi akapewa dawa ya kumeza hedhi ikakatika, tatizo la hedhi mda mrefu lilijitokeza mwezi wa 5 na huu mwezi wa 6 anasema tatizo limerudi, hii ni siku ya7 damu inatoka kidogo kidogo haikatiki, na anapata maumivu chini ya kitovu. yanakuja na kupotea, kwa sasa hajatumia dawa yoyote
  SWALI: je hili tatizo linatibika na linaweza kuathiri uwezekano wa mke wangu kupata uja uzito? Tupo mwanza, naomba msaada tafadhali.
   
 2. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Nakushauri uende ukamuone daktari wa magonjwa ya wanawake (Gynacologist) ili amuevaluate vizuri mkeo. Maumivu ya tumbo la hedhi ni kitu cha kawaida, kwa wanawake wengine si makali lakini kwa wengine ni makali sana, pia hedhi kutoka kwa wingi kwa siku 3 za mwanzo kisha kufuatiwa na kidogo kidogo ni jambo la kawaida...wanawake wengine wanakauka haraka na wengine mpk siku 7..ni tofauti tu za kimaumbile.

  Sijawahi kusikia tatizo la kuwa na 'vidonda' kwenye mji wa uzazi au kizazi na kusababisha maumivu makali wkt wa hedhi au hedhi kuwa kwa siku nyingi...mpeleke shemeji kwa daktari wa wanawake akachunguzwe na kupatiwa ushauri/matibabu huskika.
   
 3. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  asante sana Dr. Riwa kwa ushauri wako ninaimani muhusiaka atachukua ushauri wako na kuufanyia kazi
   
 4. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Tafadhali kwa maswali na majibu ya kitaalam tembelea hii website: Wanetu.com :: Elimu kuhusu Ujauzito na Uzazi, Malezi na makuzi ya watoto, Afya ya watoto, Saikoljia, Tabia na Haki za Watoto
   
Loading...