wale jamaa ni hatari sana wakija hapa bongo iknatakiwa wafanye kazi pale Takukuru halafu hosea aone mambo mapapa wote watadakwa
Mkuu Samoche labda umeisahau hii nchi. Nchi yetu haina tabia ya kuajiri 'the best'. Labda kuwe na TISS na TAKUKURU za binafsi.
Mimi nimekuwepo kwenye 'interview panel' za baadhi ya mashirika ya Umma, nimekuwa nikionekana mnoko kwa kuwa sikuzote nimegombana nao sana. Yaani the best 3 kwenye 'interviews' huwa hawapati ajira na ndio maana wengi wanaenda sekta binafsi.
TISS, TAKUKURU, TRA, POLISI, JWTZ, BOT,TPA, TANESCO, WIZARA ZETU, IKULU, PMO, TLB e.t.c kumejaa mazezeta ambao wana vyeti tu lakini uwezo hakuna. Ndio maana ukiwa na uwezo mkubwa mfano uwe kama hao jamaa zetu watakuona 'threat' hawakuchukui ng'o.
Mashirika na Taasisi za serikali ambazo kidogo wanachukua watu wa maana ni TCRA, EWURA, UDSM, PPRA na siku hizi baada ya Utouh NAO.