VIDEO - Wanajeshi wa Marekani Wazikojolea Maiti

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
6193702.jpg

Wanajeshi wa Marekani wakizikojolea maiti za wanamgambo wa Taliban

Jeshi la Marekani limekumbwa na kashfa kubwa baada ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan kunaswa kwenye video wakizikojolea maiti za wanajeshi wa Taliban nchini Afghanistan.
Jeshi la Marekani limeanzisha uchunguzi kufuatia kusambaa kwa video inayowaonyesha wanajeshi wa Marekani wakizikojolea maiti za raia wa Afghanistan ambao inasemakana walikuwa ni wapiganaji wa Taliban nchini Afghanistan.

Jeshi la Marekani limethibitisha kuwa video hiyo ambayo imesambaa kwenye mitandao mingi duniani ni ya kweli na jeshi hilo limetangaza kuwachukulia adhabu kali za kijeshi wanajeshi hao wanne ambao tayari wameishatambulika majina yao.

Video hii huenda ikawa pigo kubwa la pili kwa Marekani kufuatia skendo kubwa ambalo liliitingisha Marekani mwaka 2004 pale picha na video zilipowaonyesha wanajeshi wa Marekani nchini Iraq wakiwanyanyasa wafungwa kwenye jela ya Abu Ghraib.

Hivi karibuni wanajeshi 11 wa Marekani walipatikana na hatia ya kuunda kundi la wauaji ambalo bila ya sababu yeyote lilikuwa likiua raia wa Afghanistan wasio na hatia ambao hawakuwa hata na silaha yeyote ya kujilinda.

Angalia chini VIDEO ya wanajeshi wa Marekani wakizikojolea maiti za wanamgambo wa Taliban.

VIDEO - Wanajeshi wa Marekani Wazikojolea Maiti


<tbody>
</tbody>


chanzo. VIDEO - Wanajeshi wa Marekani Wazikojolea Maiti
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom