Vidhibiti muhimu kwenye jaribio lililoshindikana la kutaka kummaliza TL

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,606
696,727
Misahafu inasema hakuna mkamilifu LA hata mmoja chini ya jua..
Kama hakuna mkamilifu basi hata miundovitu vya mwanadamu sio kamili, kamilifu, timilifu....

Tukio lolote la kupanga huacha alama ama ushahidi mdogo kabisa unaopelekea uvumbuzi wa kushangaza sana wa tukio lote
Tone la damu
Kifungo cha shati
Unyayo ardhini
Risiti ya mafuta

Tairi za gari nknk ni vidhibiti vikubwa mno kwenye kutatua kesi zinazotatiza sana
Sakata la shambulio lililotakiwa kumuondoa Lisu duniani liko wazi mno.. Na mamlaka zikiamua kutenda kwa weledi hii ni kesi rahisi mno

Kinacholeta urahisi zaidi ni kwamba Lisu na dereva wake wote wako hai na wana kumbukumbu kamili, sura za watuhumiwa zimeganda vizuri kwenye bongo zao kwakuwa si mara ya kwanza kukutana ama kuonana kwa karibu kabisa

Magari yaliyotumika, rangi na namba zao, vinajulikana na ni rahisi mno kufuatilia....
Mawasiliano ya simu, namba, jumbe fupi, masafa ya mawasiliano, vituo(locations) muda, uelekeo na hata sauti, hivi vyote zinapatikana TCRA kwa amri ama ombi la polisi
Nyumba za wageni ama binafsi walizofikia, sehemu walizotembelea nk... Kumbuka hapa kuna watu washukiwa kwa majina kwamba siku ya tukio walionekana Dodoma.... Siku hizi kuna tekinolojia ya camera, nina hakika hawa watu wasiojulikana, kuna mahali bila wao kujua ama kutegemea walinaswa na camera... Hizi picha zipo kama hazijafutwa bado

Walinzi wa getini, kule area D, tukumbuke yale maeneo sio uswazi kunakaa viongozi hivyo ulinzi rasmi haukosekani

Maganda yale ya risasi yanaweza kutoa mwanga mkubwa kwenye hili ni rahisi mno kufuatilia na kujua silaha iliyotumika nknk kama tukiamua kutenda kwa weledi
Mchoro wa safari toka bungeni, eneo la maegesho muda waliotoka mpaka kuja kugundua wanafuatuliwa ni clue muhimu pia

Kuna mengi kwenye hili lakini tukiamua kutenda kwa weledi watuhumiwa wetu hawako mbali na sero ni suala na muda tu
 
Acheni nadharia acheni kuhukumu acheni kunyooshea watu vidole wangapi walikuwepo dodoma bwana...yaani nyie mnataka watu wafanye kazi kulingana na matakwa yenu na mnataka tuu yule mtu fulani ndo atajwe kuwa mhalifu ili tuu mridhike hata kama sio kweli??
si haki na wala si sheria inavosema kama nyie mnavojinasibu wafuataji wa sheria
Nimemtaja mtu yeyote kwa jina hapa?
 
Acheni nadharia acheni kuhukumu acheni kunyooshea watu vidole wangapi walikuwepo dodoma bwana...yaani nyie mnataka watu wafanye kazi kulingana na matakwa yenu na mnataka tuu yule mtu fulani ndo atajwe kuwa mhalifu ili tuu mridhike hata kama sio kweli??
si haki na wala si sheria inavosema kama nyie mnavojinasibu wafuataji wa sheria
Sorry we unazungumzia mada gani tena mbn kama unalalamika na kujihami kuna nini huko?
 
What i believe you can not commit a serious crime.. Forensic evidence inaweza kupatikana kama wakitumia weledi
 
Umenena vyema mkuu ila Mungu naamini yupo atawaumbua wenye nia mbaya...

Wazungu wanasema KEEP CALM AND LET KARMA FINISH IT

Pole sana TunduLissu
May be not in this life... Tumwachie Mungu huku tukitafakari kwa umoja kwa pamoja....
 
Acheni nadharia acheni kuhukumu acheni kunyooshea watu vidole wangapi walikuwepo dodoma bwana...yaani nyie mnataka watu wafanye kazi kulingana na matakwa yenu na mnataka tuu yule mtu fulani ndo atajwe kuwa mhalifu ili tuu mridhike hata kama sio kweli??
si haki na wala si sheria inavosema kama nyie mnavojinasibu wafuataji wa sheria

Sasa ww hutaki wasiojulikana wajulikane, tunataka wajulikane bwana!
 
Acheni nadharia acheni kuhukumu acheni kunyooshea watu vidole wangapi walikuwepo dodoma bwana...yaani nyie mnataka watu wafanye kazi kulingana na matakwa yenu na mnataka tuu yule mtu fulani ndo atajwe kuwa mhalifu ili tuu mridhike hata kama sio kweli??
si haki na wala si sheria inavosema kama nyie mnavojinasibu wafuataji wa sheria
Unaposema waache nadharia unamaanisha nini hasa?

Unafikiri ni nani hapo kanyooshewa kidole?

Habari ya wangapi kuwa Dodoma au kutokuwepo inahusiana vipi na huu uzi?
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom