Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,916
Mada hii ni zao la mada hii ya kumbukumbu za ulimwengu
Kumbukumbu za ulimwengu (World Archives)
Ni wazi dunia inatembea na ulimwengu unahama.. Ama vyote viwili vinatembea na kuhama kwa wakati mmoja ama kwa nyakati tofauti na dereva wao mkuu anayewahamisha ama kuwatembeza ni muda
Haya ni matembezi yasiyoonekana mwendo wake na ni uhamisho usioweza kujionesha kwa maramoja bali kupitia wakati na nyakati haya hujidhihiri. Ni jambo la ajabu na kushangaza mno ukiweza kupiga taswira namna dunia inavyohama na ulimwengu unavyotembea
Kabla sijaendelea nisikuchanganye na haya mawili! Dunia na ulimwengu
Dunia ni yabisi kwa maana ya kwamba inaonekana
Ardhi (milima, mabonde misitu nk)
Maji (bahari, mito, maziwa na chemchem)
Ulimwengu ni mchanganyiko wa yasibi na visivyoonekana kwa maana ya
Mwanadamu binadamu
Viumbe hai vyote
Mitazamo na maono
Ufundi, ubunifu,ugunduzi sanaa na uumbaji wa majengo, miundombinu, barabara, vyombo vya usafiri nchi kavu, angani na baharini nk
Sayansi, fizikia, teknolojia nknk
Kwenye ulimwengu ndio unapata walimwengu na malimwengu
Combination ya hivi viwili huathiri kuhama ama kutembea kwake.. Kimoja kikiwa ni kwa asili na kingine kikiwa ni kwa matendo ya walimwengu
Kuhama na kutembea kwa dunia kisababishi ni matendo ya asili yasiyoweza kuzuilika kwa namna yoyote ile kama vile
Tufani/kimbunga
Mafuriko
Tetemeko la ardhi
Milipuko ya volcano na mawimbi ya bahari
Kuhama na kutembea kwa ulimwengo kisababishi ni matendo ya asili na matokeo ya athari za matendo ya walimwengu kama
Ukame
Biashara
Vita
Majanga ya asili
Magonjwa
Muingiliano wa vizalia na kikomo cha matumizi ya nyakati
Kwa wasomaji na wafuatiliaji wa mambo ya kale ya akilojia watakuwa wameona ugunduzi wa ajabu juu ya
Miji maarufu hapo kale iliyomezwa na bahari na kufukiwa chini ya vifusi vya mchanga
Maeneo ambayo hapo kale yalikuwa tambarare na uoto wa asili lakini sasa yamemezwa na kuwa bahari ama ziwa ama mto
Maeneo ya mashamba miji mikubwa na miundombinu ya kila aina lakini sasa yametelekezwa na kufunikwa na vichaka miti na mapori
Maeneo yaliyokuwa maarufu kwa sanaa, uhunzi uchoraji na ugunduzi mbalimbali sasa ni magofu na makazi ya wanyama na wadudu warukao na kutambaa
Maeneo yaliyokuwa ni misitu na mapori ama vilindi vya maji, mabwawa maziwa na hata bahari leo hii yamegeuzwa miji na majiji yenye viwanda mbalimbali makazi ya watu nknk
Kwa macho ya kawaida na uono wa haraka huwezi kuona hili lakini unapoanza kufuatilia mambo ya akiolojia unaweza kuona dunia na ulimwengu namna vinavyotembea na kuhama kwa namna ya ajabu kabisa
Ni jambo la kushangaza unapogundua ya kwamba baada ya muda fulani kupita walimwengu huchoshwa na eneo husika kutokana na majanga ya asili ama kufujwa na kuchakazwa na wao wenyewe na kuamua kutafuta maeneo mapya na kuyaendeleza upya..
Ulipo leo hapakuwa hivyo tangu asili.. Pengine palikuwa pori ama bahari ama ziwa nk halafu pakapata uhai wa walimwengu wakapachakaza wakapahama pakajitibu na kurudi kwenye asili yake pakawa pori na msitu tena leo hii pamevamiwa na kujengwa makazi ama shughuli zingine za kiuchumi..
Hapo hapatabaki hivyo milele patadumu kwa muda tu kisha pachahamwa...
Asili inazunguka na kutibu kila panapoharibiwa na walimwengu ama majanga ya asili ambayo sometimes ni kazi ya asili yenyewe ili watu waweze kuondoka kuepusha uharibifu zaidi
Je, asili ina macho? Ina masikio? Ina roho?

Hii ni mada ya mtiririko wa matukio ya kidunia yasiyo ya kawaida, yaliyohifadhiwa toka vyanzo mbalimbali kwa njia ya picha, maandishi ama vyote viwili. Lengo kuu ni kupanua ufahamu wa wale wote wanaoependa kufahamu matukio ya kidunia yaliyopita ambayo hawakupata nafasi kuyaona ama kuyasoma huko...
www.jamiiforums.com