barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Nimeiona hii clip ikizunguka mitandaoni.Inamuonyesha mwanamke wa makamo ya kati akitandikwa viboko vya kutosha tu makalioni na wanaume wenye nguvu zao.
Inaonekana ni "adhabu" dhidi ya mwanamama huyu,hata anapotaka kupinga kuchapwa;Wazee wa Kimila wanaamuru vijana waje wamkamate ili atege kalio na achapwe sawasawa.
Lafudhi za wazee hawa inaonekana ni wale wa "Kanda Maalumu".Huu ni ukatiri mkubwa sana dhidi ya akina Mama.Katika zama hizi kumchapa mwanamke viboko,tena vya makalio kwa idadi kubwa,si ni udhalilishaji tu,bali ni unyama na kinyume cha haki za binadamu.
Kuna wizara mtambuka,Kama Wizara ya Mambo ya Ndani ya ndugu yangu Mwigulu Nchemba pia Wizara ya Dada Ummy Mwalimu na Kituo cha Haki za Binadamu cha Madam Hellen Kijo Bisimba.Likemeeni jambo hili na wahusika wachukuliwe hatua na iwe fundisho kwa wengine wenye mila hizi za ajabu ajabu.