Misahafu inasema hakuna mkamilifu LA hata mmoja chini ya jua..
Kama hakuna mkamilifu basi hata miundovitu vya mwanadamu sio kamili, kamilifu, timilifu....
Tukio lolote la kupanga huacha alama ama ushahidi mdogo kabisa unaopelekea uvumbuzi wa kushangaza sana wa tukio lote
Tone la damu
Kifungo cha shati
Unyayo ardhini
Risiti ya mafuta
Tairi za gari nknk ni vidhibiti vikubwa mno kwenye kutatua kesi zinazotatiza sana
Sakata la shambulio lililotakiwa kumuondoa Lisu duniani liko wazi mno.. Na mamlaka zikiamua kutenda kwa weledi hii ni kesi rahisi mno
Kinacholeta urahisi zaidi ni kwamba Lisu na dereva wake wote wako hai na wana kumbukumbu kamili, sura za watuhumiwa zimeganda vizuri kwenye bongo zao kwakuwa si mara ya kwanza kukutana ama kuonana kwa karibu kabisa
Magari yaliyotumika, rangi na namba zao, vinajulikana na ni rahisi mno kufuatilia....
Mawasiliano ya simu, namba, jumbe fupi, masafa ya mawasiliano, vituo(locations) muda, uelekeo na hata sauti, hivi vyote zinapatikana TCRA kwa amri ama ombi la polisi
Nyumba za wageni ama binafsi walizofikia, sehemu walizotembelea nk... Kumbuka hapa kuna watu washukiwa kwa majina kwamba siku ya tukio walionekana Dodoma.... Siku hizi kuna tekinolojia ya camera, nina hakika hawa watu wasiojulikana, kuna mahali bila wao kujua ama kutegemea walinaswa na camera... Hizi picha zipo kama hazijafutwa bado
Walinzi wa getini, kule area D, tukumbuke yale maeneo sio uswazi kunakaa viongozi hivyo ulinzi rasmi haukosekani
Maganda yale ya risasi yanaweza kutoa mwanga mkubwa kwenye hili ni rahisi mno kufuatilia na kujua silaha iliyotumika nknk kama tukiamua kutenda kwa weledi
Mchoro wa safari toka bungeni, eneo la maegesho muda waliotoka mpaka kuja kugundua wanafuatuliwa ni clue muhimu pia
Kuna mengi kwenye hili lakini tukiamua kutenda kwa weledi watuhumiwa wetu hawako mbali na sero ni suala na muda tu