VIDEO: Wamasai wakimnyang'anya nyama simba.

VIDEO: Wamasai wakimnyang'anya nyama simba.

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,932
Ni mara nyingi nimeona watu wanaoishi karibu na mbuga za wanyama kufukuzwa humo kwa kisingizio kuwa wanaharibu mazingira. Kitu ambacho 'wataalamu' wetu wanachokisahau ni kuwa watu hawa wamekuwa wakiishi kwenye mazingira hayo kwa maelfu ya miaka na kuyamudu vizuri. Je 'wataalamu' wetu hawa wanaweza kuthubutu kufanya hiki bila kumuua simba kwanza?


[video=youtube_share;Z3AtVgiYKd8]http://youtu.be/Z3AtVgiYKd8[/video]
 
Mtu kwao, simba wamesalimu amri...

Inabidi viongozi wa Tanzania waione hii video kabla hawajauza nchi yote kwa waarabu wanaowinda Loliondo.

Ardhi tunayo na watu tunao, tulichokosa ni siasa safi na uongozi bora...

'Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne; watu ardhi, siasa safi na uongozi bora' (Mwalimu J.K.Nyerere - RIP)
 
Mtu kwao, simba wamesalimu amri...

Inabidi viongozi wa Tanzania waione hii video kabla hawajauza nchi yote kwa waarabu wanaowinda Loliondo.

Ardhi tunayo na watu tunao, tulichokosa ni siasa safi na uongozi bora...

'Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne; watu ardhi, siasa safi na uongozi bora' (Mwalimu J.K.Nyerere - RIP)




Ongezea na "Mzungu" Mkuu hata net tunasubiri atupe, hata tangazo kwenye TV mdhamini ni yeye.
 
Mere Propaganda by Park Authorities/ Conservators. Kwanza Wamasai hawali nyama pori ni mwiko ni taboo kwao. Tena kamwe hawali vibudu. Hata ingekuwa hivyo isingefanyika mbele ya Camera. Kuna kikosi cha Kamera nyuma yao, labda ni usanii, acting tu. Stupid compaign/ play by stupid Actors/ Mgt. Let them continue to coexist with wildlife as their basic human right.
 
Hii inatisha mkuu hawaogopi?njaa si mchezo
 
wamasai tuna kula nyama pori sema hadi kuwe na umuhimu wakufanya hivyo labda ngome wamekufa au wako wachache .....
 
wa dorobo sio wamasai

Dorobo ni wamasai maskini asie na mali meaning hana ngombe hata mmoja hawezi oa kisa hana mali kikubwa ni hana ngombe ,hawa ndio wana itwa ndorobo. Na hili jina huitwa na wamasai wenye mali

kwa hiyo ndorobo na masai n i kitu kile kile sema mali tu ndio inawatofautisha
 
Back
Top Bottom