Video yavuja inayodaiwa wafanyakazi wa TPA wakiiba vifaa vya gari. TPA yasema video ina mpango wa kuchafua taswira ya bandari

Magari ya kukodisha

JF-Expert Member
Sep 16, 2019
412
695
Wakuu habari

Kwanza nampongeza sana Rais wetu kipenzi Rais Magufuli hakika huyu kwetu sisi watanzania ni lulu.mungu amesikia kilio chetu sisi wanyonge kutuletea Magufuli.

Kuna video imerekodiwa wafanyakazi wabandari wanafanya wizi wakiiba kwa kufungua matair kwenye magari ya wateja yaliyofika kutoka nje jamani inauma sana ukiona video hii

Najiuliza kwanini kuna wachache hawaitakii mema nchi yetu. Kwanini kuna wachache wanaitia doa bandari yetu pendwa
Kwanini kunawachache wanataka kukwamisha juhudi za rais magufuli

Kwenye video hii baadhi yao sura zimeonekana waziwazi

Jamani tupaze sauti tumsaidie Rais inauma sana kuona rais wetu mpendwa anahangaika kuhakikisha Tanzania inakuwa kileleni halafu kuna wapuuzi wanamkwamisha

Video ninayo ila jamiiforums inasumbua Sana kuupload video


-- KANUSHO KUTOKA MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA--

Taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na wizi bandarini ni ya kupuuza na imelenga kuchafua taswira nzuri ya Bandari zetu na Tanzania kwa ujumla. Tukio husika halijafanyika kokote katika Bandari zetu hivyo wateja wetu wasiwe na wasiwasi.

Wateja/Wadau na Watanzania wote Taarifa zaidi kuhusiana na “videoclip” ya upotoshaji kuhusiana na wizi bandarini inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii itawajia muda sio mrefu.

TPA.PNG

Tanzania Ports Authority - TPA
HAKUNA VITENDO VYA WIZI BANDARINI!
MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA:
IJUMAA OKTOBA 11, 2019
DAR ES SALAAM.​
Mapema leo katika Mitandao ya Kijamii hasa katika Instagram, kumesambaa habari kwa njia ya Video na picha za Mnato zikionyesha tukio la Wizi wa Vifaa vya Magari ukifanywa na Vijana katika eneo linalosadikiwa kuwa ni moja kati ya Bandari za Tanzania.

Taarifa hiyo iliambatishwa na maelezo yanayosomeka kuwa ‘Aina ya wizi mpya Bandarini, Magari yanapofika wahuni hawa wanabadilisha matairi na Rims…yanawekewa ya zamani its Pathetic ‘.

Taarifa hiyo imezua taharuki kubwa, kusambazwa na kupata Wachangiaji wengi katika Mitandao ya Kijamii wanaoilaumu TPA kutokana na vitendo hivyo.

Kupitia taarifa hii, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inapenda kuujulisha Umma kuwa, Taarifa hizi si sahihi hata kidogo na kwamba hazistahili kupewa umuhimu wowote, zipuuzwe. Sababu za Msingi za Kanusho hili ni hizi zifuatazo:

Kwanza:
Namba za Makasha(Kontena) zinazoonyeshwa kwenye picha hizo haziko katika mifumo ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wala ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TANCIS). Hii inamaanisha kwamba, Kontena hizo hazipo Tanzania.

Pili:
TPA haina miundombinu katika Bandari zake kama inavyoonekana katika Video na Picha za ,mnato zilizosambazwa.

Tatu:
Bandari zetu hazina geti linalotumika kuondoa Shehena ya makasha na gari kwa wakati mmoja kama ilivyoonekana kwenye taarifa hiyo. Pia na gati na yadi zinazotumika kushusha na kuhifadhi mizigo hiyo haziko pamoja.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inapenda kuwasihi Wananchi wote na hasa Watumiaji wa Mitandao ya Kijamii kuepuka kutuma taarifa zenye kupotosha, kuchafua taswira ya Mamlaka na kuleta taharuki kwa Wateja, Wadau na Umma kwa ujumla.

Tunasisitiza kuwa, hakuna matukio wala Vitendo vya Wizi wa vifaa vya magari katika Bandari za Tanzania hasa baada ya TPA kufanya maboresho makubwa katika mifumo yake ya kiulinzi.

Tunawasihi Wateja wetu, Wadau na Umma kwa ujumla kuendelea kutumia Bandari zetu kwa uhakika kwa kuwa Sheria, Kanuni na taratibu za Uendeshaji wa Bandari zetu zinazingatiwa kikamilifu ambapo ulinzi na usalama wa mali za Wateja na Bandari unasimamiwa kikamilifu.

Imetolewa na:
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
 
Wakuu habari


Kwanza nampongeza sana rais wetu kipenzi Rais Magufuli hakika huyu kwetu sisi watanzania ni lulu.mungu amesikia kilio chetu sisi wanyonge kutuletea Magufuli.

Kuna video imerekodiwa wafanyakazi wabandari wanafanya wizi wakiiba kwa kufungua matair kwenye magari ya wateja yaliyofika kutoka nje jamani inauma Sana ukiona video hii

Najiuliza kwanini kuna wachache hawaitakii mema nchi yetu.kwanini Kuna wachache wanaitia doa bandari yetu pendwa
Kwanini kunawachache wanataka kukwamisha juhudi za rais magufuli

Kwenye video hii baadhi yao sura zimeonekana waziwazi

Jamani tupaze sauti tumsaidie mtukufu rais inauma sana kuona rais wetu mpendwa anahangaika kuhakikisha Tanzania inakuwa kileleni halafu kuna wapuuzi wanamkwamisha


Video ninayo ila jamiiforums inasumbua Sana kuupload video
Hata mimi nnayo ni mambo ya aibu wateja kila siku wanalalamika kuhusu matairi kumbe wezi wako bandarini, aisee JPM bdo una kazi sana na hii bandari, Mzee Kakoko aibu hivi si kuna CCTV Kamera jamani au zilizimwa ?
 
Katika mambo ninayomsifu Magufuli kuyafanya katika muda wake aliokaa "utawalani" ni hili la Bandari Kuu ya Dar es Salaam.

Kati ya sehemu nyingi zilizokuwa na uozo mkubwa mojawapo ni hapa.

Inawezekana bado pakawa pana dosari, lakini kazi kubwa imefanyika hadi hapa.

Na kama bado kuna watu wanaojiita kuwa wao ni waTanzania, na bado wakataka kuweka kampeni za kuididimiza bandari yetu, hao ni maadui zetu. Tunapaswa kupambana nao kwa kila njia.

Uongozi wa Bandari, haitoshi 'kukana'. Chunguza na chukua hatua zinazostahiri. Kama hawa watu bado mnao bandarini, kukana kwenu ni sehemu ya kuwalinda maadui wakubwa hawa wa taifa letu.

Mleta mada anajiita "Mexican Gang" lakini uandishi wake wa 'kinyonge' na wa 'kujikweza' unamdharirisha.
 
Back
Top Bottom